Saturday, May 21, 2011

Furaha Guest House


Ukitokea Mikumi kwenda Iringa baada ya kumaliza kona za Iyovi na kuvuka daraja la mto Ruaha, pale Ruaha Mbuyuni tazama upande wa Kushoto utakutana na Guest safi Furaha Guest House! Chumba Tshs 3,000/= kwa siku (nimeambiwa).

Wanajitathmini


Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wafanyakazi wa kituo cha Utafiti Uyole wanaoshiriki kwenye programu ya EAAPP-Regional Rice Centre of Excellence (Utafiti wa Mpunga na Ngano) walivyojitathmini kutokana na uwezo waliokuwa nao ili kuandaa programu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo sehemu zanye mapungufu

Anamwagilia kitalu

Miche ya mite aina mbalimbali inayostahimili hali ya hewa Nyanda za Juu Kusini huoteshwa pia kituoni Uyole. Moja ya miche hiyo ni mipaini (Pines). Maji ni muhimu kwa miche kukua vizuri.

Hali ya hewa Je?


Kituo cha kupima hali ya hewa kipo Uyole na taarifa za kila siku hutolewa. Hebu soma mwenyewe ilivyokuwa tarehe 16/5/2011. Kipupwe hakijaanza Mbeya.

Taarifa hutolewa


Kila kitu kiko wazi matangazo hubandikwa kwenye mbao za matangazo mara tu unapoingia kituoni hakuna kusingizia kuwa sifahamu. Huu ni utaratibu mzuri wa mawasiliano uliopo katika kituo cha Utafiti wa Kilimo Uyole.

Utafiti wa unaendelea




Utafiti wa mazao mbalimbali unaendelea katika kituo cha utafiti Uyole yakiwemo mazao ya mahindi, maharage na ngano.

Unapoingia kituo cha Utafiti wa Kilijmo Uyole


Hapa ndipo yalipo makao Makuu ya Utafiti wa Kilimo kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Uyole, Mbeya. Kituo hiki ni maarufu kwa utafiti wa mahindi, maharage, mpunga na mbogamboga.

Thursday, May 19, 2011

Anawasiliana na Dafur


Tukiwa Ifakara Omy aliwasiliana na shemeji (Mama Lulu)aliyeko Dafur. Faida ya mawasiliano hiyo.

Nina papai langu


Ilibidi nipige picha kabla ya kuvuka mto Ruaha kuelekea Mikumi tarehe 18/5/2011. Maji ni mengi na papai ni tamu.

Mbega Resort


Moja ya Hotel nzuri mpya na ya Kisasa mjini Ifakara. Mbeya Resort. Chumba Tshs 30,000/- bed and breakfast. Mambo yote kama majuu.

Anawasiliana na Tegetero

Tuliokuwa Ruaha. Kaka Jakka (Fr) alipata simu kutoka nyumbani Tegetero, Morogoro. Vilongalonga vimerahisisha mawasiliano kweli kweli.

Karibu Bw. Mdogo

Fr.Jakka akishughulika kutuandalia chakula cha mchana tulipopita kwenye Parokia yake Ruaha kumsalimia tukielekea KATRIN-Ifakara tarehe 17/5/2011.

Saturday, May 7, 2011

Kisemvule na michezo


Moja ya shughuli zinazofanyika katika kijiji cha Kisemvule kilichopo wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ni Michezo. Mwezi Machi mwaka huu Kijiji kilitoa Kikombe kwa mshindi wa Kwanza Timu ya Wakali Kwanza baada ya kuifunga Klabu kongwe ya kijijini hapo Kisemvule Sport. Pichani viongozi wa Kata na Kijiji wakiangalia mechi ya fainali.

Kuku Kishingo

Niambie utamu wake!

Familia

Kila inapobidi ni vizuri kuwa pamoja na familia.Pichani familia baada ya Ibada ya Ijumaa Kuu Parokiani Vikindu.

Kuku wa kienyeji


Wengi hupenda kula kuku wa kienyeji lakini hatufugi. Kuku wa kienyeji ni mtamu!

Kardinali Pengo

Kofia na fimbo ni ishara ya Mamlaka.

Ujumbe wa Pasaka kutoka Kwa Kardinali Pengo

Ibada ya Pasaka Parokiani Vikindu iliendeshwa na Kardinali Polycarp Pengo (Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam). Ujumbe wa Baba Kardinali Pengo ulikuwa ufufuko wa Bwana Wetu Yesu Kristu haupaswi kuhojiwa. Hii ni moja wa vipaji vyake Mungu.

Monday, May 2, 2011

Hawa ndiyo wakali wa Kise KIDS Soccer Club ya kijiji cha Kisemvule. Ni timu ya mpira wa miguu inayocheza kandanda safi.

Maria Banzi


Maria I.J.Banzi akiwa nyumbani kwao mbele ya bomba la kijiji cha Kisemvule,Mkuranga Pwani.

Mwenzangu Pokea pete hii

Ndivyo anavyosema Bi Valentine wakati alipokuwa akimvisha pete ya harusi mumewe Bw. Valentine siku ya tarehe 25/4/2011 Parokiani Vikindu.

Miaka 70 ya Ndoa

Mzee Mathias na mkewe katika ibada ya maadhimisho ya miaka 71 ya ndoa yao iliyofanyika siku ya Jumatatu ya Pasaka(25/4/2011)katika Parokia ya Vikindu, Jimbo la Dar Es Salaam.