Friday, August 19, 2011

Banzi wa Moro


Chini kulia miaka 37 iliyopita nikiwa Njombe Secondary School - FORM ONE. Nyuma yangu ni Library ya shule!Juu kushoto mwaka huu nalishwa keki na Mamaa- nyumbani Kisemvule, Mkuranga, Pwani.Taja tofauti 5 za picha hizo.SHUKRANI KWA MUNGU


Tuesday, August 16, 2011

Lugaluga wanalima na kuuza




Kama tunataka wakulima wetu wasinyonywe na wakione kilimo kinalipa wazalishe na kuuza wenyewe huku wakimiliki zana za usalishaji na ikiwezekana na miundo mbinu. Lugaluga wameshaanza kufanya hivyo. Kinachowakwimisha ni miundo mbinu ya umwagiliaji na barabara safi za mashambani. Hilo linatakiwa kufanyiwa kazi.

Viongozi na wanachama wa Lugaluga



Namimi nimo ni mwanachama mwanzilishi wa Lugaluga.

Lugaluga walikuwepo 8/8




LugaLuga Agricultural Marketing and Cooperative Society kulikuwepo kwenye maonyesho ya wakulima ya mwaka 2011 kwenye uwanja wa maonyesho-Morogoro. Walioneysha zana wanazotumia (matrekta madogo na makubwa) ambayo wanamiliki wanachama kupitia Ushirika wao. Bidhaa wanazozalisha- Mpunga, alizeti na mahindi. Hao ndiyo Lugaluga waliojizatiti kuondoa umaskini kupatia Ushirika.

Wakorea wanataka kuibadilisha Pangawe






Katika muda wa miaka mitano ijayo, Wakorea wanataka kukibadilisha kijiji cha Pangawe kilichopo wilaya ya Morogoro vijijini kuoenakana cha kisasa zaidi kikiwa na miundombinu ya umwagiliaji, barabara za mashambani, shule bora ya msingi, maji safi huduma ya afya, umeme na huduma nyingine. Tusubiri tuone. Kazi hiyo inafanywa na KOICA-Korea Interanational Cooperation Agency.

Tunatarajia kupata aina mpya ya kunde


Watafiti wa kituo cha Utafiti cha Ilonga-Kilosa, Morogoro wanatarajia kutoa aina mpya ya kunde ifikapo mwishoni mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2012.Hilo limebainika katika maonyesho ya NaneNane ya mwaka huu huko Morogoro.

Banda la utafiti wa Kilimo mwaka 2011




Kwenye banda la maonyesho ya Utafiti kanda ya mashariki. Tekenolojia mbalimbali zilionyeshwa ndani na nje ya banda.

Banda jipya la Utafiti - Morogoro

Wizara ya Kilimo na Chakula imeanza kujenga banda jipya la Utafiti na Maendeleo katika viwanja vya Nane Nane - Morogoro na kuanza kutumika katika maonyesho ya mwaka huu.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti kanda ya Mashariki - Dr. Chaboba Mkangwa, banda hilo likikamilika litakuwa likitowa huduma za mikutano na shughuli nyingine muhimu za Wizara katika viwanja hivyo.

Hivi sasa Kibungo Juu


Baada ya kufundishwa teknolojia mbalimbali za kilimo bora na hifadhi ya ardhi. Wakulima wa Kibungo Juu wanaendesha kilimo chenye tija. Wanalima kwenye miteremko na kuhifadhi ardhi. Ona maharagwe yalivyostawi!

Kilimo cha zamani-Kibungo


Enzi hizo wakulima wa Kibungo Juu walikuwa wakilima kilimo cha aina hii kwenye miteremko ya milima.

Tunalisha na kuhifadhi ardhi


Majani yajulikanyo kwa jina la mabingobingo yanatumiwa na wakulima wa Kibungo Juu wilayani Morogoro vijijini kwa kulishia mifugo hasa mbuzi na nguruwe pamoja na kuhifadhi ardhi. Pichani mkulima akimuonyesha Banzi wa Moro majani hayo katika banda la Maonyesho ya Idara ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi.

Kijana na Kilimo cha Nyanya- Kibungo


Kijana huyu aliyekuwa kwenye banda la maonyesho la Idara ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi alinieleza jinsi alivyojifunza kilimo bora cha nyanya juu ya milima ya Kibungo na kusema kuwa kwa mara ya kwanza magari ya mizigo yalipanda mlimani kubeba mazao ya mbogamboga ambayo yamemsaidia sana kuongeza kipato chake.Pichani akiwa kwenye bustani ya maonyesho ya nyanya.

Utunzaji wa Ardhi ni pamoja na ufugaji bora


Banda la mbuzi la wakulima wa Kibungo Juu kwenye maonyesho ya Nane Nane 2011 mkoani Morogoro ndani ya Banda la Idara ya Matumizi na Hifadhi Bora ya Ardhi.

Wakulima kutoka Kibungo Juu


Hawa ni baadhi ya Wakulima kutoka Kibungo Juu wanaoshiriki katika Mpango wa Hifadhi ya Vyanzo vya Maji na Matumizi Bora ya Ardhi.

'LUP' yafanya kweli 8/8 Moro


Idara ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imefanya kweli katika maonyesho ya Wakulima (Nane Nane) 2010 kanda ya Mashariki mkoani Morogoro wameleta wakulima halisi kutoka Tarafa ya Kibungo wilaya ya Morogoro vijijini. Wakulima hawa wanashiriki katika mpango wa kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na utunzaji na matumizi bora ya ardhi.

Tuesday, August 2, 2011

Na mashine ya kupura mpunga je?

Moja kazi ngumu katika kilimo cha mpunga ni kupura (kutoa punje kwenye mmea). Kwa wakulima wadodo hutumnia njia nyingi iliyo maarufu ni kuupiga kwa kutumia fimbo au kufikicha majani.Unapopiga mpunga uliotandazwa chini mara nyingi ubora wake huathirika sana hasa mchele kuwa na mchanga na harufu ya udongo. Kwa kutumia mashine hii ya Wakorea (pichani) kazi huwa nyepesi na ubora wa mchele huongezeka hivyo kumvutia mlaji.

Teknolojia ya umwagiliaji

Moja ya aina ya teknolojia inayotumika katika umwagiliaji wa mashamba ya miwa huko Kagera (Kagera Sugar Company) ni hiyo ya 'TANDEM' inayoonekana pichani. Inamwagilia kama vile mvua inanyesha!

JK afungua maonyesho ya Wakulima 2011

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akishangaa mkungu wa ndizi katika viwanja vya maonyesho ya kilimo mjini Dodoma viwanja vya Nzuguni wakati alipofungua maonyesho hayo jana.

Monday, August 1, 2011

wanatafakari taarifa za kikao cha Africana

Da Ceasar (mzungu)na Da Etha wakitafakari taarifa za kikao!

Kariakoo usiku

Dar Es Salaam-Kariakoo wakati wa usiku mitaa mingine huonekana hivi na biashara zinafanyika kama kawaida.

Mwenyekiti wa Africana anawasili

Mwenyekiti wa Africana alipowasili mkutanoni kwa Bajaj! Poa tu.

Mtaa wa Msimbazi

Hapa ndipo yalipo makao makuu ya 'Mnyama' Simba Sports Club. Mtaa wa Msimbazi - Jijini Dar.

The Banzis

Hawa wote ni akina Banzi kutoka kushoto - Innocent,Renatus,Slyvester na Macarios. Guess na kaka mkubwa?

Wajumbe wa Africana wakisikiliza kwa makini


WanaAfricana walihudhuria kwa wingi katika kikao hicho na kutoa maoni yao ya kuendeleza kikundi na changamoto zailizopo.

Mwenyekiti wa Africana awataka wanakikundi kulipa ada za uanachama

Tarehe 17/7/2011 kikundi cha Africana kilichopo jijini Dar kilifanya kikao chaker cha mwezi nyumbani kwa Bw. Gaitan Banzi huko Kimara Temboni. Moja ya maazimio makuu yaliyotolewa kwenye kikao hicho ni kuwataka wanakikundi kukamilisha malipo ya ada ya kila mwezi kuanzania mwaka jana hadi Desemba 2011. Pichani Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Innocent John Banzi akitoa msisitizo wa jambo hilo.