Saturday, September 22, 2012

Muhogo umeshambuliwa

Tukiwa shambani wilayani Bunda kwenye jaribio linalendeshwa na watafiti kutoka kituo cha Utafiti Ukiriguru, Mwanza baadhi ya aina za muhogo zilishambuliwa na wadudu na magonjwa. Muhogo huu pichani unaonyesha dalili ya kushambuliwa na 'redspider mites'

Tuesday, September 18, 2012

Ujenzi unaendelea kwa kasi ya kutisha Kisemvule

Wezi wa kompyuta wabambwa Kilimo

Leo mchana wezi waliofanikiwa kuiba compyuta (laptop) kwenye gari lilikuwa limeegeshwa maeneo ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika huko Temeke Veterinary walibambwa na mmojawapo kuta kipigo cha nguvu. Kwa muda mrefu sasa jijini Dar kumekuwa na mtandao mkali wa wezi kuvunja magari na kuiba vitu vinavyokuwemo ndani ya gari hasa laptop
Dereva ambaye aliendesha gari ambalo mwizi alilikimbilia akiwa amwekwa chini ya ulinzi kwenye kibanda cha jengo la Kilimo II.

Saturday, September 15, 2012

Asha Rashid uko wapi?

Nani anajua au anafuatilia habari za mwanandinga huyu aliyewahi kuichezea Twiga Stars 9Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake)

Miaka 12 -Mwanafunzi wa Chuo Kikuu

Mtoto Xavier Gordon wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 12 (pichani) amejiunga na Chuo Kikuu huko Uingereza. Inasemekana Xavier ndiye mwenye umri mdogo zaidi kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu. Ingawa kwa sasa anaendelea na masomo yake ya darasa la nane lakini mara tatu kwa mwezi huhudhuria masomo katika Chuo Kikuu Huria huko East Grinstead Uingereza, tena masomo anayochukua kwenye shahada yake ni hesabu.Yeye hupendelea maeneo magumu ya hesabu kama vile 'abstract structures' Vector and calculus na Newtonian mechanics - tena kwa muda wake mwenyewe (kujisomea). Hata hivyo kulingana na umri wake wakati anapokwenda chuoni husindikizwa na watu wazima kwani bado ni mdogo.

Walioimba "Yatubidi tukeshe"

Kwaya ya Mt. Vincent wa Paulo - Parokia ya Vikindu, jimbo kuu la Dar Es Salaam walioimba wimbo "Yatubidi Tukeshe kila wakati kwa maana hatuijui siku wa la saa...." Hivi sasa wanajiandaa kutoa mkanda wao wa picha wa kwanza.

Vituko vya jiji la Dar

Usione ajabu kijana huyu kuning'inia nyuma ya bus hili. Kuna sababu mbili 1) Ni mchezo tu ii) Anakwepa kulipa nauli. Vyote vinaweza kugharimu maisha yake kisa kutolipa sh 300 tu!

Kilwa Road yakarabatiwa

Barabara ya Kilwa ya sehemu ya jiji la Dar Es Salaam kutoka Bendera Tatu-Kurasini hadi Mbagala Rangi 3 inaendelea kukarabatiwa baada ya Waziri wa Ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli kuikataa ilipokanidhiwa hapo awali kwa kuwa kiwango chake baada ya kutengenezwa kilikuwa ni cha chini mno na kuamru mkandarasi kuitengeneza upya. Kwa wakati huu usafiri kwa kutumia barabara hiyo ni wa shida kidogo hasa nyakati za asubuhi na jioni.

Friday, September 14, 2012

Jiwe hilo!

Ndiyo maana jiji la Mwanza linaitwa Rocky City. Hapa ni eneo la Nyegezi-Mwanza karibu kabisa na kituo cha mabus ya mikoani. Ni kawaida kuona nyumba imejengwa kando au juu ya jiwe hili.

Mambo ya 'Rocky City'- Mwanza

Jiji la Mwanza linajengwa kutokana na uchumi wa vitu vitatu- Biashara ya samaki, madini na kilimo cha pamba. Hakika kila mwaka jiji la Mwanza linabadilika kwa kasi ya kutisha. Utunzaji wa jiji na ni wa hali ya juu. Usafi unazingatiwa.


Thursday, September 13, 2012

Utamaduni haukwepeki

Kila mmoja anapiga ngoma. Wasanii wa Sri Lanka wakiwakaribisha wajumbe wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA. Pichani Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe wakiwasili katika ukumbi huo.

Usafiri wa treni Dar kuanza Oktoba

Ukarabati wa reli kutoka ubungo maziwa hadi steshini jijini Dar unaendelea. Pichani mafundi wa Kampuni ya Reli (TRL) wakijaza mabonde kwa udongo katika eneo la Tabata Relini jana. Reli hiyo ikikamilika itasaidia sana kuboresha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam.(Picha kutoka gazeti la Mwananchi)

Utafiti wa Ulezi unaendelea kanda ya Kaskazini

Tanzania ina uwezo wa kuweza kuzalisha ulezi kwa wingi na kutumika kwa lishe hasa uji wa watoto.Wachaga hutumia sana ulezi kwa kutengeneza mbege (kile inachoitwa kilemba ni ulezi). Ulezi hutoa kimea kizuri hivyo huweza pia kutumika kwa kutengeneza bia.Pichani watafiti wakiangalia jaribio la zao la ulezi huko Miwaleni. (Picha na Livingstone Mwedipando- ARI-Selian, Arusha)

Magufuli na daraja la Kigamboni

Sasa ni vitendo. Daraja linalounganisha Kigamboni na Kurasini limeanza kujengwa. Pichani Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli (mwenye shati la draft) akikagua ujenzi huo jana tarehe 12/9/2012. Aliwataka wajenzi wa darajani hilo kampuni kutoka China kukamilisha daraja hilo kabla ya mwaka 2015.

Matatizo ya maji mkoa wa Mara

Bado kuna wananchi wengi hapa hawapati maji masafi, salama na karibu kama inavyoonekana pichani akinamama wakikwangua maji kutoka kwenye korongo. Matatizo haya ya maji yanasibu sehemu mbambali hapa nchini kama vile mkoa wa Mara.Picha kutoka Daily news - 13/9/2012).

Banki ya asili ya mazao

Hivi ndivyo wenyeji wa mkoa wa Mara wanavyohifadhi mazao yao ya nafaka kwenye vihenge vya asili.

Wednesday, September 12, 2012

Pikipiki tumeikuta Bunda

Wajapan wanasaidia sana sekta ya kilimo hasa katika kilimo cha umwagiliaji cha mpunga. Hutoa vitendea kazi kwa wafanyakazi wanaohusika na miradi hiyo. Pikipiki nyekundu pichani tumeikuta Bunda ilisafirishwa kutoka Dar Es Salaam. Wajapan wanahakikisha kinachununuliwa kinawafikia walengwa.

Ofisi za serikali Bunda

Kuna wafanyakazi wengi wa serikali wanapopata uhamisho kwenda sehemu nyingine huogopa na pengine huamua hata kuacha kazi. Nawashauri msiogope kuhama ofisi nyingi za serikali sikuhuzi zimeboreshwa na ofisi mpya zina miundombinu mipya kama tuliyoikuta Bunda mwezi Agosti 2012

Utafiti wa mahindi Kanda ya Kaskazini

Watafiti wa kituo cha Selian kilichopo Arusha wanaendelea na utafiti wa mahindi. Hili ni jaribio lilipo Ngaramtoni. (Picha kwa hisani ya Livingstone Mwedipando -Selian)

Banda bora la mbuzi

Kituo cha Utafiti wa Mifugo - West Kilimanjaro imejenga mfano wa banda bora la mbuzi.Hii inasaidia kwa wafugaji kujifunza na kuweza kujenga banda kama hilo katika kuboresha ufugaji wa mbuzi.(Picha kwa hisani ya Livingstone Mwedipando-Kituo cha utafiti Selian, Arusha)

Kama una zaidi ya miaka 50

Hilo ndilo lilikuwa kabati lako la kwanza (Picha na Frank Mdimi)

Watoto utawapenda tu

Ukiwafuatilia kwa karibu watoto utawapenda tu. Ndiyo maana Bw. Yesu alisema waacheni watoto waje kwangu!

Anatangaza kazi yake

Nilipokuwa Bunda kijana huyu aliniomba nimpige picha akiwa na madumu yake ya maji. Anatangaza kazi yake.

Kwa waliofika Bunda tu

Tupendane Grocery. Huwezi kukosa kupelekwa mtaa huu kwa ajili ya maakuli. Mtaa huu unasehemu nyingi za kujipatia msosi na ni karibu na mjini bunda.

Mitaa ya bunda

Kibanda maarufu cha Samaki

Hicho ni kibanda maarufu za kuuzia samaki pembeni mwa uwanja wa ndege- Mwanza. Hapa unaweza kununua Sato na Sangara. Lakini siku hizi samaki ni bei ghali jijini Mwanza. Ndoo ndogo ya samaki ni zaidi ya shilingi 50,000/=!

Nje ya Airport - Mwanza

Ukitoka nje ya uwanja wa ndege wa Mwanza kunapendeza sana

Mwanza Airport Duh!

Uwanja safi, ndege o.k. lakini majengo yake choka mbaya na yaleyale. Lakini nimetaarifiwa kuwa kuna mpango kabambe ya kuboresha majengo na miundombinu mingine ya kiwanja hicho ili kuvutia watalii zaidi kwani ni rahisi kwa watalii kuanza safari zao kwenda mbuga za Serengeti kupitia Mwanza kuliko Arusha.

'Bungalows' za Mwanza

Hili ni moja ya majumba mazuri yaliyopo kwenye barabara ya kwenda Airport karibu kabisa na uwanja wa CCM - Kirumba.

Keep left cha Mwanza

Hapa ni sehemu maarufu katika jiji la Mwanza. Ukifika hapa ni rahisi kwenda kituo cha reli, kwenda Nyamagana, kwenda Kirumba, kwenda Hospital ya Bugando na kwenda Sokoni. Hapa kuna sanamu ya samaki mkubwa aina ya sangara anayetoka maji kinywaji ni alama ya jiji la Mwanza.Watu wengi hupenda kupiga picha hapa.

Unapokaribia kutua Mwanza

Hivi ndivyo ilivyoonekana hivi karibuni kabla ya kutua Mwanza kutoka angani

Precision imetua Mwanza

Ndege za Shirika la ndege la Precision hutuoa huduma za usafiri wa anga zilizo bora. Precision haina longolongo.

Tayari kwenda Musoma

Ukisafiri kwa Precision Air kwenda Musoma wakati mwingine unaweza kuunganishwa kwa bus kutoka Mwanza kwenda Musoma iwapo hali ya uwanja zi mzuri au abiria ni wachache.Bus la Precision husubiri uwanja wa ndege kwa nauli ile ile ya ticket ya Ndege.

Tuesday, September 11, 2012

Masela wa Kisemvule!

Masela maana yake nini hasa. Kwa lugha ya mitaani masela ni watu ambao hawana shughuli maalumu utawakuta wapowapo tu. Angalia vijana hawa wanaozagaazagaa kijijini Kisemvule. hawa ni masela wa Kisemvule. Tubadilike!

Kisemvule maji bwerere

Moja ya kivutio cha Kijiji cha Kisemvule kilichopo mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga ni upatikanaji wa maji. Kijiji hiki kiko umbali wa km 27 kutoka stesheni ya TAZARA-DSM. Ni kijiji kinachokua kwa kasi ya haraka kimaendeleo kiviwanda, biashara na elimu.

Furaha ya maisha

Banzi wa Moro aliwanasa hawa wakifurahi!

Monday, September 10, 2012

Kaka na dada!

Huyo wa kushoto anamwita wa kulia ni dada yake na huyo wa kulia namwita mke wangu. Mke wake huyo wa kushoto mimi ni dada yangu. Hii ni logic ya kaka na dada wote ni ndugu!

Akina Mbetwa waongezeka

Bw na Bibi Paulo Mbetwa wa Dar wamebahatika kupata kijana wakiume na kuongeza familia ya watoto watatu akiwemo binti mmoja (wa kwanza). Pichani Mrs Nancy Banzi akimpakata mtoto mchanga-Mbetwa JR.Hongereni sana familia ya Mbetwa.

Mashuhuda wa ndoa ya Bw na Bibi Moshi

Wazee wa Vikindu kutoka kushoto Bw. Barongo na Mgaya wakishuhudia ndoa ya Bw na Bi Christian Moshi ikifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Visent wa Paulo Vikindu.

Bibi harusi akiwasili Kanisani

Bi harusi akiwasili kwenye kanisa la Mt. Visent wa Paulo-Vikindu, jimbo kuu la Dar es Salaam kubariki ndoa yake na Bw. Christian Moshi siku ya tarehe 8/9/2012, Jumamosi.