Friday, January 28, 2011

Wengi hawafahamu Chuo cha Utumishi wa Umma


Wengi wamezoea kukiita Chuo cha Maskretari-Magogoni chini ya Idara Kuu ya Utumishi. Sasa Chuo hicho kinaitwa Chuo cha Utumishi wa UMMA. Chuo hiki kilianzishwa kama wakala wa Serikali chini ya Sheria ya Uwakala wa Serikali ya mwaka 1997. Wakala huu ulizinduliwa rasmi mwezi Agosti 2000 kupitia mpango wa Uboreshaji Utumishi wa Umma (PSRP).Programu ya uboreshaji utumishi wa umma kuwa chombo chenye uwezo, taratibu na utamaduni mpya wa utoaji huduma kwa ubora na ufanisi zaidi.

Thursday, January 27, 2011

Subiri MNYAMA utafukuzwa Yanga


Papic kocha mahiri Yanga amejiuzulu. Eti kocha sasa ni Fred Felix Minziro. Ole wako uufungwe na mnyama utafukuzwa tu!

Kingo haeleweki


Hivi huwa unamuelewa Kingo kweli? Jamani Kingo haeleweki. Hivi ni kweli kung'oa shoka hadi uunguze kigogo? Sasa kuni itatoka wapi si hata gogo lililokuwa linapasuliwa litaungua? Kingo haeleweki.

Hata Waziri anakagua nyama


Tangu achaguliwe kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Dkt. Mathayo David Mathayo amelivalia njuga suala la usafi wa machinjio mpaka kieleweke. Hivi ndivyo inavyotakiwa. Anataka kuona walaji wanapata nyama bora. Pichani anaonekana akikagua machinjio ya kisasa ya Kizota mjini Dodoma (Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi-27/1/2011)

Goodwill UNICEF Ambassador


Angelique Kpasseloko Hinto Hounsinou Kandjo Manta Zogbin Kidjo she has been a UNICEF Goodwill Ambassador since 2002.

Yatima sawa-Mazingira je?


Siwezi kubisha kuwa aliyeongoza katika mtihani wa kidato cha nne ni msichana Lucylight Mallya ambaye ni yatima. Lakini msichana huyu amesoma katika moja ya shule bora nchini za sekondari St. Marian iliyopo mkoa wa Pwani. Isitoshe hata picha hiyo inaonyesha kwao (ukoo wao) anakoishi kumetulia. Hebu check shangingi lilivyotulia kwenye garden. Tunamtaka yatima atakayeongoza kutoka shule za kata!

Wednesday, January 26, 2011

Noti mpya tena!

Jana katika pitapita zangu mitaani nilifika pale Tahfif kupata mahitaji ya clear packets (mifuko ya kutunzia maandiko nakusomeka-tafsiri yangu). Pale nilimkuta mama mmoja naye akipata mahitaji yake. Mhudumu wa duka alipomrudishia 'change' akampa na noti mpya na kumtahadharisha kuwa ikidondokea maji tu basi itakuwa imeshaharibika. Kusikia hivyo yule mama akairudisha ile noti mpya. Mimi nikashangaa kusikia hilo na sikuamini. Baadaye mchana wakati nakula chakula cha mchana nikasikia habari hiyohiyo kuwa noti mpya ubora wake ni wa hali ya chini ukilinganisha na noti za zamani. Hivi ni kweli hapa ndipo tulipofikia? Tatizo la umeme liko nje ya uwezo wetu. Hata kutengeneza noti tumeamua kuwa na noti zinazochuja?

Hebu soma habari hii ya kutoka Kigali Rwanda

Wanatosa
Niko huku Butare Rwanda kuwafundisha mambo ya forodha hawa jamaa wenye shingo ndefu yaani hapa ni typical Ipamba. Huku jamani miji ni misafi hakuna mfano. Yaani tolauwanja wa ndege hadi huku niliko kama kilomita 150 toka Kigali, ni kusafi na maua utafikiri mtoni kwa mama bustani. Siwezi kuelezea. Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi Mhe Rais na wananchi wote wanashika fagio na hakuna gari kutembea barabarani. Ukiwa unasafiri siku hiyo utajiju. Kama Mstahiki Meya Masaburi na Jerry Silaa akaamua na wenzao wa Temeke na Kinondoni kufanya zoezi hilo Dar itkuwa mbinguni yaani Lupalama, hakuna harufu ni upepo tu. Kuna manispaa moja ilianzisha lakini haikufanikiwa kwani lazima manispaa zote zishirikiane. Mbona kule kwetu Moshi wameweza? (alaa Nyange unacheka nini si nimeoa huk?. Biblia nasema mtu atamwacha babaye ataambatana na mkewe siyo mke ataambatana na mumewe. Duu ishakuwa ishu kwaBanzi)iNimewasiliana na Ahmed Rashid Tagambwaga aliyeko Sitzerland ameona gele sana tulivyokutana. Address yake ni mhehear@yahoo.com
Mr. George Israel Mnyitafu

Thursday, January 20, 2011

Hicho kikombe cha kijani ni cha nini?


Kwa sisi tunaojua kula mafenesi. Hicho kikombe cha kijani kimwekwa mafuta ya kula. Kwa kuwa mafenesi yana utomvu hivyo ukitaka kula fenesi kwanza ni vyema ukachovya vidole vyako kwenye mafuta kwa kufanya hivyo utomvu hautoganda vidole na hivyo kufaidi fenesi (local knowledge). Mafenesi kama haya kutoka Morogoro ni matamu sana lakini hayana bei. Hebu fikiria fenesi moja huuzwa kwa bei ya shilingi 1000 na 2500 kweli inalipa?

WanaTosa wakutana Peacock


Wataalamu na wafanya biashara 12 waliosoma Tosamaganga High School miaka ya mwisho ya 70 walikutana jijini katika Hotel ya Peacock kwa lengo la kumpongeza mwanatosa mwenzao Dr.Haji Mponda kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Aidha walitumia fursa hiyo kumpongeza pia Dr.Florence Turuka ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia.

Wanatosa hao walimweleza bayana Waziri huyo kuwa wanajivunia kuona kuwa TOSA imetoa zao ambalo limeonekana kufaa kuongoza katika moja ya sekta muhimu nchini (AFYA). Walimsihi Waziri kuhakikisha kuwa anaacha 'legacy' katika Wizara hiyo. Waziri aliwawakikishishia wanaTosa kuwa hatowaangusha na yupo tayari kupokea ushauri utakaomsaidia kufanya kazi yake kwa ufasaha zaidi. Pichani G.Mnyitafu (NGI) mmoja wa waratibu wa shughuli akizungumza kwa niaba ya wanatosa katikati ni Waziri Mponda na Kushoto ni Dr.Turuka.

Monday, January 10, 2011

2010 nimening'iniza 314 ndani ya Banzi wa Moro

Pamoja na matatizo ya kukatika kwa umeme, mtandao kukorofisha, camera yangu kuharibika na kubanwa na shughuli za kikazi. Hata hivyo, nimeweza kuning'iniza habari 314 ndani ya Banzi wa Moro. Nimevunja rekodi ya mwaka 2009 YA HABARI 250.Nilibakiza 55 tu nifikishe wastani wa habari moja kwa siku. NAJIPONGEZA!

Jamani huyu anaweza kuwa Mchagga!


Mmiliki wa mtandao wa Wikileaks anajulikana kwa jina la Assange. Hivi huyu kweli si Assenga mchagga?

He hata Marekani kuna Kunguni


Marekani nao wanasumbuliwa na kunguni

Hatimaye Mbagala R3 imepata ufumbuzi

Dereva anayepiga U-turn pale Mbagala Rangi Tatu karibu na kituo cha mafuta - fine ni sh. 50,000/- Madereva wanashikishwa adabu na sasa hakuna msongamano wa magari tena. Kumbe tatizo ni utaratibu na siyo ubovu wa barabara. Lakini leo hii kuna madereva wameanza kupiga U-turn baada ya kuona kuwa hakuna askari wa usalama wa barabarani. Hivi Watanzania tunataka tuchungwe kama wanyama?

Tuesday, January 4, 2011

Hivi ni halali kweli magari ya mafuta kutumia Kilwa Road

Amini usiamini kuna mlolongo wa magari makubwa yanayotokea Kigamboni na kupitia barabara ya Kilwa yakitokea Kongowe hivyo kusababisha msongamano wa magari kuanzia Mbagala Rangi Tatu hadi Kizuiani. Aidha, barabara hiyo haikujengwa kwa kupitisha magari yenye uzito mkubwa. Tutegemee nini hivi karibuni?

Barabara itaanza kuwa na mabonde na milima na hatimaye kushindwa kupitika. Mipango yetu na matumizi vioane. Tujiulize, hivi ni nani aliyeruhusu kujengwa visima vya mafuta ukivuka Kigamboni?

Katiba Mpya sawa uelewa je?

Ni kweli kuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa mazingira ya sasa. Lakini wanaoipigia debe si wananchi wa kawaida. "Wajanja wanatafuta ajira hasa wasomi kwa gharama ya walalahoi." Nilimsikia jamaa mmoja akinena nikiwa ndani ya Daladala juzi Jumapili.

Watanzania si Wavivu

Jumapili tarehe 2/1/2011 nilimtemebelea mzee wangu Mapunda kule Yombo Dovya. Nikiwa ndani ya daladala niliona wananchi wakishughulika na shughuli mbalimbali. Kuna waliokuwa wakiuza mitumba, kuna akina mama waliokuwa wakiuza korosho za kukaanga,samaki wa kukaanga, wengine walikuwa wakiuza mananasi na maembe.

Nikajiuliza jana mwaka mpya leo jumapili lakini hakuna anayepumzika. Abiria mwenzangu alinijibu anayesema Watanzania wavivu hajui alisemalo. Hivi utalalaje wakati hujui utakula nini? Utastarehe vipi wakati senti mfukoni hakuna?Wanaosema hivyo ni kukejeli wananchi! Watanzania si wavivu wanatakiwa kutengenezewa mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Mwaka 2011 wa changamoto

Nimeuanza mwaka 2011 kwa changamoto nyingi. Kubwa zaidi ni kwamba mwaka 2010 haukuisha vizuri kwa upande wa mawasiliano. Nina matatizo makubwa kimtandao hivyo kushindwa kuwasiliAna nanyi hadi mwaka huu ulipokwisha.

Tatizo jingine ni kukatika kwa umeme mara kwa mara. Hata hivyo leo nimejitahidi kuweza kupata fursa ya kuweza kurusha hii ya kwanza kavukavu. Ni kweli mwaka 2011 umeanza na changamoto nyingi. Lakini nyingi ni zile zile. Hivi kweli Watanzania tunashindwa kutatua matatizo yetu hata yale ambayo ni mepesi tu. Tusiwe wavivu kiasi hicho. Mwaka 2011 uwe wa kuchapa kazi zaidi kupambana na changamoto zinazotukabili.

Nawashukuru sana wasomaji wangu wa Banzi wa Moro. Big up kwa wale waliokuwa wanaochangia mada hasa Mwana IT - BELO!

HERI YA MWAKA MPYA