Wednesday, December 15, 2010

Sangara wameadimika ziwani Victoria


Mwaka 1985 nilibahatika kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi ya Rural Comminication kwenye chuo kilichojulikana Nyegezi Social pale Mwanza sasa hivi St. Agustino University. Siku moja tulipangiwa kusafiri na meli ya Chuo Cha Uvuvi iliyojulikana kama MV-Mdiria. Tulitumia siku nzima kuvua samaki kwenye ziwa Victoria. Tulivua samaki wengi sana wakubwa kwa wadogo. Samaki aina ya Sangara wakati huo walikuwa wengi na wakubwa lakini hawakuwa na soko. Nakumbuka baada ya safari ili ya kichuo kwa madhumuni ya kuandika habari tulipewa Sangara mkubwa mmoja ili tugaweane na sisi tulikuwepo watano tu. Hivi sasa Sangara ni adimu ziwani victoria wamevualiwa sana na kusafirishwa nchi za nje (mapande)sasa bei ya samaki haikamatiki jijini Mwanza.Hapa ndipo tulipofikia.

Saturday, December 4, 2010

Dr. Fidelis Myaka- Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo


Dkt Fidelis A.Myaka ndiye Mkurugenzi mpya wa Idara ya Utafiti na Maendeleo katika Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika kuanzia Januari 2010. Anashahada ya uzamivu katika nyanja ya agronomia.

Katika utumishi wake wa umma hasa utafiti ameshughilikia sana utafiti wa mazao jamii ya mikunde (mbazi,kunde,choroko) na kuongoza programu za utafiti katika kanda kama kiungo wa habari na mawasiliano katika kanda, mratibu wa utafiti katika kanda pamoja na kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Utafiti kanda ya Mashariki kuanzia mwaka 2008 hadi mwanzoni mwa mwaka 2010.

Anayo machapisho ya kitaalamu yapatayo 40 na amewahi kunyakua tuzo ya kwanza ya uchapishaji katika katika mashindano yaliyoandaliwa na Idara mwaka 2006. Elimu yake ya msingi ameipata katika shule zilizoko katika mikoa ya Kagera na Pwani. Sekondari 'O'level Pugu Sekondari na 'A' level Mkwawa Sekondari. Alirushwa kutoka shahada ya Kwanza hadi Uzamivu. Waswahili au hata wachaga huita'Kichwa.'

Anapendelea sana masuala ya TEKNOHAMA.

Dr.Kafiriti na mamaa


Muda wa sherehe za kuagwa wastaafu. Dr. Elly Kafiriti - Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo kanda ya Kusini alikuwa makini kabisa kwenye meza yake pamoja na mkewe. Kanda hiyo iliwazawadia vifurushi vya korosho wastaafu wote pamoja na viongozi wapya wa Idara wa lioteuliwa akiwemo Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Dkt. Fidelis Myaka.

Champaigne kwa waagwa


Kinywaji kwa wanaoagwa kwanza.

Nilifungua champaigne


Kama sikosei hii ni champaigne yangu ya nne kuifungua katika tafrija mbalimbali. Kizibo kilirushwa juu kabisa. Naanza kuwa mtaalamu.

Wazee wa EAAPP


Wageni waalikwa walikuwa ni wengi kutoka vituoni na makao makuu pia hata wazee wa EAAPP (Rice Centre of Excellence) walikuwepo.

Tunywe kwa afya zetu



Unapokuwa na furaha unakunywa na kula na ndugu zako, marafiki zako, wafanyakazi wenzako na wengine. Ndivyo wanavyosema wastaafu waandamizi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo walioagwa hivi karibuni.

Familia ya Chambi


Wengi huwa wanauliza hivi pale Kibaha unafanyika utafiti wa miwa hivi wanafanyaje? Swali hilo ni rahisi kwa Mzee Juhudi Chambi. Ingawa amestaafu lakini kutokana na maarifa, utaalamu na uzoefu katika utafiti wa miwa swali hili ni rahisi kwa Mzee Chambi. Muda wake mwingi katika utumishi wa umma ametumikia katika utafiti wa miwa pale Kibaha akiwa mratibu wa utafiti wa zao hilo pamoja na uongoziwa Kituo cha Utafiti wa Miwa-Kibaha. Mzee Chambi ni mtu wa QUALITY kama alivyosimulia mwenyekiti wa Sherehe za kuwaaga wastaafu Bw. Ninatubu Lema. Ni mtaalamu wa uzalishaji wa mazao (Plant Breeder). Ni mkarimu sana na mcheshi ni mtu wa familia kama anavyoonekana pichani akiwa na familia yake katika tafrija ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara tarehe 19 Novemba 2010. Juhudi zake katika zao la miwa ni kuongeza uzalishaji wa zao la miwa bora kwa kutatua tatizo la mbegu bora zenye kuvumilia magonjwa na wadudu.

Timothy Kirway

Kwa wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo jina la Kirway si geni. Kwanini? Kirway aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Utafiti wa Mifumo ya Kilimo na Uchumi Jamii kama ilivyo kwa wafanyakazi waliozaliwa mwaka wa 1950 alistaafu rasmi katika utumishi wa umma mapema mwaka huu. Mzee Kirway atakumbukwa zaidi kwa kuchapa kazi na umakini wa kazi na hasa ufuatiliaji na utunzaji wa kumbukumbu. Daima alisimamia haki na usawa. Ndiye hasa mwanzilishi wa utafiti shirikishi na mifumo ya kilimo hapa nchini.Pichani katika kumbukumbu ya kuagwa kwake akiwa na mkewe katika viwanja vya KILIMO II tarehe 19/11/2010.

Dr. Shomari Shamte mstaafu wa Kanda ya Kusini


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafiti kanda ya Kusini,Dr. Shamte Shomari amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria katika mwaka wa fedha 2009/10. Dr. Shomari atakumbukwa zaidi katika utendaji kazi wake kwa umma kwa zaidi ya miaka 30 katika kuboresha utafiti wa korosho hapa nchini. Ndiye Mkurugenzi mwanzilishi wa kanda ya kusini na pia ameboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya kazi katika kituo cha Utafiti wa Kilimo-Naliendele. Tarehe 19 Novemba 2010 Wizara iliandaa tafrija ya kuwaaga wastaafu waandamizi akiwemo Dr. Shomari. Pichani Dr. Shomari akiwa ametulia tuli na mkewe.

Watafiti waandamizi wastaafu waagwa

Tarehe 19 Novemba 2010. Idara ya Utafiti na Maendeleo iliyoko katika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika iliwaaga wastafu waandamizi kwa mwaka 2009/10. Tafrija hiyo ya nguvu ilifanyika kwenye viwanja vya makao makuu ya wizara KILIMO II. Walioagwa ni Dr. Mohamed Msabaha (Pichani akiwa na mkewe)aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi - Utafiti wa mazao, Bw. Timothy Kirway aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafiti Mifumo ya Kilimo na Uchumi Jamii, Dr. Shamte Shomari aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda wa Utafiti- Kusini, Dr. Ally Mbwana aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda wa Utafiti-Kaskazini na Bw. Juhudi Chambi, Afisa Mfawidhi kituo cha Utafiti wa Miwa na Mratibu wa Utafiti wa Miwa -Kibaha. Dr. Msabaha atakumbukwa zaidi katika ubunifu wake wa kukifanya kituo cha Uyole kuwa mfano wa kuigwa katika uzalishaji wa mbegu za mazao hasa mahindi na maharagwe. Aidha katika utendaji kazi wake alisimamia ubora wa kazi na kuvumiliana.