Wednesday, June 29, 2011

Morogoro inapendeza

Hapa ni Morogoro pale Kola karibu na makaburi njia ya kwenda nyumbani Matombo.

Wednesday, June 22, 2011

Trekta letu

Sijatembelea maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea hapa jijini katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Lakini kitu kilichonivutia ni kusoma ndani ya blog ya Mjengwa kuwa kuna trekta lililobuniwa na Mtanzania ambalo lina uwezo wa kulima ekari 5 kwa siku. Linaweza kusaga nafaka na pia kutoa nishati ya umeme. Haya ni maendeleo makubwa katika nyanza ya sayansi na Teknolojia. Trekta hili lilibuniwa na CARMATEC-Arusha mwaka 2008 na Dr. Patric Jonathan

KATRIN kujengewa uwezo


Kituo cha Utafiti - KATRIN kilichopo Ifakara mkoani Morogoro kinatazamiwa kuwa Kituo Mahiri cha Utafiti wa Mpunga (RRCoE)katika Afrika Mashariki na Kati chini ya Programu ya Kuendeleza Tija katika kilimo Afrika (EAAPP).Picha ya juu Mratibu wa Mradi wa Kituo Mahiri Bw. Nkori Kibanda akitoa maelezo ya jinsi mradi huo unavyotekelezwa na mahitaji ya kujengewa uwezo hasa kwa watumishi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufasaha na hatimaye kufanikisha lengo.

Utafiti wa Mifugo Uyole - Mbeya


Dkt. Pilika Mwakilembe akifanunua jambo ofisini kwake Uyole,alipotembelewa na Banzi wa Moro hivi karibuni.

ASA-Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Tayari Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) wameshaandaa. Mkataba wa Huduma kwa Mteja. Ndani ya Mkataba imewekwa bayana huduma zitolewazo na Wakala hii na jinsi huduma anavyopaswa kuhudumiwa. Lengo ni kutoa huduma za mbegu zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kuongeza tija katika kilimo.

Dakawa-Kituo cha usambazaji wa Teknolojia


Kituo kipya cha usambazaji wa teknolojia za kilimo kimejengwa Dakawa-Morogoro kwa msaada wa Serikali ya China kimefunguliwa mwaka huu na Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

SARO- Nyumbani kwake Cholima-Dakawa


Moja ya vituo vya Utafiti wa Kilimo kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kituo hiki kilizinduliwa mwaka 1985 na Rais wa awamu ya Kwanza Mhe. Julius K.Nyerere. Kimejengwa kwa ushirikiano na wa Jamhuri ya Korea Kaskazini. Shughuli zake kuu ni utafiti wa mpunga. Aina ya mbegu ya mpunga SARO nyumbani kwake ni hapa.

Ni madaraja



Ukisafiri kwa kutumia gari kutoka Mikumi kwenda Ifakara kitu kimoja ambacho ni dhahiri kukiona ni madaraja. Mojawapo ni hilo hapo juu la Mikumi ambapo reli inapita juu na hili la kulia la Ruaha.

Friday, June 17, 2011

Chini ya Daraja la Umoja

Ukitembelea kijiji cha Mtamba swala-Nanyumbu na kuliona daraja la Msumbiji utashangaa sana.Pichani- Mshana,Kadeng'uka na Banzi chiniya daraja la Umoja.

Mgahawa wa Kituo cha mabus-Masasi

Huu ni mgahawa maarufu Masasi.Hapa nilipata chapati moja,na supu ya kuku wa kienyeji!

Zawadi kutoka Msumbiji

Kweli imetengezwa Msumbiji!

Nangurukuru

Hapa ndipo panaitwa Nangurukuru ni maarufu kwasamakiwakukaanga. Ni kituo maarufu sana wakati unaelekea Lindi kupitia barabara ya Kilwa. Kiko njia panda ya kwenda Kilwa Masoko. Angalizo usikurupukekununua samaki wakukaanga hovyo hovyo hapa na kubugia. Mimi yalinikuta!

Nyama choma na supu ya mbuzi ok!


Endapo utafiti wa kupata aina bora za mbuzi utafanikiwa,tutaongeza uzalishaji wa mbuzi na kufaidi matunda yake kama hivi.

Mbuzi wa utafiti - Mnima


Hawa ni mbuzi wa utafiti waliopo kwenye kituo cha majaribio ya utafiti kilichopo Mnima huko Newala.Hapa ndipo panapotarajiwa kutoa aina mpya ya mbuzi kwa miaka ijayo kwani ili kupata aina ya mbuzi kwa kuzingatia sifa zinazotakiwa utafiti huchukua muda mrefu.Ili kufikia lengo lazima uwekezaji katika utafiti uongezeke zaidi kwa kuongeza wataalamu na vitendea kazi.

Unapoingia mjini Lindi

Mara unapoingia mjini Lindi ukitokea Dar unapata mandhari hii.Kwambali upande wa kushoto ni bahari ya Hindi.

Tunasali na kutafakari

Ndivyo tufanyavyo Jumuiya ya Mt.Joseph- Parokia ya Vikindu.Kila Jumamosi jioni tunakutana kwenye nyumba ya mwana jumuiya mmoja tunasali na kutafakari neno la Mungu kwa pamoja. Jumuiya zinatuweka karibu zaidi.Tunajifunza mengi na kusaidiana.

'Kocha'akiwakambini Nyegezi Mwanza

Kocha anapokuwa kambini na wachezaji na huku kukiwa na mechi ngumu kesho jioni.Kwa hali hii hakuna mategemeo ya ushindi.

Kise Kids wanasubiri zawadi

'Kise Kids Soccer Club' ni Klabu ya soka ya vijana iliyopo kijijini Kisemvule,Vikindu,wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.Mapema mwaka huu iliweza kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano yaliyoandaliwa na kijiji cha Kisemvule.Pichani wachezaji na washabiki wakisubiri zawadi ya mshindi wa tatu (walipata mpira mmoja).

Daraja la Umoja - Msumbiji naTanzania

Hili ni daraja la kujivunia kati ya nchi mbili maskini za dunia ya tatu- Tanzania na Msumbiji.Limejengwa kwa fedha zetu wenyewe kwa kutumia wa wataalamu kutoka China.Pichani Omary Shomari akiwa kwenye daraja hilo alipotembelea kijiji cha Mtambaswala mpakani mwa Tanzania na Msumbiji,wilayani Nanyumbu.

Tunakwenda kusali kwenyeJumuiya

Baba na mwana wanaelekea kwenyeJumuiya huko Vikindu Kisemvule.Jumuiya zetu ziko mbalimbali sana kutoka nyumba hadi nyumba.

Na hii ndiyo familia yangu

Maisha poa kabisa!

Mamaa ananipa pongezi

Mamaa alinipa pongezi ya Birthday niliporudi nyumbani!

Tuesday, June 7, 2011

HA! LEO 'BIRTH DAY' YANGU


Leo ni 'Birth day yangu'. Na leo natimiza post ya 1000 katika blog yangu. Namshukuru Mungu kwa kunipa uhai hadi kufikia siku ya leo Jumanne 7/6/2011. Nimefurahi pia kuingiza post ya elfu moja tangu kuanza kwa Blog hii. Mwezi huu ni mwezi wa mafanikio kwangu kwa mara ya kwanza kwa mwezi mmoja nimeingiza zaidi zaidi ya post 60!

Monday, June 6, 2011

Hili ndilo daraja la Mkapa

Daraja hili ni refu sana na huwezi kulinganisha na daraja la mto Mfizigo lilipo Matombo, Morogoro vijijini.Ni kazi nzuri ya Rais wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.Ndivyo anavyothibitisha Mtafiti wa Kilimo Bw. Laurent Kadeng'uka alipotembelea mikoa ya Mtwara na Lindi hivi karibuni.

Na huu ni mgahawa

Kuna mahali pa kupata chakula na vinywaji baridi na vikali! Hapa ni Mangaka, Nanyumbu.

OFISI YA DC NA DED NACHINGWEA


Moja ya majengo mazuri ya utawala wilayani. Hapa ndipo yalipo makao makuu ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Nachingwea.

Ng'itu bus la kwanza


Tulikuwa tunajiuliza kuna nini? Bado hatujakutana na mabus kutoka Dar! Mara hilo Ng'itu, bus la kwanza maeneo ya Namwage.

Katibu wa muda


Katika kuandaa taarifa, ilibidi kuinamia Laptop.

Hakuna kulala tunaandaa taarifa


Ukiwa na Dkt. Mkangwa, hakuna kulala. Unamaliza kazi ya field. Usiku lazima timu ikutane kuandaa taarifa.

Joan Kasuga katikati ya daraja la Umoja

Hili ndilo daraja la umoja linalounganisha Msumbiji na Tanzania.

Mlipeni dada twende zetu

Ndivyo anavyosema Mtafiti Tenga akiwahimiza wanatimu kumlipa dadalishe wa pale Mangaka, Nanyumbu.

Saturday, June 4, 2011

Mnima Field Site

Timu ya Kupelemba ilifika Mnima Livestock Field Site kilichoko Newala. Hapa tuliona mbuzi na kupata supu ya mbuzi. Unakumbuka zile picha? Basi ndo hapa! Ofisi nzuri, samani nzuri za mninga kutoka misheni ya Ndanda.

Chumba changu Tandahimba

Kitanda, TV, Fan,na sofa nililipia Tshs 12,000/- kwa usiku mmoja. Cha kufurahisha sana asubuhi kwenye mgahwa wa karibu ni supu ya kuku wa kienyeji.Tandahimba raha tupu siyo adhabu. Ila tulipokuwa safarini usiku kuelekea Tandahimba watu walikuwa wakipiga kelele- CCM hao!

Marafiki

Kushoto ni John Tenga na kulia ni John Banzi wote ni wekundu wa Msimbazi. Ila kwa bahati mbaya tu kwa kuwa walikuwa field imebidi waweke yellow kidogo!

Shabiki wa Liverpool


Starehe, ushabiki na ukokrochi popote. Banzi wa Moro ilimnasa huyu pale Mangaka,Nanyumbu, wakati tulipopata 'Lunch' mara baada ya kutoka kijiji cha Naharawa.

Karanga bomu


Wakulima kupitia utafiti wanafahamu zipi ni karanga bomu. Mimi na wewe hatujui. Picha juu endapo utachagua fungu la karanga kwa kuangalia ukubwa wa karanga, basi utakuwa umeliwa. Ndani hamna kitu. Mimi nilicheza pata potea pale Naharawa na kuchagua karanga bomu!

Striga-Kiduha


Gugu chawi!Ni hatari kwa mazao ya nafaka hasa mahindi na mtama. Gugu hili tumelikuta kwenye moja ya mashamba ya utafiti kijijini Nangaka, wilaya ya Nanyumbu.

Tunatambulishwa kijijini


Unamfahamu huyo mwenye cap?

Masasi-Mtambaswala



Bus hilo linafanya safari zake kutoka mjini Masasi hadi Mtambaswala kupitia Mangaka. Coaster safi.Mtambaswala ni kijiji kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Anapoibiwa mkulima


Ndiyo mihogo imepangwa vizuri kwenye gari. Ni mihogo mizuri. Nenda kamuulize mkulima amepata shilingi ngapi? Hili lori limetoka wilaya ya Rufiji.

GUEST PERHAPS!


Hii ni guest ya Masasi. Inavutia kwa nje lakini in poor management.Hapa ndipo tulipoingizwa mkenge tuliambiwa kuna internet service kwa wateja free of charge. Air conditioners zipo lakini ziko disconnected, matanki ya maji ya mato yapo lakini disconnected. Chai asubuhi saa 2.00. Malazi kwa siku ni kati ya Tshs 30,000- 40,000/=. Basi hii ni Guest Perhaps! Angalia hiyo computer tuliyoingizwa nayo mkenge.

J.Banzi

Chumba changu Mtwara


Bonge la Master bedroom!

Nimepata mchumba Msumbiji


Tuliweza kuwasiliana vizuri tu kwa lugha ya Kiswahili. Mambo, poa. Ah kumbe ni ni Mmakua tu wa Msumbiji wapo mpakani mwa Msumbiji na Tanzania. Kijiji cha kwanza baada ya kuvuka daraja la Umoja.

Friday, June 3, 2011