Friday, April 23, 2010

Jeuri ya Mourinho


Ukitaka kusikia ngebe za Mourinho kocha wa sasa wa Inter Milan subiri akufunge. Utasikia vibweka vyake maneno ya kajeri na mambo kadha wa kadha. Muone alivyofurahi wakati Inter ilipoifunga Barcelona mabao 3-1 mapema juma hili.

Tuwe makini kwa maneno ya kiswahili tunayoyatumia

Hebu soma sentensi hii "Huu ndiyo usafiri wetu hakuna kulemba tunaomba utulivu" Neno kulemba halina maana hapa kwani maana ya kulemba ni kumnyang'anya mtu kwa hila au kumhadaa mtu. Kama alitaka kuandika kuremba hata hivyo maana ya kuremba ni kutia mapambo kwenye kitu ili kipendeze machoni au kupamba.

Huyu ndiye Arjen Robben


Anafunga magoli pale usipotegemea anaweza kucheza namba saba lakini akakokota gozi kwa mguu wa kushoto na kuwatoka walinzi kama wamesimama. Ukimuona kwa sura utafikiri babu hivi lakini acha bwana! Huyu ndiye aliyeimaliza Manchester United. Si mwingine bali ni Arjen Robben mshambuliaji wa Bayern Munich ya Ujerumani.

Samaki wachache


Picha hii niliyoipata kwa hisani ya gazeti la Dailynews la tarehe 23/4/2010 imenikumbusha moja ya za uchumi ya demand na supply. Hivi samaki hawa wachache bei yake itakuwaje? Nipe jibu.

Huyu ndiye Iluminata James

Si kumbuki kama nilimfahamu Iluminata James siku za nyuma. Na sidhani kama mrembo huyu- Miss Universe anayemaliza muda wake ametangazwa kiasi cha kutosha. Lakini macho hayadanganyi Iluminata ni bomba sana!

Si rahisi kugundua albino mzungu

Hao weupe wawili kushoto kwako ni albinos kiswahili fasaha ya jina hilo sifahamu (mtanisamehe). Albinos hawa ni ndugu na wametoka Canada. Ona walivyowatanashati mbona huwezi kugundua kama walemavu wa ngozi. Katikati ni Vicky Mtetema Mkurugenzi Mtendaji Habari na Mausla ya Kimataifa wa Shirika linaloshughulikia uhamasashaji na utetezi Jamii, kuhusu ulemavu wa ngozi nchini (UTSS) akisaidia kuwatafsiria lugha albino hao wakati wa uzinduzi wa filamu inayoonyesha ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi ulifanyika jijini Dar Es Salaam hivi karibuni. Albinos wetu wakipatiwa huduma muhimu wanaweza kuwa kama hawa.

He kumbe aghali hivyo?


"Kuwekeza kwenye ICU siyo kitu rahisi.Gharama yake ni takribani sh 250 milioni kwa kitanda kimoja chenye huduma zote hizo." Maneno haya yalisemwa na Dk. Mpoki Ulisubisya. Dk.Mpoki aliyasema hayo kwenye maonyesho ya kuadhimisha miaka 10 ya lilokuwa Shrika la Afya Muhimbili ambalo sasa ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili yaliyofanyika wiki lililopita. Magonjwa yanayoongoza hapa nchini kwa kuwa na wagonjwa wanaolazimika kufikishwa ICU ni wale wenye matatizo ya kuwa na usaha tumboni, kifafa cha mimba, pepo punda, kiharusi, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo, walioumia kichwani, majeruhi wa ajali, figo, kisukari na watoto wenye shida katika njia ya hewa. ICU ni kifupi cha 'Intensive Care Unit' kwa kiingereza. Kweli ICU ni aghali lakini ni muhimu kwa maisha yetu.

Tuesday, April 20, 2010

Tunakunywa sote!

Shida ya maji. Wanyama na binadamu wote hutumia chanzo kimoja cha maji. Ndiyo, tunakunywa sote!

Sidanganyiki


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua mwenyewe daraja eneo la Kidibo wilayani Mpwapwa. Haongejei ripoti ofisini.

Mgosi umetimiza ahadi yako



Mgosi umeikamilisha kazi kwa kutingisha nyavu za watani mara mbili. Kuna nini tena? Umetupa raha ujue? Safi sana Musa Hassan Mgosi.

Mikeka


Watanzania wengi hutumia mikeka kwa shughuli mbalimbali.Kwenye sherehe na misiba na hata kwa kulalia. Mikeka pia ni pambo. Tudumishe utamaduni wa kusuka mikeka.

Moto tena!


Wanafunzi walizwa tena. Safari hii St. Anthony Secondary School Mbagala. Hostel ya wasichana yawaka moto. Mifumo yetu ya umeme pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara si shwari.

Kilwa Road yetu

Wakati mwingine huwa najiuliza 'tumerogwa'? Sipati jibu. Barabara ya Kilwa haina hata miaka mitano toka ijengwe upya. Hebu angalia mtaro ulivyogeuzwa dampo. Fikiria huo ni msaada kutoka JAPAN. Hivi wanatuelewa?

Saturday, April 17, 2010

Hizi ndizo athari za mabadiliko ya hali ya hewa


Ukame uliokithiri-Wanyama kufa, mazao kuzaa kiaina aina hivi (hebu angalia gunzi la mhindi). Pamoja na mafuriko si kwa Tanzania tu. Majanga haya hutokea sehemu mbalimbali za dunia yetu. Hili ni tatizo kwa maisha yetu sisi wanadamu. Tanzania tunalionaje hili. U tayari wetu upo wapi au hatuoni? Mafuriko ya Kilosa hivi karibuni ni moja ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Ndizi tamu kutoka Morogoro



Msichana mrembo amejitwikwa kitenga cha ndizi tamu za malindi kutoka milimani Morogoro kwenda kuuza mjini Morogoro. Tusiache aina hizi za ndizi zikapotea. Tuwezeshe watafiti waweze kutunza aina hizi za ndizi na kuzizalisha kwa wingi. Utajiri ndiyo huu. Licha ya kuliwa kama tunda, ndizi zinaweza kutengenezwa vinywaji vya aina mbalimbali.

Kila la kheri Simba Sports Club


Pamoja na kumkamia sana Emmanuel Okwi. Lazima kesho mnyama aue. Kila la Kheri Simba Sports Club.

Wadudu wanaoshambulia mazao shambani ni hatari


Kiasi kikubwa cha mazao yetu hushambuliwa na wadudu bado yakiwa shambani. Wadudu hawa wasipodhibitiwa mapema huathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao na hivyo kumpa hasara kubwa mkulima na kukata tamaa ya kuendelea na kilimo. Njia zifaazo zitumike kudhibiti wadudu mashambani. Muone mtaalamu wa kilimo aliye karibu nawe ili aweze kutoa ushauri sahihi.

Pipe irrigation system- Inawezekana


Umwagiliaji huu wa mabomba (pichani) unafanyika hapa nchini wilayani Mwanga. Ni umwagiliaji kwa kutumia mabomba. Ona mpangilio wa kulima mazao. Ona maji yalivyotegeshwa. Kwa hakika haya yote yanawezekana na kuweza kuongeza uzalishaji wa mazao.

Hivi maisha yanaongelewaje?- What is life?


Life is a challenge Meet it,
Life is a gift Accept it,
Life is an adventure Dare it,
Life is a sorrow Overcome it,
Life is a tragedy Face it,
Life is a duty Perform it,
Life is a game Play it,
Life is a mystery Unfold it,
Life is a song Sing it,
Life is an opportunity Take it,
Life is a journey Complete it,
Life is a promise Fulfil it,
Life is a love Enjoy it,
Life is a beauty Praise it,
Life is a spirit Realise it,
Life is a struggle Fight it,
Life is a puzzle Solve it
Life is a goal Achieve it

Mpaka bargashia idonndoke


Mambo yameanza kuiva pilika pilika za uchaguzi mwaka 2010 zimeanza kuna wanaojiandaa kwa vyombo vya usafiri, kuna wanaochapisha kanga, vitenge na fulana na kuna wanaojiptisha vilabani na kutoa ofa za kangala. Poa, mpaka kieleweke. Tutajinadi hadi kieleweke kama inavyoonekana pichani. Tukishapata. 'Business as usual'!

Kutoka ufugaji hadi kilimo cha mahindi


Lazima twende na mabadiliko. Wamasai hwa kutoka wilaya ya Ngorongoro wameamua kulima mahindi mwaka huu baada ya mifugo yao mingi kufa kutokana ukame uliyoikumba sehemu za wilaya yao msimu uliopita. Utamaduni haujasahaulika hata shambani!

Hebu soma hii ya tabasamu -'smile'

A smile costs nothing but gives much. It enriches those who receive without making poor those who give. It takes a moment, but the memory of it sometimes lasts forever. Ni KWELI. Jamani tutoe TABASAMU siyo kila wakati umenuna tua aka!

Nilitingwa na kazi



Ni muda mrefu sijatumbukiza chochote ndani ya Banzi wa Moro. Wasomaji wa blog hii wamenikosa kwa muda mrefu. Poleni sana kwa usumbufu. Ukweli ni kwamba nilitingwa na kazi za ofisini hivyo kukosa muda wa kuning'iza majambos! Sasa kazi zimepungua msikose kufungua blog hii.

Saturday, April 3, 2010

Wafugaji wa kesho?


Pamoja na mazingira waliyonayo (pichani) wameamua kufuga. Angalia walivyokumbatia mbuzi wao. Wanaleta matumaini huenda wakawa wafugaji wazuri wa kesho wakipatiwa utaalamu pamoja na kuwezeshwa.

Eriteria haitoki ng'o!


Kwa mazoezi haya, Eriteria haitoki ng'o! Angalia dada yetu akijifua golini kama K...... vile!

Ali Hassan Mwinyi na Azimio la Arusha


Rais wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa, kufilisika kwa mashirika zaidi ya 400 ya umma nchini kulitokana na waliokabidhiwa dhamana ya kuyaongoza pamoja na Watanzania kwa ujumla kutojua maana sahihi ya ujamaa. "Wengi wanadhani kuwa Azimio la Arusha limefutwa na wengine wanadai kuwa Azimio la Zanzibar ndilo lililofuta Azimio la ARUSHA, lakini ukweli ni kwamba Azimio la Arusha halijafa." Mwinyi aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Benki ya Mkombozi ya Kanisa Katoliki nchini iliyofanuyika jijini Dar Es Salaam tarehe 18 Machi 2010.