Friday, March 25, 2011

Hii ni Kwaresima


"Kumbuka wewe ni mavumbi na utarudi kuwa mavumbi"

Jumatano ya majivu


"Wewe ni mavumbi na utarudi kuwa mavumbi"

Kabwe utajiri mkononi


Tanzania tunao utajiri mkubwa wa mali asili hasa madini. Madini ya chuma yanapatikana kwa wingi nchini mwetu. Pichani Mbunge Zitto Kabwe akilifurahia dini la chuma. Tatizo ni nini? Teknolojia? Mipango au?

Wote tutafika kwa babu?


Wanaokwenda Loliondo kwa babu kupata KIKOMBE ni wengi. Viongozi na wananachi wa kawaida, matajiri na mafukara, rika na jinsi mbalimbali. Kufika Loliondo kila mgonjwa hutumia aina ya usafiri anao umudu ili mradi apate Kikombe cha Babu!

Wednesday, March 23, 2011

Tangazo la kudhalilisha mweusi

Kama umewahi kubahatika kusafiri na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini (SAA). Kabla ya ndege kuruka huwa linatolewa tangazo kupitia video clip linalowaeleza abiria jinsi ya kufunga mikanda, kuweka mizigo midogo kwenye cabin na mambo mengine. Kinachonishangaza ni ile sehemu inayoonyesha abiria mweusi asiye mwangalifu aliyekurupuka na kuweka mizigo kwenye cabin na kisha kumporomokea abiria mzungu (mweupe) na kumuumiza. Kwanini mzembe asiwe mzungu?

Kisemvule Sports hoi kwa Wakali Kwanza

Timu chipukizi ya Wakali Kwanza kutoka Kisemvule imeiadhabu timu kongwe ya kijijini hapo Kisemvule Sports Club kwa magoli 2-0 kwenye fainali ya 'KISEMVULE CUP' iliyochezwa kwenye kiwanja cha Kisemvule Magengeni siku ya Jumapili tarehe 20/03/2011. Kwa ushindi huo washindi wamejinyakulia jezi na kikombe cha mashindano hayo. Nayo timu ya Kisemvule Kids Soccer Club imeibuka mshindi wa tatu na kukabidhiwa zawadi ya mpira mmoja.

Ubunifu unatakiwa kukabili tatizo la Mbagala

Kwa kipindi hiki ambacho mvua nyingi zimeanza kunyesha,kero kubwa imeibuka kwa watumiaji wa barabara ya Kilwa kutoka Zakhem hadi Mbagala Rangi Tatu. Kipande hicho cha barabara kimeharibika sana. Hakuna maelezo sahihi yaliyokwishatolewa ili wananchi wafahamu kwanini kipande hicho hakikarabatiwi. Ubunifu mdogo tu wa kunyonya maji,kuchonga barabara na kisha kufukia mashimo kwa kifusi kikali hata kama hakuna lami ingesaidia kutatua tatizo.

Watamani Kiswahili

Katika mazungumzo yangu na mmoja wa wakilishi wa Warsha ya Kujenga Uwezo katika Utafiti wa Kilimo Afrika katika nchi za SADC alionyesha mapenzi makubwa katika lugha ya Kiswahili, huyu alikuwa kitoka nchini Swaziland.Kwa maoni yake angependa kuona kuwa Kiswahili kinatumika katika nchi za SADC.

Tuesday, March 1, 2011

Migomo Migomo


Wimbi la migomo kwenye vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini limezidi kupamba moto baada ya wanachuo wa IFM kugoma kufanya mtihani hapo jana. Migomo mpaka lini?

Tanzania's first university graduate


Mwl. Mathew Douglas Ramadhan is the first Tanzanian university graduate, education officer and black secondary school headmaster. Born on September 11, 1915 in Zanzibar, Mwalimu Mathew graduated with B.A. (Econ) in 1951.

Aibu!


Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Bunda hivi karibuni alishushwa jukwaani na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Wilbroad Slaa baada ya wafuasi wa chama hicho jimboni humo kumtuhumu kuwa alihongwa wakati wa kampeni za uchaguzi na kusababishwa chama hicho kushindwa. Aibu!

Mrema ni Doctor


Tarehe 28/2/2011 itakuwa siku ya kukumbukwa na Mr. Agustine Mrema, Mbunge wa Vunjo kwa kutunukiwa shahada ya Udaktari wa heshima na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Omega Global cha Afrika ya Kusini, Profesa Nehemia Sibiya. Sasa Mrema atatumbulika kwa Dr. A.Mrema!