Thursday, July 17, 2014

Nasaba za mahindi kama tulivyo wanadamu

Mahindi yako ya aina nyingi.Meupe, meusi,njano, myembamba,mafupi,mbegu nene. Hata wandamu tuko wa aina nyingi.Watalaamu wa kilimo tunatunza nasaba za mimea. Wahindi wamepiga hatua kubwa katika shughuli ya ukusanyaji nasaba za mimea katika maabara yao.

Jembe la mkono ni lilelile

Katika kilimo jembe la mkono haliepukiki. Hili ni aina ya jembe la mkono linalotumiwa India hasa kaskazini  mashariki ya  nchi. Banzi wa Moro aliliona jembe hili katika jimbo la HARYANA. Mpini mfupi n jembe ni pana. Jembe la mkono ni lilelile. Hata hivyo India  hutumia sana  wanyama katika shughuli za utayarishaji shamba.

Wednesday, July 16, 2014

Uzalishaji kwenye udongo wenye chumvichumvi india


CSSRI ni kifupi cha 'Central Soil Salinity Research Institute.' Hii ni Taasisi ya Utafiti wa Udongo wenye chumvi nchini India. Taasisi hii imepewa kazi ya kutoa ufumbuzi wa uzalishaji kwa maeneo yenye udongo wa chumvi chumvi ambao unasababisha uzalishaji mdogo wa mazao au kutozalisha kabisa hivyo kuwafanya wakazi wa maeneo hayo kuishi kwa kubangaiza. Tatizo hili nchini India ni kubwa.

Kama mnavyofahamu nchi ya India ni Penisular. Karibu sehemu kubwa imezungukwa na maji tena ya bahari hivyo chumvi imeathiri sehemu kubwa ya ardhi ya India. Kwa kuona tatizo hilo Serikali ya India imeunda CSSRI. Taasisi hiyo imeshafanya tathmini ya maeneo yaliyoathirika na kufanya tafiti mbalimbali za udongo  na kutoa teknolojia mbalimbali za kuboresha uzalishaji kwa mazao,mifugo na mifumo mingine ya kilimo. Moja ya teknolojia hizo ni uzalishaji wa aina za mbegu za mpunga zinazostahimili chumvichumvi .Aina hizo ni  CSR 27, CSR 30 na CSR 36.

Tatizo hili hata hapa Tanzania ni kubwa, kwa sehemu ambazo zinafaa kuzalisha mpunga lakini kutokana na chumvi mpunga umeshindwa kustawi. Utafiti wa kutatua tatizo hili unaendelea katika Kituo chetu cha Utafiti cha KATRIN- Ifakara. Kuna haja ya kuanzisha mashirikiano ya kitaalamu kwa pande zote mbili kuweza kufanya tafiti za pamoja za kupambana na tatizo hili na kuweza kuwasaidia wakulima wetu ili waweze kuzalisha mpunga kwenye maeneo yenye chumvi.

Miundombinu ya usafiri India

Jijini New Delhi - barabara za magari, treni  zinaimarishwa. Pamoja na kwamba idadi ya watu jijini New Delhi ni kubwa takaribani 250 milioni. Hata hivyo barabara kwa kiwango cha lami ni nyingi na ni pana. Usafiri wa reli - metro na za kawaida upo na miundo mbinu hiyo inaendelea kujengwa sehemu nyingine za mji.

India - hakuna kulala utafiti wa Bioteknolojia








Utafiti wa Biteknolojia umepiga hatua kubwa nchini India. Hapa kuna Centre ya Biotechnology Research. Bioteknolojia ni muhimu kwa wakati tulionao sasa kwasababu matatizo yanayoikumba sekta ya kilimo katika uzalishaji ni mengi kama vile visumbufu vya mimea na maabadiliko ya hali ya hewa ambapo baadhi yake utafiti wa kutumia njia za kawaida umeshindwa kuleta majibu yanayotakiwa.Kwa kutumia bioteknolojia imewezekana. India imewekeza  vya kutosha katika utafiti huu. Wana watafiti mahiri  na miundo mbinu ya kisasa. Tulipotembelea centre hiyo, tuliwakuta  watafiti vijana wanaume kwa wanawake wakiendelea na utafiti kwa ari. Hii imebainika kutokana na uwezo wao wa kujieleza pamoja na taarifa za kitafiti walizokwishazitoa.

Utafiti wa Post Harvest -Technology- India



Tunaweza kuzalisha mazao mengi tukashindwa kuyatumia au kuyahifadhi kwa matumizi ya baadaye. Badala ya kula maembe,machungwa, mananasi au ndizi kama tunda, mpunga kama wali, mahindi na muhogo kama ugali, tunaweza kusindika na kupatabidhaa nyingine kama vile  juice,pombe, biskuti,maandazi,mikate n.k. Bidhaa hizi zinaweza kuuzwa kwa bei nzuri kuliko zinapouzwa kama matunda au nafaka. Isitoshe kama tutajenga viwanda vya kutengeneza bidhaa hizo kama afanyavyo Bakhresa, wananchi watapata ajira. Hivyo kuna haja ya kujenga uwezo wa 'Post harvest research' katika vituo vyetu vya Utafiti kama walivyofikia wenzetu Wahindi. Katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo India, watafiti wamefanya kazi kubwa katika eneo hili na hivyo kuwa na ushirikiano na viwanda katika kuzalisha bidhaa hizo kwa wengi kwa ajili ya matumizi kwa walaji hivyo kuongeza kipato cha wakulima na kuboresha maisha yao,lishe ya wananchi na kukuza uchumi wa taifa

Tuesday, July 15, 2014

Utafiti wa mazao ndani ya - Phytophtoron Centre- IARI


Mpunga umeoteshwa kwenye-Green house

Nyanya ndani ya Green House



Utadhani Madaktari!






Maabara yana masharti yake. Sayansi ni kufuata taratibu bila ya hivyo mambo huharibika. Moja ya sharti ya kuingia kwenye maabara hii ni kuvaa makoti. Tulipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo India (IARI) tulipata fursa ya kutembelea kituo/maabara ya utafiti wa mimea katika mazingira ambayo siyo ya kawaida - kitaalamu inajulikana kama 'Phytophtoron.' Maabara hii ni kubwa na ya kisasa. Miundo mbinu iliyomo ndani ya maabara kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kwa kompyuta. Hapa mimea inajaribiwa katika mazingira tofauti  kama vile hali ya joto,mwanga,maji na rutuba. Maabara hii hufanya kazi mwaka mzima. Mtafiti anapofanya jaribio lake katika maabara hii hakuna kusingizia kuwa jaribio halikuweza kuendelea kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa sababu katika maabara hii kila kitu kiko ndani ya uwezo wa mtafiti. Kwa kufanya hivyo matokeo ya utafiti hupatikana katika muda uliopangwa.Ushirikiano kati ya watafiti, wahandisi na wafanyakazi wengine ni mkubwa katika maabara hii, kwani lengo ni moja na kufanya utafiti na kutoa matokeo haraka.

Saturday, July 12, 2014

Visumbufu vinafanana - tofauti ni mikakati ya kitafiti ya kutokomeza








Watafiti wa Kilimo India wameshafanya kazi ya kutosha kupata suluhisho la visumbufu vya mimea. Wadudu na magonjwa mengi yaliyopo India yapo pia nchini Tanzania. Wameshafanya kazi kubwa na visumbufu vya mpunga isipokuwa ugonjwa wa kirusi cha mpunga ujulikanao  'Rice Yellow Mottle Virus' au kule Ifakara maarufu wa jina la 'kimyanga.'  Hivyo kuna umuhimu wa kufanya kazi za pamoja na watafiti hawa ili kuweza kutoa majibu sahihi ya kuviangamiza visumbufu hivi vinavyosababisha uzalishaji mdogo na usiyo bora wa mazao yetu.

Utafiti wa Visumbufu vya mimea (NCIPM) - IARI

Tulikaribishwa kwa furaha - NCIPM

Mkurugenzi wa NCIPM-IARI

Watafiti wanawake wa NCIPM-IARI

Bi. Ruth Kamala akikabidhiwa ua na mwenyeji wake katika kituo cha Utafiti wa Visumbufu vya mimea

Tunapata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo

Tuliyoyaona Kituo cha Utunzaji wa Nasaba za Mimea India


 
 Tulipotembelea National Bureau of Plant Genetic Resource - India  aliye kushoto kwangu ni 'Kaka' yangu Prof. Bansal ( ndiye Banzi wa  Tz !) Mkurugenzi wa Centre.




Wajibu wa centre umewekwa wazi ili kila mtu afahamu


Tuzo ammbazo centre imepata kwa kazi nzuri

 Vituo vya utafiti vinavyohusika na utunzaji wa nasaba za mimea nchini India




Kumbukumbu ya Wakurugenzi waliongoza Centre ya Utunzaji wa nasaba. Wa sasa ni Banzi wa India huko anajulikana kama Dr.Bansal (sasa ni Professor). Ha! akina Banzi mpaka India hongera baba zetu Wambiki!
Wahindi wameweza kukusanya nasaba za mimea kutoka sehemu mbalimbali za dunia



   Angalia wenzetu wanakotaka kwenda na mikakati iliyopo.