Tuesday, December 31, 2013

Hongera Dogo Richard Banzi

Dogo Richard Banzi (a.k.a Mjeshi) akisakata rumba na kitu chake kwenye ukumbi wa Tanzania mjini Morogoro siku ya Tarehe 27/12/2013. HONGERA!

Ndafu, acha mchezo msee!





Huu ndiyo utaalamu wa kuchoma ndafu.Huhitaji kuwa na oven. Chimba shimo kipimo cha mbuzi na weka mkaa. Mbuzi anaiva kwa mvuke tu. Wenyewe wachagga!

Shem Tom

Shemeji Tom Schoemacker akionyesha utaalamu wake wa kuogelea huko Mbezi Beach-Dar Es Salaam

Meab Mdimi na Catherine Banzi

Dada Meab Mdimi na binti yangu Catherine Banzi wakishangaa watoto wakiogelea nyumbani kwa mjomba Dr. G.Mluge (Marehemu) huko  Mbezi Beach tarehe 26 Des 2013.

Mama Jack na Mtani Jembe!

Mama Jack wa Kisemvule ni shabiki wa kutupwa wa Simba Sports Club akiwa pamoja na Baba Herieth  wakifurahi ushindi wa Simba kumchabanga Yanga 3-1

Mchoraji kazini




Aliitwa mchoraji na kuwachora watoto  hata wakubwa pia jinsi walivyotaka na hapo ndipo walipotokea spidermen!

Dada Batsheba Sajan

Tarehe 26/12/2013 tulialikwa na dada Janet Mluge nyumbani kwao Mbezi Beach-Dar. Hapa nilikutana na ndugu zangu wengi pamoja na watoto zao ambao wengi wao walikuwa ni akina uncle! Mbele ya picha hii anaonekana dada Batsheba Sajan a.k.a Sheba! Alikuwa siku moja nzuri ya kukumbukwa kwa mwaka 2013. Asante Dada Janeth pamoja na shemeji yetu Tom kwa wazo zuri na kulitekeleza pia. Asante aunt Rest kwa kutukaribisha.

Karibuni wajukuu zangu

Hivi ndivyo Bi. R.Mluge alivyowakaribisha wajukuu zake siku ya tarehe 26/12/2013 (boxing day) nyumbani kwake Mbezi Beach.

Ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar- KILIMO II



Mtaro umefurika Tandika Dar

Licha ya kujenga mitaro mizuri lakini uchafu umefurika ndani ya mitaro. Je ni uzembe au ni kutokujali tu!

Duka la mayai mbagala rangi 3

Hapa ni Mbagala Rangi 3 jijini Dar  yanapouzwa mayai kutoka shamba la Mkiu wilaya la Mkuranga

Dogo Kamsopi!


Mdogo wangu Joseph Kamsopi ni shabiki  mkubwa wa Simba Sports Club ya Msimbazi a.k.a mnyama

Tumepata goli moja tu!

Shabiki huyu wa Yanga haamini kuwa licha ya kuwa na akina Kiiza, Okwi, Ngassa, Kavumbagu wameambulia goli moja tu huku wakibugizwa magoli matatu.

Huyu alizawadiwa jezi nyekundu ya ZAMALEK!

Shabiki huyu wa Yanga wa Kisemvule alizawadiwa jezi  nyekundu ya Zamalek na shabiki wa Simba baada ya mchezo wa Mtani Jembe kumalizika na Yanga kufungwa 3-1

Mambo ya kukumbukwa 2013-MTANI JEMBE

Baada yaYanga kufungwa mabao 3-1 kwenye mechi ya MTANI JEMBE. Shabiki huyu wa Yanga  (aliyekaaa katikati na kushika chupa ya safari) alipozwa munkari na mashabiki wa Simba wa Kisemvule

Tuesday, December 24, 2013

Monday, December 23, 2013

Uzembe wa Kaseja

Uzembe wa Kaseja katika mchezo wa Mtani Jembe ulivyoigharimu Yanga. Na hilo likawa goli la tatu- Goooo! (Picha kwa hisani ya gazeti la Mwanaspoti - 23/12/2013)

Ngasa utalia sana tu

Ngasa utalia sana tu. Furaha yako ya kwenda Yanga utaisubiri sana kupitia SIMBA.

Nani Mtani JEMBE

Huyo aliyeshika jembe ndiye MTANI JEMBE! HONGERA SSC.

Tuesday, December 17, 2013

Tunakula ili tuishi!


Toyota Landcruiser kazini

Haya ndiyo magari yanayofaa kwa mazingira ya barabara za vijijini. Toyota Landcruiser.

Naulizia bei ya pepeta

Nilipotembelea Ifakara mwezi Juni mwaka huu kando ya kivuko cha Kilombero niliweza kununua pepeta!

Samaki wa mto Kilombero











Hapa ni kuonja na kununua tu. Halafu nipe feedback!

Wasichana wanakula kidogo tu

Inasemekana wasichana wanakula kidogo tu. Je ni kweli? (Picha na Dr. L.Kasuga, ARI-Naliendele, Mtwara)

Kiti cha Tanzania kipo

Mkutano wa Kimataifa wa Korosho. Nafasi ya Tanzania ipo.

Mtwara-Dar 'kuchimba dawa'

Safari ya Mtwara-Dar abiria "wanachimba dawa' (Picha kwa hisani ya Dr. L.Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)

Kumbukumbu ya mafuriko Mtwara Januari 2013

Mafuriko ni balaa. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa eneo la Majengo mjini Mtwara Januari 2013(Picha kwa hisani ya Dr. L.Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)

Mwembe wa Dr. Kasuga

Dr. Kasuga anasema kilimo ni biashara haonjeshi hata embe moja. (Picha kwa hisani ya Dr. L.Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)

Kusoma kuelewa kukesha mbwembwe

Ujumbe unatosha kwa wasomi! (Picha kwa hisani ya Dr. Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)

Gulio la samaki

Gulio la samaki. Hapa wapo wauzaji na wanunuzi wa samaki. (Picha kwa hisani ya Dr. Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara).

Aina za karanga

Hizi ni aina mbalimbali za zao la karanga. Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Mtwara ni maarufu kwa utafiti wa zao la Karanga.