Tuesday, August 31, 2010

Tumeshika kadi za bluu hakuna kulala


Nipo Afrika ya Kusini kwa warsha inayohusu habari na mawasiliano katika kilimo. Hapa kweli tuko kwenye w/shop ili tutoke na meza au stool. Hakuna kulala. Pichani nipo kwenye kundi la bluu tumepewa kazi tunatakiwa kutoa majibu lazima tuchonge stool! Maarifa hayaji hivi hivi hakuna kulala

Thursday, August 19, 2010

HONGERA YANGA!


Kama kuna siku wanayanga wamefurahi basi ni ya jana. Yanga imeweza kuishinda Simba Sports Club watoto wa Msimbazi kwa penati 3-1 na kubeba ngao ya Hisani. Lakini Asamoah kutoka Ghana hakufurukuta na ilibidi atolewe na kocha wake Papic. Ndo mpira!

Upendo wa Familia


Maisha ya waafrika ni ya familia iliyotanuka (Extended Family)mke watoto, wadogo, shemeji, wapwa, binamu na wengineo. Ndivyo tunavyoishi na tunapata raha sana na Mungu anatusaidia. Tunasaidia nao wawasaidie wengine. Hata sisi tulisaidiwa pia.

Cocacola na DAWASCO katika KILIMO KWANZA



Maonyesho ya NaneNane ya mwaka 2010 katika viwanja vya Mwl.J.K.Nyerere mkoani Morogoro yameleta mengi ya kujifunza kwa yale tusiyoyafahamu. Blog hii ilipata bahati ya kutembelea banda la Idara ya Mipango ya MATUMIZI bORA YA ardhi ya Kilimo na Hifadhi imeweza kuwashirikisha wakulima kutoka Tarafa ya Matombo, kata ya Kibungo Juu wanaoshiriki katika Mradi wa 'Equitable Payments for Watershed Services (EPWS) - Tanzania unaowezeshwa na CARE International-Tanzania kuonyesha teknolijia wanazotumia katika kuhifadhi ardhi ya milima ya Uluguru ambayo ni chanzo kikuu cha mto Ruvu ambao maji yake hutumiwa na wadau mbalimbali kama vile Kampuni ya CoCaCola na DAWASCO. Kampuni hizi kwa kupitia mikataba maalumu kati yao na vikundi vya wakulima huwalipa wakulima katika jitahada zao za kuhifadhi ardhi na vyanzo vya maji. Hapa ndipo ile dhana ya 'Public Private Partnership'katika kilimo inapojionyesha katika uhalisia wake.

Choroko zawapatia wakulima wa Nanyumbu bilioni 1.5



Habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 19 Agosti 2010 ukurasa wa 5 kuhusu choroko zinasisimua na kuhamasisha kulima. Hebu fikiria zao la choroko lilivyoweza kuwaingizia wakulima wa wilaya ya Nanyumbu kipato cha shilingi bilioni 1.5 msimu uliopita. Kwa kweli hiki ni kiasi kingi cha fedha. Kwa mazoea, wakulima wa Nanyumbu hutegemea Korosho kama zao la biashara. Msimu uliopita kilo ya choroko ilinunuliwa kwa shilingi 1,500 wakati korosho zilinunuliwa kwa shilingi 994 kwa kilo. Hii inatupa picha kuwa si lazima ulime mahindi au mpunga ili uweze kupata kipato na kuboresha maisha yako, choroko nazo zinalipa tena sana!

Wednesday, August 4, 2010

Ilipasa kuchunguza kadi kwa makini


Inasemekana kuwa kadi nyingi za wanachama wa CCM walikwenda kupiga kura za maoni kuwapata wagombea wa CCM walikuwa na Kadi mpya itawezekana wapi wengi wanachama wajiunge mwaka huu ndo maana ilibidi kuchunguza kadi kwa makini.

Huwezi kuamini kuwa hawa wamebwagwa!


Ndiyo, Shamasa Mwangunga, Dr.Mwamtumu Mahiza na Alfred Tibaigana wamebwagwa katika kinyang'anyiro cha kuwania ubunge kupitia CCM.

Hakuna sababu ya kuogopa HISABATI


WANAFUNZI walio wengi wanaogopa hesabu kwa sababu hawapati msingi mzuri. HISABATI si somo gumu kama mwanafunzi atafundishwa na mwalimu anayejua kufundisha na kulielewa somo la hesabu.Ili uweze kukotoa vizuri lazima ufahamu kanuni za hesabu. HESABU HUENDA NA KANUNI (FORMULAE)!

Utaratibu mzuri wa kupanda mabus ya wanafunzi unahitajiwa


NDIYO, Bank ya CRDB imetoa mabus machache kwa ajili ya wanafunzi wa jiji la Dar Es Salaam. Pamoja na kuwa na mabus hayo bado wanafunzi hugombania wakati wa kupanda mabus hayo. Kwanini kusiwepo utaratibu mzuri wa kuingia kwenye mabus hayo? Njia rahisi ni kwa wanafunzi kujipanga katika mstari. Aliyewahi ndiye atakuwa wa kwanza kupanda gari. Wanafunzi mkifanya hivi hata abiria wengine wataiga kwenye vituo vya mabus. Mnapogombania bus kuna hatari ya kuchana sare zenu za shule, kuchafuka, kuibiwa, kuchana vitabu na madaftari na wakati mwingine hata kuumia na kuzua ugomvi usio na sababu.

Nililipenda somo la Baiolojia


Somo la Baiolojia ndilo lililonipeleka kwenye sekta ya KILIMO.Nililifanya vizuri nikiwa "O" Level na kunipeleka "A" Level. Kutoka "A" nikaenda kusomea Crops Production (Diploma) kule Ukiriguru - MWANZA.Baadaye kwenye elimu ya juu nikabobea kwenye UCHUMI kilimo. Nilipokuwa "O" LEVEL nilizifahamu barabara sehemu kuu za ua.

Anajifunza biashara


Picha hii nimeipata kwa hisani ya gazeti la Daily News toleo la tarehe 4/8/2010. Nimeipenda kwa kumwona mtoto huyu akijifunza kupanga bidhaa zinazouzwa na mzazi wake. Angalia anavyopanga limau huku akielezwa na mzazi wake. Hakika mtoto huyu anajifunza biashara.

Rasimu ya Katiba Mpya majibu leo Kenya


KUNA makundi makubwa mawili nchini Kenya kuhusu mabadiliko ya Katiba ya KENYA kuna wale wanaosema NDIYO na wale wanaosema HAPANA. Makundi haya yanapigiwa debe na vigogo wakubwa wawili Kibaki kundi la NDIYO na lile linalosema "NO" linapigiwa debe na aliyewahi kuwa Rais wa Kenya Daniel Troitch Arap Moi. Makundi haya yanapigana vijembe kweli kweli kuna mawaziri wa Serikali ya Moi wanaoipinga Rasimu ya katiba hiyo pia.

Kocha Poulsen amrudisha Kaseja Taifa Stars


Kocha mpya wa Taifa Stars Mdenish Jan Poulsen amemrudisha Juma Kaseja katika kikosi cha Taifa Stars. Kaseja anaaminika kuwa ni golikipa nambari moja kwa sasa nchini Tanzania, hata kwa kipindi kirefu sasa hajaonekana langoni akiichezea Taifa Stars kwa kile kilichodaiwa na kocha wa zamani Maxio Maximo kuwa ni mtovu wa nidhamu.Hii ni nafasi pekee kwa Kaseja kuwadhihirishia Watanzania kuwa haikuwa kweli, na inampasa kujituma ili aweze kupata namba ya kudumu katika Taifa Stars.

John Waziri ashinda Kichangani


Habari za uhakika ambazo Banzi wa Moro imezipokea muda mfupi uliopita zinaeleza kuwa John Raphael Waziri ameshinda katika kura za maoni za kumpta mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro. John ambaye ni mtoto wa mkulima kutoka Matombo, Morogoro na mkazi wa Kichangani katika manispaa hiyo amewabwaga wapinzani wake kwa tofauti ya kura nyingi.

Tuesday, August 3, 2010

Safari ya Dutumi


Bado kuna shida ya usafiri kutoka Morogoro kwenda Dutumi. Picha hii imepatikana kwenye gazeti la Mwananchi la leo likielezea kuwa wasafiri wakipanda lori kutoka Mtamba, Morogoro kwenda Dutumi. Mbunge atakayechaguliwa wa jimbo la Morogoro Kusini ana kazi ya kuhakikisha kuwa anaboresha miundombinu ya usafiri kwenye jimbo lake.

Huyu ndiye aliyemshinda Mzee Malecela


Kama ufahamu, Livingstone Lusinde ameweza kumbwaga mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mhe. John Malecela kwenye kura za maoni zilizofanyika Jumapili iliyopita.Unatakiwa kuthubutu tu. Tusiogope.

Phiri arejea Msimbazi


Kazi kwisha mwanangu, Phiri ametua Msimbazi ili aje awauwe watu. Si unaujua mchakamchaka wake ni pointi tatu kutoka mwanzo! Je, watani watatoka tarehe 14 Agosti. Hebu muone mzee wa mipango Nyange a.k.a Kaburu. Si ndo amekwenda kumpokea Phiri kule Ukonga.

Shule Je?


Mvulana huyu alitakuwa kuwa shuleni kama si Sekondari basi Msingi lakini amekuwa mmachinga wa karanga za kukaanga. Je, biashara hii ni ya kwake au ametumwa? Kweli biashara hii itamkwamua. Sidhani. Na kama ndivyo basi biashara hii iboreshwe zaidi, angalia karanga zilivyotungwa kweli hazivutii kuzinunua. Elimu ya biashara ni muhimu pia.