Friday, October 30, 2015

Unapopiga picha

Mahali sahihi,muda sahihi na staili ya pekee. Hakika kuna wanaojua kupiga picha

Utajiri wa raslimali za Matombo-Kibungo Juu


Kunambi Jakka, akishangaa maji yakitiririka kutoka milimani Kibungo Juu.

Matombo-Kibungo Juu inastawisha viungo kama Unguja

Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyo. Matombo-Kibungo juu karafuu na hiliki vinastawi

Hii ndiyo Kibungo Juu-Matombo,Morogoro

Hebu angalia jinsi Matombo-Kibungo Juu inavyopendeza. Angalia  migomba inavyochipuka. Mkakati wa makusudi wa kuendeleza kilimo cha ndizi sehemu hizi kinatakiwa ili kuwajaza wakulima mapesa.

Landscape ya Kibungo Juu

Kwetu Matombo- Kibungo Juu ni kuzuri. Viongozi waliochaguliwa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi taifa tupange pamoja jinsi ya kuwaendeleza wananchi wanaoishi sehemu hizi.

Huku ni Matombo-Kibungo Juu

Angalia kwetu Matombo-Kibungo Juu kulivyo na neema ya mazao- Migomba ilivyostawi bila kutumia mbolea za chumvi chumvi. Lakini sijui bendera ya CHADEMA imefuata nini huku juu!

Ilibidi kutumia shina la muhogo kupanda milima

Safari kuelekea Kibungo Juu-Matombo, Morogoro.Pamoja na kuvaa jeans na viatu maalumu  vya kumuwezesha kupanda milima Kunambi Jakka ilibidi kutumia shina la muhogo kama nyenzo

Matombo-Kibungo Juu

Bro.Kunambi baada ya kupanda mlima na kundi lake ilibidi kupumzika kidogo

Monday, October 26, 2015

Friday, October 23, 2015

Wafanyakazi wa Kilimo tunapambana na NJAA & UMASIKINI

Hata wafanyakazi wa Kilimo wanapambana na Njaa na Umaskini. Kauli hii waliitoa kwenye moja ya Sikukuu ya Wafanyakazi hivyo si kitu kipya.

Niliosoma nao Kirusi-Tashkent

Hili ndilo kundi nililosoma nalo lugha ya Kirusi nikiwa Tashkent, Uzbekstan ( former republic of USSR). Hapa naweza kuwakumbuka wachache kwa majina. Kushoto kwangu ni Osama kutoka Syria anayefuata ni Dada Aurelia kutoka Madagascar (Huyu alikuwa ni mkali wa computer, Hesabu na Kirusi) wengine ni madada kutoka Nicaragua. Ilikuwa ni mwaka  1987 katika Kitivo cha Maandalizi ya Wanafunzi.Baadaye niliendelea na masomo yangu katika mji wa Simferepol huko Ukraine mji ambao Russia umeuchukua tena kama sehemu ya nchi yao.

Unapokuwa na watoto unajifunza lugha kwa wepesi zaidi

Nilipokuwa katika mji wa Tashkent huko Uzbekstan ambako nilipangiwa  kujifunza lugha ya Kirusi kabla ya kuendelea na masomo yangu ya uchumi kilimo, niliweza kujifunza lugha hiyo kwa kuongea kuongea na wananchi wa aina mbalimbali ili kupata uzoefu. Pichani niko na mwanafunzi mwenzangu kutoka Kigoma, Tanzania (jina nimelisahau) tukiwa na wanafunzi wa shule ya msingi. Tuliwaomba kupiga picha wakati wakirudi nyumbani kwao wakitoka shuleni. Tuliweza kuzungumza nao kwa kirusi na kutuelewa. Wakati huo tulikuwa tumetimiza miezi mitatu tu tangu tutoke nyumbani Tanzania mwaka 1987.(Picha kutoka Maktaba ya John Banzi)

Walimu wangu nikiwa Tashkent- Uzbekstan

Hawa ni walimu wangu nikiwa kwenye mafunzo ya lugha ya Kirusi kule Tashkent, Uzbekstan moja ya majombo iliyokuwa USSR - mwakwa 1987.

Maria Banzi na Mwalimu wake

Maria Banzi akiwa na mwalimu wake wa Mount Carmel Convent Primary School Vikindu kwenye dawati la maonyesho ya sayansi mwaka 2015

Zamani picha nyingi tulipiga studio

Hii ni picha yangu ya zamani nikiwa Simferpol-Urusi.Picha hii niliofotolewa nikiwa ndani ya studio eti nikijidai kupiga simu.

Ezrome Magagula- Facilitator Mananga


Ezrom Magagula ni Mwalimu wangu wa masuala ya Menejimenti. Ezrome ana kipaji kikubwa kwenye masuala ya Menejimenti akikufundisha Human Resource Mgt utampenda, Monitoring and Evaluation yumo sana, Gender and Environment Mgt  safi sana. Project Management zaidi sana. Ukibahatika kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi Mananga Centre for Regional Integration and Management Development unaweza kukutana naye kama hajaenda kutafuta "malisho ya kijani"

Mimi Kipaumbele changu ni Kilimo

Hivi bila shibe utasoma? Kwanza chakula, Elimu baadaye. Nakumbuka nilipokuwa Tosamaganga High School    (Kidato cha  5-6) Mkuu wa Shule Mpogole alikuwa anatupatia chakula kizuri. Kila siku mchana sisi tulikuwa tunakula wali na nyama, mara moja kwa juma tunapata karanga za kukaanga (nusu kilo). Kweli tulikuwa na upungufu wa waalimu wa Chemistry na Biology lakini tulifundishana wenyewe kwa wenyewe hadi tulipopata walimu hao tukiwa kidato cha sita. Ajabu tulifaulu wote na sasa wengine ni maprofesa vyuo vikuu na wengine ni mabingwa katika fani mbalimbali kwa sababu tulishiba na si kushiba tu tulipata balanced diet. Muulize George Nyaupumbwe a.k.a Ngi wa TRA.

Upendo wa Waafrika

Tulipokuwa nchini Swaziland kwa mafunzo ya muda mfupi  mtoto huyu,mama yake na baba yake ambaye ni mfanyakazi wa Mananga  Centre for Regional Integration and Management Development walikuwa nasi kwenye safari ya kutembelea mji wa Nelspruit nchini Afrika ya Kusini. Angalia jinsi Waafrika walivyo na upendo. Hii ni nadra sana kutokea huko Ulaya.

The Mantenga Cultural Group-Swaziland

Kikundi cha Utamdaduni cha Mantenga nchini Swaziland. Hiki ni kikundi kinachoendeleza utamaduni wa Waswati ni kikundi kilichoandaliwa vizuri kuimba na kucheza ngoma za kitamaduni. Ni mchanganyiko wa wanawake na wa wanaume wengi wakiwa vijana. Hakika ukipata bahati ya kuwaona wakitumbuiza  utasuuza moyo wako.

Tanzania tuna vikundi vingi vya aina hii, lakini miaka ya hivi karibuni naona vimedorora. Tuna nafasi kubwa ya kuendeleza vikundi vya utamaduni kujenga uzalendo nchini na pia kutangaza nchi yetu. Ni moja ya chanzo cha ajira kwa vijana wetu.

Zana za kupakua na kupakia mzigo Bandarini Dar





Sisty Banzi alipokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo Bandarini Dar, aliweza kupata picha hizi zinazoonyesha zana za kupakua na kupakia mzigo bandarini Dar. Hakika Mamlaka ya Bandari Tanzania imejipanga kutoa huduma bora za bandari ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Tulivyomuaga mzee wetu Anderson Mtui






Hivi ndivyo tulivyomuaga Mzee wetu Anderson Mtui ( Mjomba wake Sifuel Felix a.k.a. shaft) pale Azania Front Cathedral jijini Dar ilikuwa ni majonzi majonzi majonzi. Shaft alinieleza kuwa Mtui alikuwa zaidi ya uncle. "I lost my friend!"

Zamani Motel Agip

Hotel Agip, zamani Motel Agip kama ilivyokutwa na JB jana wakati nikiwa AFC (Azania Front Cathedral). Miaka ya themanini Motel Agip ilikuwa ndiyo mpango mzima. Vijana walikutana hapo kwa mipango mbalimbali hasa starehe. Disco la nguvu lilikuwa likipigwa hapo. Sikuhizi licha ya kubadilisha jina na kuwa Hotel ni cha mtoto kabisa sikuhizi kuna Hotel za viwango vya juu ikiwemo Serena!

Mara ya mwisho ya kula chakula na Mangengesa Mdimi

Katikati ni mjomba wetu Charles Pius Hugo kushoto akichekesha,mama Dolorosa Mdimi na kulia ni Mzee Chrispin Mangengesa Mdimi ( R.I.P.) hii ni picha ya ukumbusho wa chakula cha pamoja na Mzee Mdimi wakati wa kupokea mahali ya binti wake wa mwisho Bi.Hellena Mdimi pale External-Makuburi jijini Dar. Mzee Mdimi  alifariki tarehe 12/10/2015 na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 15/10/2015.

Vijana wanapopenda vitu ghali!

Kijana wangu Sisty Banzi anapenda sana magari. Angalia jinsi alivyodiriki kupiga picha mbele ya gari ya babu yake Dr. Gregory  P.Mluge (R.I.P). GMC ni gari ya kimarekani.Ni gari zuri na la kifahari lakini matumizi yake ya mafuta utachoka mwenyewe hata bei ya vipuri ni ghali sana. Lakini kupanga ni kuchagua. Akitaka kumiliki gari kama hili lazima ajitume katika kazi na kuingiza kipato cha kutosha. Vinginevyo ataishia kupiga picjha mbele ya gari ya babu!