Friday, April 29, 2011

Watoto wa Utatu walikuwepo

Watoto wa Utatu Mtakatifu walitoa burudani ya pekee kwenye misa takatatifu ya Pasaka iliyoongozwa na Mhasahamu Askofu Kardinali Polycarp Pengo katika Parokia ya Vikindu.

Ilikuwa Pasaka ya kukumbukwa kwa waumini wa Parokia ya Vikindu

Sikukuu ya Pasaka.Maandamano yanaingia Kanisani

Thursday, April 21, 2011

Mambo ya kompyuta hayo

Wanasoma St. Vincent Nursery School Kisemvule


Kutoka kulia Maria Banzi na Asia watoto wa Kisemvule, Mkuranga mkoa wa Pwani wanasoma St. Vincent Nursery School Vikindu.

Mtoto Asia wa Ksemvule

TUGHE-KILIMO YACHAGUA VIONGOZI




Tarehe 13/4/2011 Tawi la TUGHE Kilimo Makao Makuu lilifanya Uchaguzi wake Mkuu kwa Halmashauri Kuu ya Tawi. Bw. Lazaro Kitandu (Afisa Kilimo Mkuu) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Bw.Abdallah Mbonde (Msaidizi wa Ofisi Mkuu) alichaguliwa kuwa Katibu. Viongozi hao pamoja na wajumbe Takribani 13 wa Halmashauri Kuu wataongoza Tawi kwa kipindi cha miaka 5.Banzi wa Moro inawapongeza na kuwatakia mafanikio. Picha wanachama katika mkutano wa uchaguzi.

Wednesday, April 20, 2011

Mama wa Kise Kids Soccer Club


Meneja wa Kise Kids Soccer Club, Mama Makope akikabidhi zawadi ya Mpira kwa wachezaji wa Timu hiyo baada ya kuibuka washindi wa Tatu kwenye mashindano ya Ksemvule Cup yalifanyika mwezi Machi 2011

Anapenda kubukua


Huyu ndiye Maria Mwaka Banzi. Anasoma KG3 St. Vincent Nursery School Vikindu.Anatarajia kuhitimu mwezi Septemba mwaka huu. Kweli Maria anapenda kubukua!

Dada Ana mambo!


Anastazia Mdimi a.k.a. Dada Dodo!

Mt. Joseph tulibarikiwa kwa vipaji


Ni mkusanyiko wa vipaji, bata (live), sabuni, fyekeo, kausho,juice. mifagio, fedha n.k. vilitolewa Jumapili ya Matawi na Jumuiya ya Mt. Joseph Parokia ya Vikindu.

Anatafakari


Mama Beatrice akitafakari jambo.

Nasaidia kufungua bahasha


Mama Mdimi alipewa bahasha asaidie kuifungua tusome ujumbe.

Tukio linawahusu

Lazima wawepo.

Mzee Mdimi karatasi hizo nyekundu ni za nini?

Sikieni Matangazo


Mwenyekiti Msaidizi wa Kigango cha Vikindu, Parokia ya Vikindu. Bw. Mwambeleko a.k.a Mwambe akitoa matangazo Jumapili ya Matawi.

Mpiga kinanda wa Kwaya ya St. Vincent De Paulo Vikindu


Ukibahatika kusali Parokia ya Vikindu utasikia sauti nzuri ya kinanda kutoka kwa mpiga kinanda mahili wa kwaya ya Mt. Vincent wa Paulo. Pichani anaonekana akikoleza mambo Jumapili ya matawi.

WANAJIANDAA KWA VIPAJI


Sikukuu ya Matawi ilifana sana Parokiani Vikindu. Jumuiya ya Mt. Joseph walijipanga vizuri. Muone mtoto John Mengi akiwa na Bata wake tayari kwa kutoa vipaji.

Waumini walitoa sadaka

E Bwana unioshe kabisa mikono yangu

MASISTA NDANI YA KANISA LA ST.VINCENT DE PAUL VIKINDU

Tulisali pamoja na masista.

Tuesday, April 19, 2011

Paroko Tom alihubiri


Paroko Tom katika mahubiri yake wakati wa sikukuu ya Matawi alitoa ujumbe mzito kuwa ni mara ngapi tuna mkana Kristo kama vile Petro alivyomkana Yesu. Alitusihi tuishi kama Wakristu na kuonyesha matendo mema. Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristu tuyatafakari kwa kina wakati tukijiandaa kwa PASAKA.

Injili Mt. Mathayo Sura 14-27



Hii ni injili inayokumbusha mateso ya Bw wetu Yesu Kristu. Waumini wa Vikindu walisoma Injili hiyo wakishirikiana na Paroko wao.

Waimbaji walimsifu Mungu


Waliimba kwa shangwe na kumsifu Mungu wetu aliyetuumba.

Paroko anafungua lango kuu la Kanisa St. Vicent Vikindu


Maandamano yaliishia kwa kuingia kanisani tayari kwa ibada takatifu.

Amepanda punda mwana wa Mungu


Jana Jumapili (17/4/2011) Wakristu wote Duniani walisherehekea sikukuu ya matawi. Waumini wa Parokia ya Vikindu Jimbo kuu la Dar Es Salaam kabla ya ibada takatifu walifanya maandamano huku wakipungia matawi na msalaba ukituongoza.

Friday, April 1, 2011

Wageni karibuni harusini


Waswahili husema shughuli ni watu. Ndivyo inavyokuwa katika shughuli za kizaramo. Pichani ndugu wa Bw. Harusi wakikaribishwa nyumbani kwa bi harusi mtarajiwa.

Huyu ndiye aliyekuwa akichezewa dufu


Bi Harusi wa Kizaramo

Dufu show


Dufu huchezwa na vijana wakiume pia.

Dufu manjonjo


Akina dada hucheza dufu kwa manjonjo.

Dufu


Dufu ni aina ya ngoma itumiwayo katika kisomo cha maulid kwa dini ya kiislamu. Hivi sasa jijini huku Pwani kuna vikundi mbalimbali vya kutumbuiza wakati wa kisomo cha maulid. Hakika dufu imebadilika sana na huchezwa kwa staili tofauti na za kusisimua

Mzee Juma wa Kisemvule


Kila kijiji hakikosi wazee. Kijijini Kisemvule kuna mzee mmoja al maarufu wa jina la Juma. Mzee Juma ni mchacharikaji sana katika maisha. Licha ya kujenga nyumba yake ametoa eneo ili msikiti wa kisasa uweze kujengwa na waamini wafanye Ibada. Pichani Mzee Juma akiwa karibu kabisa na msikiti aliosimamia kujengwa hapo kijijini. Msikiti huu upo karibu sana na shule ya msingi Kisemvule.

Tuwafundishe watoto wetu kupenda kazi


Banzi wa Moro ilimkuta Maria Banzi katika harakati ya kumwagilia maji bustani ya maua nyumbani kwao Kisemvule, Mkuranga.