Wednesday, June 30, 2010

Mtaa wa Kongo wa Dar


Huu ndio mtaa wa Kongo. Watu ni wengi na mambo ni mengi.

Hivi ndivyo anavyokiri TEVEZ


"I know I was offside, I know it was selfish but as long as they say it was a goal it's OK for me and the team...." Haya yalisemwa na mwenyewe TEVEZ alipojiwa kuhusu goli lake moja alilogunga dhidi ya Mexico siku ya Jumatatu.

Vicent Enyeama ameonyesha uwezo mkubwa


Golikipa nambari wani wa Green Eagles ya Nigeria, Vicent Enyeama ameonyesha uwezo mkubwa katika mashindano ya Bingwa wa Dunia wa Soka yanayoendelea hivi sasa nchini Afrika ya Kusini ambayo ni mara ya kwanza kufanyika barani Afrika. Uwezo aliouonyesha Vicent ni wa ahali ya juu, licha ya timu yake kutolewa katika hatua za awali.

Anafikiria kuplemba na kutathmini utafiti

Dkt. Catherine Madata amebobea katika nyanja za uzalishaji wa maharage. Aidha kwa sasa ndiye Mkurugenzi wa Utafiti Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambako makao yake makuu ni kituo cha Utafiti wa Kilimo Uyole kilichoko Mbeya. Mwezi wa sita mwaka 2010 alikuwa kwenye timu iliyohusika na kupelemba na kuthatmini shughuli za Utafiti kanda ya Mashariki (vituo vya Utafiti Mikocheni, Kibaha, Mlingano,Utafiti wa Mifugo Tanga na Utafiti wa Ndorobo na Malare-Tanga). Pichani Dr. Madata yuko tayari kwa safari za kukagua shughuli za utafiti.

Mategemeo yetu ni kwa Ghana


Afrika imebakiza timu moja tu kwenye WOZA 2010 na si nyingine ni timu ya Taifa ya GHANA. Ghana wanaweza kufika mbali na kututoa kimasomaso Waafrika. Tuwaombee na kuwapa support.

Vita ya majambazi


Ukiwa jambazi utauwawa. Majambazi wanaendelea kuitikisa nchi hasa mijini. Hivi karibuni kikosi cha polisi cha mji wa Arusha kilipambana na majambazi na kufanikiwa kuwaua. Pichani (kwa hisani ya gazeti la mwananchi) majambazi waliouwawa wamelala milele!

Hii nayo kali


Eti naambiwa huyu aliyeko pichani ni mmoja wa mastaa wa filamu hapa nchini. Wadau nipeni jibu.

Hili lipo pia Dar


Nilishangaa kuona picha hii katika gazeti la mwananchi la tarehe 26/6/2010. Hii ni nyumba ya mkazi mmoja wa jijini anaitwa Yose Francis. Amekuwa akiishi katika mazingira haya kwa muda wa miaka 10 sasa. Makazi haya yako katika wilaya ya Temeke. Hebu jiulize huduma ya choo anaipata wapi mkazi huyu? Mamlaka zinazohusika zimelifumbia macho hili kwa muda wa miaka 10? Hii ni hatari.

Watafiti wa Mikocheni waanza kutafiti maembe


Watafiti wa kituo cha Utafiti Mikocheni kilichopo jijini Dar, wameanza kufanya utafiti wa uzalishaji wa maembe. Utafiti wao unalenga katika kupambana na nzi wa matunda (fruit fly) ambaye husababisha maembe kuoza na kupunguza ubora wa maembe na hatimaye kukosa soko ndani na nje ya nchi. Utafiti mwingine ni ule wa kutafuta aina bora za maembe kwa mahitaji mbalimbali. Tayari miche imeanza kuoteshwa katika kituo kidogo cha utafiti Mkuranga.

Tuesday, June 29, 2010

Mimi Karata yangu ni kwa JERUMANI!


Watu wananishangaa ninaposema kuwa karata yangu naichanga kwa JERUMANI. Ni kweli. Mimi sishabiki rangi kama bwana Mkwawa wa KILIMO.Wajerumani wameonyesha kandanda safi ya kujituma na yenye malengo. Angalia alivyochapwa MWINGEREZA! Kelele zote, majigambo yote kwisha yu wapi ROONEY?

Unapokaribishwa kwenye ukumbi wa mfugaji


Nilifurahi tulipokaribishwa kwenye ukumbi wa mikutano wa mmoja wa wafugaji waliopo Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Ndani ya ukumbi tulipata maelezo ya kina jinsi mfugaji anavyoendesha ufugaji wake na utaalamu anaoupata na kuutumia pamoja na changamoto zinazomkabili.

Safari ya kupelemba na kutathmini utafiti


Ni vizuri kuwatembelea wakulima kuweza kufahamu jinsi wanavyoendesha shughuli zao ili kufahamu mafanikio na changamoto zinazojitokeza. Shughuli hii inahitaji usafiri wa uhakika pamoja na vitendea kazi mbalimbali. Pichani wataalamu wakiwa katika safari ya kupelemba na kutathmini shughuli za Utafiti kanda ya Mashariki.

Utafiti wa muhogo kwa mkulima


Ili utafiti uweze kukubaliwa ni vema ukajaribiwa katika mazingira ya mkulima. Watafiti wa zao la muhogo katika kituo cha Utafiti wa Kilimo Kibaha wanafanyakazi karibu sana na wakulima. Huko visiga mkulima maarufu ambaye anajishghulisha na kilimo cha maembe na muhogo amekubali kufanya utafiti na watafiti hao. Tatizo kubwa la zao la muhogo ni soko. Mkulima huyo wa Visiga aliwafahamisha watafiti waliomtemmbelea shambani kwake mwezi Juni mwaka huu kuwa mwaka 2009 aliacha hekta 40 za muhogo zikitekea shambani kwa kukosa soko. Pichani linaonekana bango la IITA

Ningekuwa mtafiti ndama huyu angeitwa Lugoba


Timu ya watafiti mahiri wa sekta ya Kilimo ilipomtembelea mfugaji mmoja kata ya Lugoba wilaya ya Bagomoyo mkoani Pwani, katika zizi la wanyama wake tulimuona ndama huyu. Ndama huyu mwenye rangi nyeupe ni mzuri na mwenye afya. Ametokana na ng'ombe dume bora. Mimi ningekuwa mtafiti wa mifugo ningeanza kushughulika kuwapata ng'ombe wa aina hii tu na hatimaye kuwaita 'ng'ombe wa Lugoba.'

Vituo vya utafiti vyaanza kukarabatiwa


Serikali kwa kupitia Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo imeanza kukarabati vituo vya utafiti zikiwemo nyumba za wafanyakazi pamoja na miundo mbinu muhimu ya utafiti. Pichani nyumba ya wafanyakazi (Quarter C) iliyokarabatiwa katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Tanga (LRC-Tanga).Endapo ukarabati huu utaendelea kufanyika kila mwaka vituo vya utafiti vitakuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na hivyo kutoa matokeo yaliyokusudiwa na kusaidia kuleta maendeleo nchini.

Monday, June 28, 2010

Ng'ombe wa mfugaji Lugoba


Kijiji cha Lugoba mkoa wa Pwani ni cha wakulima na wafugaji. Katika shughuli za kupelemba na kutathmini shughuli za utafiti. Tulimtembelea mfugaji mmoja na kutueleza mengi kuhusu ufugaji mafanikio na changamoto anazozipata. Pichani ni baadhi ya ng'ombe wa mfugaji huyu ambaye kwa maneno yake mwenyewe amesema kuwa ng'ombe bora mwenye umri wa miaka mitatu aliyetunzwa vizuri anaweza kuwa na uzito wa kilo 500-600 ambaye anaweza kuuzwa sokoni kwa bei ya shilingi 1,000,000 hadi 1,500,000. We acha tu ufugaji unalipa.

Kwa wanaopenda kuvaa suti

No wardrobe of a man can be completed without including mens suit. The popularity and reputation of mens suits have long been widespread around the globe. Now, men suits are not only worn to make a style statement but also are a symbol of professionalism and distinctive character. There are various types of mens suits available in different style and pattern that can be worn according to the occasions.

Among different types of suits that are worn today the first is the dinner suit. It is part of a black tie suit which arose as a lounging alternative to dress coats in much the same way as the day lounge suit.

The second type of mens suits is business suits. A business suit is a lounge suit mostly preferred by businessmen. It is most suitable attire for men while going for conference, conducting meeting or any other business activity. There is a range of choices available in business suits in different style, color and fabric.The next type is wedding suits. Wedding suits are worn on special occasion like ceremony, marriage party etc. and displays esteem on special occasion. These suits are fusion of rare fabrics and classic style with an elegant touch. Another type is designer suits. Designer suits are one of most favorable choices of everybody. As fashion changes, these suits also changes from year to year and sometimes can be tricky to buy. These suits can be found in many different styles, materials and colors.

There are also vintage suits. Vintage suits usually consist of 3 pieces: the trousers, jacket, and vest. They can be found in many different colors and patterns, but will traditionally be made up of the same 2 materials that is wool or polyester. The list of mens suits is endless and it goes on and on like there are church suits, dress suits, classic suits, Italian suits and contemporary suits. In the market, mens suits are available for every occasion.If you are looking to buy a suit for you then the best place is online suits store. On these stores, you can check a huge variety of in popular colors like navy blue, black, charcoal gray etc. which are manufactured by top brands. Finding the perfect suit whether a business suit or wedding suit- at affordable prices has now become very easy on these online suits store.

Makala hii imeandikwa na Shaindera Singh

Thursday, June 24, 2010

Mwezi wa sita nilitingwa


Kama kuna mwezi ambao nimetingwa sana hadi sasa ni mwezi wa sita. Wasomaji wangu wa Banzi wa Moro hawajanisoma tangu mwezi uanze na sasa unakaribia kufikia ukingoni.

Kwa wasiofahamu huu ni mwisho wa mwaka wa serikali shughuli ni nyingi kweli kwa wafanyakazi wa serikali na ni kipindi hiki ambacho bajeti ya serikali husomwa kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. Mwezi huu wa sita nimeweza kusafiri kikazi kwenda mikoa ya Pwani (hususani Wilaya ya Mkuranga na Kibaha), Mkoa wa Tanga (Muheza na Pangani) kwa shughuli za kupelemba na kutathmini shughuli za utafiti wa kilimo hapa nchini.

Jana nimerudi kutoka Dodoma ambako nilihudhuria kikao cha Bunge ambacho Wizara ninayofanyia kazi iliwasilisha Bajeti yake na kupita siku hiyo hiyo bila mizengwe!

Kote nilikopita nimeona mengi na kujifunza mengi. Muda ukiruhusu nitawarushia baadhi ya yale niliyoyaona nikiwa huko.