Saturday, June 27, 2009

Hivi tumejitayarisha kwa bei mpya za mafuta

Ni majuzi tu tulipokuwa tukifurahia kushuka kwa bei za mafuta na hata kushuka gharama za usafirishaji. Lakini ghafla bei zimepanda tena. Hii ina maana kuwa gharama za usafirishaji zitaongezeka na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha. Bei za mafuta zimeongezeka wakati Bunge la Bajeti linaendelea huko Dodoma. Kama Bajeti hizi zilitayarishwa kwa bei za chini za mafuta kwa vyovyote vile utekelezaji wa mipango yetu kwa kiasi kikubwa itaathirika. Ndiyo maana nauliza je tumejitayarisha kwa bei mpya za mafuta?

BURIAN MICHAEL JACKSON

Watu hufa na sote tutakufa. Lakini wanapokufa watu kama akina Michael Jackson dunia nzima inapata habari na hisia ni kwa watu wengi. Mwanamuziki huyu alikuwa na kipaji cha pekee katika nyanja za muziki tangu utoto wake. Alivutia watu wengi wa mataifa mbalimbali ndiyo maana kifo chake ni habari kubwa. Amefanya mambo mengi.

Hata hivyo pamoja na kuwa maarufu amepita katika misukosuko mingi ya kuchafuliwa jina lake na hata kushitakiwa. Ameacha watoto lakini hatujui kama ameacha mjane. Huyu ndiye Michael Jackson ninayemfahamu. Burian Michael.

KARIBU NYUMBANI KASEJA

Ndo hivyo tena, Kaseja karudi nyumbani nasi wapenzi wa wekundu wa Msimbazi - Simba Sports Club tunasema karibu nyumbani Kaseja.

Kujiamini na kujituma siri ya ushindi wa USA dhidi ya Hispania

Ni wachache waliotabiri kuwa USA itashinda dhidi ya Hispania katika mashindano ya FIFA kombe la mabara mchezo wa nusu fainali uliofanyika nchini Afrika Kusini tarehe 25 Juni 2009.

Wakicheza kwa kujiamini, kujituma na uzalendo wa hali ya juu. USA iliweza kuitandika Hispania mabingwa wa Ulaya bao 2-0 mbele ya wachezaji wenye majina (mafathers) akina Fernando Torres na Ikker Cassilas anayesemekana kuwa ni mmoja wa magolikipa bora kabisa ulimwenguni. Soka ndivyo ilivyo na mpira siku zote unadunda. Walicheza kama timu na hawakujali kuwa wanacheza na wachezaji wenye majina makubwa. Lakini walikuwa na kitu cha ziada kuwa ni Waamerika taifa kubwa ingawa soka kwao ndo kwanza linapanda chati.

Wabunge mnawaumiza wafanyakazi wa serikali

BUNGE hili la bajeti limekuwa kali kweli kweli kila mmoja anaongea tena kwa jazba! Hakuna anayefuata sheria na taratibu. Lakini kibaya zaidi ni wabunge kuwafanya wafanyakazi wa serikali wasipumue huku wao wakipitisha maslahi yau bora zaidi kimya kimya. Huu ni unafiki.Eti oh mikutano na warsha stop! Huku wao wakiendesha mikutano. Serikali bila mikutano na warsha itaendeshaje shughuli zake. Chai na vitafunwa vimezidi, posho kwa kazi nzuri (Honorarium) ondoa. Sasa huyu mafanyakazi mnayemtaka afanye kazi kwa tija bila kumpatia mazingira mazuri ya kufanya kazi hiyo tija itapatikanaje? Ongezeni mishahara iwe ya kuvutia basi. Wabunge msikurupuke tu na hoja muwe makini vinginevyo sisi tunafikiri ni kujisafishia njia kwa uchaguzi wa mwakani.

Tuesday, June 23, 2009

Je, t-shirts na caps ndo ubora?

Imekuwa mtindo kwa siku hizi kila linapotokea tamasha au maadhimisho ya aina fulani basi sare za T-shirts na Kep kapa (caps) ndizo zinazotawala. Watu hupigania kupata sare hizo hata kama si mshiriki. Yuko tayari kupata hata sare tano kwa lolote lile. Hivi ni muhimu kuwa na sare katika maadhimisho? Je, sare ni T-shirts na kep kapa tu?

Tuwe na mipango madhubuti ya power tillers tutakazonunua

Hivi sasa viongozi wanaimba KILIMO KWANZA. Kila Halmashauri inunue powertillers za kutosha. Je, mipango imewekwa ya kutumia powertillers hizo. Je, ni kweli mapinduzi ya kijani yataletwa na powertillers. Tusije kubweteka na power tillers. Mapinduzi ya kijani yataletwa na factors nyingi zinazohusiana katika kuboresha uzalishaji wa kilimo hapa nchini. Viongozi wa Halmashauri wawe makini katika kutoa maamuzi katika suala hili.

Wamiliki wa mabus wanapokuwa na sauti dhidi ya abiria

Kabla ya kutangazwa nauli mpya za mabus kutokana na kushuka kwa bei za mafuta. Usafiri kutoka Mbagala R3 hadi Kisemvule haukuwa na matatizo. Mabus yalikuwa yanapatikana wakati wote na nauli ilikuwa sh 600 kwa mtu mzima. Mara tu bei ziliposhuka na kuwa sh 400. Wamiliki wa mabus wamekuwa wakipeleka mabus kwa kupenda wao tena kwa nauli ya si chini ya sh 500. Hii maana yake nini? Utakuta abiria wamejazana pale Mbagala R3 lakini mabus yanakwenda Mkuranga. Hayataki kupakiza watu wa Vikindu wala Kisemvule. SUMATRA mko wapi? Hivi ni halali kwa wenye mabus kuwanyanyasa abiria kwa hali hii?

Tuesday, June 9, 2009

Mkulima anapotambua magonjwa ya mimea


Magonjwa ya mimea ni moja ya matatizo yanayoathiri uzalishaji wa mazao shambani. Mara nyingi mazao yanaposhambuliwa na magonjwa uzalishaji hupungua kwa kiasi kikubwa. Moja ya zao ambalo hushambuliwa na magonjwa kirahisi ni zao la nyanya. Pichani Mkulima Maulid Pembe wa Kisemvule akiionyesha blog hii mmea wa nyanya ulioshambuliwa na ugonjwa.

Kisemvule wajikita kwenye kilimo cha mbogamboga


Wananchi wa Kisemvule vijana, wajane, na wazee wamejiunga katika vikundi na kuanza kuzalisha mboga za aina mbalimbali kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao. Mradi huo unafadhiliwa na TASAF.


Mradi umeanza rasmi mwaka huu na tayari mazao yameshaanza kupandwa na wakati wowote kuanzia sasa yako tayari kuvunwa hasa pilipili hoho. Blog hii ilitembelea kwenye eneo lililolimwa na kujionea mazao mazuri ya bamia, nyanya maji (tomato) na pilipili hoho na nyanya chungu.

Kutokana na mazungumzo na mmoja wa wana kikundi, Bw Maulid Pembe, TASAF imetoa madawa, mbolea na vifaa muhimu vya kilimo cha mbogamboga kama vile mashine ya kumwagilia maji na mabomba. Mategemeo ni kuvuna mboga kwa wingi tatizo ni soko. Kwa mfano aliuliza blog hii kama wanaweza kupata soko la pilipili hoho. Pichani Bw Maulid Pembe akikagua mche wa nyanya chungu uliostawi vizuri.

Monday, June 8, 2009

Makutupora nyumbani kwa zabibu


Kituo cha Utafiti wa Kilimo Makutupora ndicho kituo pekee kinachofanya utafiti wa zao la zabibu hapa nchini. Kituo hiki kipo mkoani Dodoma. Mkoa wa Dodoma pia ni maarufu kwa kilimo cha zabibu ambalo ni zao muhimu la biashara kwa wakulima wa Dodoma. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti Kanda ya Kati Mtafiti Leon Mrosso, utafiti wa zao hilo umekiwa ukifanyika kituoni hapo kwa takribani miaka 30 sasa na kupata mafanikio makubwa yakiwemo uzalishaji wa aina bora za zabibu . Kwa mfano mwaka 2007 kituo kimeweza kutoa aina mbili za zabibu -Makutupora red na Chenin white ambazo zote ni za kutengeneza mvinyo. Kituo pia kinatafiti aina ya zabibu za kutafuna kama vile Makutupora white,Black Rose, na Regina. Pichani shamba la majaribio la zabibu kituoni Makutupora.

Vijana wanatengeneza Tanzania katika Soka

Jana tulipata taarifa kuwa Timu yetu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 wanaotetea ubingwa wa DUNIA wameanza vyema kutetea taji lao la ubingwa wa duniani mashindano ya Copa Cocacola kwa kuwachabanga vijana wa Ethiopia magoli 5 -0. Kwa vyovyote vile ni ushindi wa kujivunia. Wako wapi waandishi wa habari? Sio coverage kubwa ya michuano hii. Tusidharau vijana wanaanza kutengeneza jina la Tanzania katika Soka.

Mkoa wa Singida fursa bwelele


Kwa mtazamo wa wengi mkoa wa Singida ni mkoa wenye shida na usio na maendeleo. Wafanyakazi wanapopangiwa kufanya kazi kwenye mkoa hiuo hujiuliza mara mbili mbili niende au nisiende. Sababu ni nyingi lakini si za msingi hata kidogo. Wakati mwingine ni maneno ya vijiweni- aaa mwanangu Singida choka mbaya! Ndo vijana wanavyoita. Blog hii ilipokuwa Singida hivi karibuni ilikuta mambo tofauti kabisa. Singida ni mji mzuri tu barabara zake za mji wa Singida kwa sasa zinaboreshwa kwa kuwekwa rangi. Kuna majumba mazuri kabisa karibu na ziwa Singida. Kuna sehemu mbalimbali za burudani. Hivyo vijana msisite kufanya kazi Singida mbona mambo mazuri tu na fursa bwelelee. Kikubwa ukiishi Singida huwezi kupata Cholestrol kwani alizeti ni kwa wingi - Singida mkoa wa alizeti! Pichani jengo la Mkuu wa Mkoa Singida

Saranda imechongwa


Ule mlima uliokuwa ukiwasumbua madereva wanaolekea Singida wakitokea Dodoma unaojulikana kwa jina la Saranda sasa umechongwa na kuwekwa lami. Kwa wale waliosafiri zamani mlima huo ulileta ajali nyingi na kwalaza wasafiri wengi. Lakini sasa mambo safi. Blog hii ilipanda mlima huo kwa kutereza mwishoni mwa mwezi wa tano. Angalia pichani jinsi Saranda ilivyochongwa. Ama kweli Tanzania imepania kuboresha miundo mbinu yake ikiwemo barabara kuu.

Wednesday, June 3, 2009

Utafiti wa Mihogo Hombolo- "superb"


Ukipata bahati kutemebelea vishamba vya majaribio ya zao la muhogo vilivyopo kwenye kituo cha Utafiti cha Hombolo utaridhika kuwa watafiti wetu wanafanya kazi. Jaribio limeandaliwa vizuri na matokeo yako wazi kabisa. Maelezo ya wataalamu yanaridhisha kwa asilimia 100. Kweli utafiti wa muhogo Hombolo ni "superb" tusubiri kupelekwa kwa wakulima.

Zabibu za Makutupora


Ni wachache wanaofahamu kuwa hapa nchini wapo watafiti wanaoendesha utafiti wa zabibu zinazotumika kutengeneza kinywaji cha mvinyo.


Zabibu ni zao linalofanyiwa utafiti kituoni Makutupora kwa muda mrefu sasa. Kituoni hapo aina mbalimbali za zabibu zinafanyiwa utafiti pamoja na teknolojia nyingine za kustawisha zabibu iliziweze kutoa zabibu nyingi na bora na kumuongezea kipato mkulima wa zabibu nchini. Pichani inaonekana jaribio la zabibu kituoni Makutupora.

Maabara ya Utafiti-Ukiriguru


Maabara za kisasa ni moja ya miundo mbinu inayohitajika kwa ajili ya Utafiti wa Kilimo. Maabara ni lazima ziwe na vifaa vya kutosha vya kufanyia uchunguzi pamoja na wataalamu waliopata mafunzo ya kutosha kwa ajili ya shughuli hizo. Kwa kufanya hivyo shughuli za utafiti wa kilimo zinaweza kuimarika hapa nchini. Pichani moja ya maabara za utafiti zilizopo kituoni Ukiriguru, Mwanza.

Wanatafuta 'vogellii'


Liko wapi! Ndivyo wanavyoulizana wapelembaji na watathmini wa utafiti waliutumwa kanda ya Kati mwaka 2009 wakilitafuta gugu hatari linalojulikana kwa jina la 'vogellii' katika shamba la majaribio Hombolo-Dodoma.

Shughuli ya Hitima ya Marehemu Nassoro Makuka


Shughuli ya Hitima ina utaratibu wake na inakusanya watu wa aina mbalimbali wazee kwa vijana, wake kwa waume na watoto pia. Hivi karibuni nilihudhuria hitima ya marehemu Nassoro Makuka jirani yangu tuliyeishi naye kijijini Kisemvule. Hitima hiyo ilifanyika nyumbani kwao kitongojini Mpera si mbali sana kutoka Kisemvule. Watu walifurika kwa wingi. Licha ya mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo, shughuli ya hitima ilikwenda vizuri sana. Sala iliendeshwa na mashehe nguli baada ya hapo sadaka ilitolewa. Mpangilio mzuri wa kugawa chakula ulifanyika bila bugudha. Pichani umati wa watu wakiwa tayari kupata sadaka. Mungu aiweke pema roho ya marehemu Nassoro bin Makuka.
Amina

Mtama kutoa nishati


Watafiti wa Kituo cha Utafiti Hombolo wakishirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kanda Kame (ICRISAT) wanaendelea na utafiti wa aina ya mtama utakaoweza kutoa nishati ya kuendeshea mitambo. Utafiti huo unaendelea vizuri katika vijashamba vya majaribio kituoni Hombolo. Pichani aina ya mtama yenye kutoa mabua yaliyo na sukari katika majaribio.

Anapelemba na Kutathmini


Kiongozi wa Timu ya Kupelemba na Kutathmini shughuli za Utafiti Kanda ya Kati mwaka 2009. Dkt. Ally Mbwana akiwa pamoja na wakulima/wafugaji wa kijiji cha Chamkoroma Wilayani Mpwapwa-Dodoma akiwahoji wanakikundi wa uboreshaji wa wa kuku wa asili mwezi Mei 2009.

Tuesday, June 2, 2009

Watafiti na alizeti


Watafiti wa Kilimo kanda ya kati wanafanya kila njia kuboresha uzalishaji wa zao la alizeti ili liweze kumuongezea mkulima wa mikoa ya kati (Singida na Dodoma) pato lake kiuchumi. Tatizo ni soko la alizeti halina uhakika. Pichani Mtafiti Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Hombolo -Dodoma, Elias Letayo akiangalia kichwa cha alizeti.

Kuku Kishingo


Watafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Mifugo Mpwapwa wanaendelea kuboresha kuku wa kienyeji ili waweze kutoa mayai mengi, kukua kwa haraka pamoja na kuwa na uzito wa kutosha. Pichani jogoo kishingo akiwa kwenye banda.

Omari Shomari-Dereva Mwandamizi


Omari Dogo ndivyo anavyojulikana dereva mwandamizi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Omari ni dereva kijana lakini mwenye elimu ya kutosha na uzoefu wa muda mrefu katika uendeshaji wa Magari.


Dogo Omari anauzoefu wa zaidi ya miaka 15 ya uendeshaji gari katika ofisi za serikali. Mwaka wa jana alihitimu elimu ya Kidato cha Nne na umehudhiria kozi nyingi za muda mfupi hapa nchini.


Omari ameshasafiri karibu mikoa yote ya Tanzania Bara akiendesha magari madogo na makubwa. Ubora wa dereva Omari unatokana na jinsi anvyotunza gari, uendeshaji wa makini na kujali muda na vilevile ni mkweli katika kutenda kazi. Kijiko yeye atakiita kijiko na si umma.


Omari hujali familia ameoa na kubahatika watoto wawili wakike na kiume wanaosoma WhiteAngels English Medium Primary School - Kisemvule Vikindu Mkoa wa Pwani. Maskani yake ni Mbagala Charambe.