Friday, November 21, 2014

Tume ya Mipango inapoperemba

Ukisikia kuperemba ndiyo huku. Huwa ni wataalamu wa Tume ya Mipango wakiperemba mradi wa Maji kwenye moja ya Halmashauri nchini. Ilibidi waende mpaka juu kabisa kuhakikisha hilo tank la maji linalojengwa ili kujihakikishia ubora wa tanki hilo baadaye kuandika taarifa. Sijui wameona nini, mimi sijui.

Jaji Mkuu wa Tanzania amjulia hali Rais Kikwete

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Chande na ujumbe wake walipomtembelea Rais wetu Dr.J.M.Kikwete alipokuwa kwenye matibabu nchini Marekani (picha kwa hisani ya blog ya Michuzi)

Ukiwa ni mkali wa Mahesabu-Omba


Spika Makinda anavyotuwakilisha


Mh. Anne Makinda (Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) anavyotuwakilisha nje ya nchi ( Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

The Legends - Djs


Kutoka Bukoba hadi Bungeni Dodoma

Hivi ndivyo tunavyotakiwa kuwajenga watoto wetu wawe na uelewa mpana na kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yetu. Wanafunzi hawa wa shule ya Rweikiza kutoka Bukoba wamesafiri hadi Dodoma kutembelea Bunge letu kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi. Hivi kweli hawa wakipata swali linalouliza jinsi Bunge linavyofanya kazi watashindwa kulijibu? Hapa wanakutana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda. Ona jinsi Pinda alivyofurahi akizungumza nao. Shule zinatakiwa kuwa na programu za aina hii. Huwezi kuzungumzia Bunge la London wakati la kwenu la Dodoma hulifahamu!

Dr. Florence Turuka Matawi ya Juu

Tulipokuwa Tosamaganga High School, Dr. Florence Turuka (kulia) alikuwa Form V  maana yake alikuwa mdogo wetu! Dr. Turuka sasa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (kushoto ni bosi wake Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda). Ninavyomfahamu Turuka tangu tukiwa Tosa ni 'kichwa' mwadilifu, social na mtu wa watu. Mpaka leo tukikutana hakosi kuniita Kaka Banzi.Je, wengine wanaweza? Dr. Turuka umetupaisha sana wana TOSA. Hata George Nyaupumbwe  a.k.a. Ngi anafahamu hilo. (Picha imenyofolewa kutoka Michuzi Blog)

Wednesday, November 19, 2014

MV-DAR ES SALAAM-Kivuko kipya jijini



Nahamia Resolution Insurance

Siku hizi bima za afya hapa nchini ni  nyingi. NHFI mkinizingua, nahamia Resolution Insurance hebu boresheni huduma zenu kwa wateja hata package pia. Haiwezekani kupima typhoid mpaka hospitali kubwa si tutakufa wateja wenu? (picha kwa hisani ya michuzi blog)

Usome ujumbe wa Pope Francis


Ni shidaaaa!


Upendo uendelee


Tafuta namba inayokosekana


Nauza gari ya urithi!

   Tena iko kwenye hali nzuri tu!

Ni ufisadi tu huo

Hebu fikiri mwaka 2010 tu alikuwa kimbambau na TV yake ya kitumbo. Mwaka 2014 miaka minne baadaye mjamaa ameshajikusanyia chake kupumua anashindwa ulimi unamtoka na huku akiwa amebadili TV na kuwa na flat screen. Ni ufisadi tu!

Achia 'tie' yangu

   Wenger wa Arsenal na Mourinho wa Chelsea  katika prukshani.

Sisali hapa

Kama wameshindwa hata kuedit bango lao la utambulisho kuna nini tena. Hakika siwezi kusali kwenye kanisa hili ni utapeli mtupu.

Nataka jibu haraka!


'Joti' akiwajibika jukwaani

Commedian maarufu nchini wa kikundi cha ZE COMEDY akiwajibika jukwaani kama polisi!

Simba wanapopata goli

Simba yangu inapouwa mtu ni furaha kwa wachezaji na mashabiki wa klabu kubwa kutoka mtaa wa Msimbazi.

Chapati hazikuokwa vizuri

Hizi si chapati. Pengine tunaweza kuita mabumunda. Chapati za ukweli ni laini zimetulia ukizichambua zinachambulika kamakaratasi. Lakini hizi bado sizielewi mwenzenu na hazinivutii

Keki namba 4 inatisha

Tengenezeni keki lakini siyo namba 4.

Wewe umesoma neno gani katika mraba huu?


Ubunifu mwingine nomaaa

Jamani kiatu umbo la mamba na kinatisha lakini ni ubunifu na inawezekana kinauzwa aghali sana

Tuesday, November 18, 2014

Vifaa ninavyotumia ofisini

Nilianza kuchukia mwandiko mbaya tangu nikiwa shule ya msingi, nilipenda kuiga mwandiko wa Mama Beatrice Mhango, shangazi Pauline Mloka, Baba yangu Mkubwa Mwl. Ephrem Ephrem Mbiki, Kaka Seraphin Chibby na marehemu uncle Longin Mizambwa hawa walinivutia kwa wakati huo na kwa kweli niliwaiga kwa kuumba herufi mojamoja niipendayo na kuchanganya na kutoka na mwandiko wangu 'unique'. Nilipofika sekondari pale Njombe niliwakuta wanafunzi wanaoandika miandiko mizuri sana akiwemo rafiki yangu marehemu John Makoroma (The Printer) wengine walionivuta kuandika mwandiko mzuri ni uncle Nestory Daulinge, uncle Balozi Daniel Mloka, rafiki  na wengine wengi walioandika vizuri. Kwa hali hiyo nilipenda pia kutumia kalamu nzuri ndiyo maana mpaka sasa moja ya vitu ninavyovipenda kuwa navyo katika maisha yangu ni kuwa na kalamu nzuri. Ingawa kuna kompyuta na ni mtumiaji mzuri lakini sikosi kununua kalamu nzuri hata fountain pens ninazo na si moja ni za aina aina. Angalia vifaa ninavyotumia kikazi na kwa mawasiliano ninavipenda na vinanipa motisha ya kuandika. Napenda kuandika katika maisha yangu napenda pia kutumia zana bora.

Baiskeli hii kikwenu mnaiitaje?


Hardest thing to find


Fuuuu!!!

   Haa kama mlgezo ndo huu ni fuuuuuuuuuu!

Kifaa hiki kinamfaa Jaja

      Kwa njumu hizi Jaja lazima aiue Simba

Mapenzi ya ukweli

    Unampenda jinsi alivyo na si kudanganyana. Haya ni mapenzi ya ukweli

Soma ujumbe mbele ya gari

   Ukiulewa ujumbe huo huwezi kulaumu.

Nipe jibu sahihi

Bila kujua kanuni za hesabu utachemsha tu. Haya nipeni majibu

Ni bora kuliko kumbeba

Anapelekwa hospitali ndani ya wheelbarrow. Ni bora kuliko kumbeba. Lakini hali inaonyesha umaskini uliokithiri.

Anaizimia CHADEMA

   Wenye CHADEMA yao huyu ni mmoja wapo, mpaka  sebuleni

Nisiikose picha ya Mh. Kikwete alipolazwa Marekani

  Si rahisi kwa Rais kutangaza anachougua.  Rais wa Tanzania Dr. J.M.Kikwete ameweka wazi kinachomsibu na matibabu aliyoyapata

Atanasa tu

Hachomoki, kwa mtego huo atanasa tu. Ni hatari kwa watoto wetu na aibu kwa watu wazima kutumia fedha kama chambo.

Mnara wa mkoa gani hapa Tanzania?

Kwa wale ambao wametembelea mikoa mingi ya Tanzania hebu tambua mnara huu uko wapi?

Polisi anapocheza pool akiwa kwenye sare ya kazi

                     Toa maoni yako kwa polisi huyu.

Mbeya City Kwishneee

Kuna msemo wa Kiswahili unaosema kuwa, ngoma ikilia sana haikawia kupasuka. Hiki ndicho kilichotokea kwa timu ya soka ya Mbeya City. Msimu uliopita ilikuwa tishio kwa timu nyingine kila timu iliyotia mguu Mbeya ilifungwa au kutoka sare.Mwaka huu kinyume chake watu wanakwenda Mbeya wanajichukulia pointi kirahisi. Nasikia kisa ni ukata. Mwaka wa jana timu ikishinda kila mchezaji alipata posho ya shilingi 25,000/= na sare 15,000/= mwaka huu mpango huo haupo. Nimesoma hivi karibuni kwenye gazeti moja hapa nchini kuwa kocha wa timu hiyo Bw. Mwambusi 'amebwaga manyanga.' Sijui ni kweli.

Ukipenda mayai jifunze kufuga kuku


Monday, November 17, 2014

Neema Kirway Send off:Ndafu ikiingizwa ndani ya ukumbi wa Best Choice

Kwa Watanzania wa kutoka mikoa ya Kaskazini hasa Arusha, Manyara na Kilimanjaro shughuli bila ndafu haijakamilika. Ndafu yaingizwa ukumbini.

Wangoni hawakukosa Ligambusi






Walipokaribishwa Wangoni (wakwe wa Neema) kutoa burudani wao waliingia na ngoma ya Ligambusi. Angalia jinsi kila mmoja alivyokuwa akijimwaga kivyake vyake. Mcheck huyo jamaa mwenye shati nyeupe na suruali nyeusi-Utamwambia nini kuhusu Ligambusi. Haa kila mmoja na asili yake.

Wairaq wakati wa kukumbuka nyumbani









 Hakika, ulifika wakati wa kukumbuka kwao. Wazazi na vijana wao walijumuika kucheza ngoma ya asili ya Wairaq wakiongozwa na Bi. Neema Kirway na wazazi wake.