Wednesday, October 31, 2012

Tanga kunani?

Hili ndilo jiji la Tanga. Jiji lililotulia, halina foleni za magari, mitaa ni misafi na nyumba zimejengwa kwa kumfuata mpango miji.

Mkaa bidhaa ghali jijini Dar Es Salaam

Bei ya mkaa jijini Dar Es Salaam inazidi kupanda siku hadi siku. Kwa sasa gunia moja linauzwa kati shilingi 30,0000/= hadi 35,0000/=. Gunia kama hilo pichani huuzwa kati shilingi 13,000/= hadi 15,000/= barabara ya Chalinze-Segera

Kijiji cha vigoda

Ukisafiri kwa kutumia barabara ya Chalinze Segera kwenye kijiji ulizia viti vya miguu mitatu yaani vigoda vinapatikana kwa wingi kwenye kijiji hiki.

Kaza nut!

Sasa uhakika wa usafiri upo. Hii ilikuwa ni safari yetu ya kutoka Arusha kurudi Dar. Kweli msafiri kafiri

Inabidi kulala uvungu wa gari

Wengine watarandaranda lakini mmoja ataingia chini ya uvungu kwa lengo la kubadilisha gurudumu

Gari pancha abiria nje

Unapopta pancha ukiwa safarini hali inakuwa hivi

Kazi hii nayo ni muhimu

Hivi karibuni katika tembeatembea zake jijini Arusha, mwandishi Livingstone Mwedipando aliinyaka picha hii. Fundi wa miundombinu ya simu akiwa amening'inia juu kabisa akirekebisha miundombinu. Ni hatari lakini ni kwa faida ya watumiaji. Kweli kila kazi ina umuhimu wake!

Barabara iendayo Nelso Mandela African Institute of Technologies

Huko linakoelekea lori ndiko kulikojengwa chuo cha Nelson Mandela-Arusha (Picha na Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Arusha 'beach' yao

Keepleft kilichopo karibu kabisa na Hotel ya Impala, Arusha maeneo ya Kijenge. Bustani hii inapendeza sana. Wakazi wa Arusha hutumia keepleft hiki kwa kujipumzisha na kwa kupata picha za kumbukumbu mbalimbali kama vile harusi. Ukweli ni kwamba hii ni'beach' ya wakazi wa jiji la Arusha!(Picha Na Livingstone Mwedipando- ARI Selian, Arusha)

Huree! Arusha sasa Jiji

Ndiyo, sasa Arusha imepata hadhi ya Jiji ni sawa kabisa na Dar Es Salaam,Mwanza,Tanga na Mbeya. Ukweli ni kwamba Arusha ina miundombinu mizuri ni jiji la kitalii na si uongo mzunguko wa fedha uko vizuri. (Picha na Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Tuesday, October 30, 2012

Na hii ni kutoka ziwa Nyasa

Wote tunatoka Ziwa Nyasa-Ukiwa Malawi au Tanzania, ngoma yetu ndiyo hii jamani.

Hii ni kizungu zaidi

Wanachagua mbegu za maharage

Katika kuhakikisha mbegu ya maharage inakuwa katika hali ya usafi tayari kwa kupanda ni muhimu kuzichagua vizuri zinazofaa kuondoa uchafu, udongo, vijimawe, mchanga na takataka zote. Pichani wafanyakazi wa Idara ya maharage kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo Selian, Arusha wakichagua mbegu za maharage tayari kwa msimu ujao. (Picha na Livingstone Mwedipando, ARI-Selian, Arusha)

Mmea wa Lukina (Leucena)

Nafikiri wengi tumeshauona mmea huu pengine na kudharau. Mmea huu ni chakula cha mifugo yako kwani majani yake yana viinilishe muhimu vinavyohitajika kwa mifugo. Mbuzi wa maziwa akilishwa majani ya mmea huu hutoa maziwa mengi.(Picha na Livingstone Mwedipando ARI- Selian, Arusha)

Friday, October 19, 2012

Wataalamu wakijadili Mradi wa EAAPP

Wasimamizi wa Mradi wa EAAPP wakiwa kwenye mkutano wa kupitia Taarifa za utekelezaji wa mradi huo ulifanyika mjini Morogoro hivi karibuni.

Maendeleo ya Mradi wa EAAPP

Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo (wa kwanaza kulia) akifuatilia kwa makini mawasilisho ya taarifa za maendeleo ya mradi wa EAAPP uliofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 15-16/10/2019

'Profate' yaanza mchakato wa ubia na serikali

Kampuni ya Usindikaji wa mazao yanayotokana na maziwa ijulikanayo kama Profate yenye makao makauu jijini Dar Es Salaam imeanza mkakati wa kushirikiana na serikali katika masuala ya kilimo. Moja ya wakurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Prosper Temu akiwasilisha pendekezo kw wataalamu wanaoshughulikia mradi wa EAAPP walikutana mjini Morogoro hivi karibuni.

MORO MJI KASORO BAHARI

Wapi hapa?

Wote tunashughulikia Kilimo

Pichani wanaoenekana baadhi ya madereva wa kilimo waliokuwa kwenye mkutano wa Mradi wa Kuongeza uzalishaji wa Kilimo kwa nchi za Afrika Mashariki (EAAPP) uliofanyika kuanzia tarehe 15-16/10/2012 mjini Morogoro. Aliyesimama wa kwanza kutoka kushoto ni Omari Shomari Kizito

Ugonjwa wa milia wa mahindi

Ugonjwa wa milia wa mahindi unavyoonekana kwenye jani la mahindi

Friday, October 12, 2012

Mkutano wa Kitaalamu

Pichani wataalamu wa kilimo pamoja na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano wa pamoja kuhusu shughuli za kilimo kanda ya Kaskazini (Picha na Livingstone Mwedipando- ARI-Selian, Arusha)

Umwagiliaji maji shambani kwa matone

Umwagiliaji maji mashambani kwa teknolojia ya matone (drip irrigation) ni nzuri hasa kwa kilimo cha mboga mboga kwani kiasi cha maji kidogo hutumika kuzalisha mazao kwa kuupa uhakika mmea wa kupata maji wakati unapoyahitaji. Teknolojia hii husaidia kuzalisha mazao kwa faida. Wataalamu wa kilimo wa umwagiliaji wanaweza kukusaidia kukupa maelezo ya kina kuhusu teknolojia hii.Ulizia Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika- Barabara ya Mandela/Kilimo- Temeke Veterinary, Halmashauri za wilaya, na Ofisi za Umwagiliaji za Kanda.

Hujuma TANESCO

Nguzo za TANESCO zilizoibwa na kufichwa huko Kigamboni jijini DAR. Hizi ni hujuma. Kwa maana hiyo kuna wateja wanauziwa nguzo kwa bei poa huku wateja waliotumia utaratibu wa kuvutiwa umeme wakisubiri kwa kuambiwa kuwa hakuna nguzo! (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog tarehe 12/10/2012)

Fikiri Madinda yupo

Fukiri Madinda (aliyesimama)yupo fit na anaendelea na kazi za ujenzi wa taifa

Raha ya nanasi ulichonge mwenyewe!

Nyumbani raha

Unapokuwa nyumbani kwako unajitanua unavyopenda

Anageuza nyama

Mchagga ni Mchagga tu. Wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2012.Mtoto huyu Dan Makishe, yeye alikuwa makini kuhakikisha kuwa nyama zinachomwa vizuri.

Uzinduzi wa Power Tiller - Arumeru

Wakulima wa kijiji cha Nduruma katika halmashauri ya Meru wilayani Arumeru siku ya uzinduzi wa Power Tiller waliyoipta kwa mkopo kupitia Halmashauri yao kutokana na juhudi zao katika kikundi cha uzalishaji wa nyanya kwa kutumia mbinu za udhibiti husishi wa visumbufu wa mimea (IPM) (Picha kwa hisani ya Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Thursday, October 11, 2012

Twiga alama ya Tanzania

Chukua noti ya shilingi 2,000/= chunguza kwa makini ina alama ya Twiga,Shirika letu la Ndege la Taifa (Air Tanzania) ina alama ya Twiga. Hakika, Twiga ni alama ya Taifa la Tanzania

Pricilla Nalitolela

Mratibu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) mkoani ARUSHA Bi. Pricilla Nalitolela akiwa makini kuweka kumbukumbu za mwenendo wa semina ya viongozi wa dini mkoani Arusha katika mapambano dhidi ya UKIMWI iliyofanyika jiji Arusha hivi karibuni.(Picha na maelezo- Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Askofu Peter Mwamasika akipambana na UKIMWI

Kamishna wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Askofu Dr. Peter Lukumbusho Mwamasika akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina ya viongozi wa dini dhidi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI iliyofanyika jijini Arsuha hivi karibuni (Picha na maelezo- Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Nyanya bila kemikali

Wakulima hawa ni miongoni mwa wakulima wanaozalisha nyanya kwa mbinu za udhibiti husishi wa visumbufu wa mmea (IPM) katika kiji cha Nduruma, Halamashauri ya Wialaya ya Meru. Kwa kutumia nyanya zilizozalishwa kwa njia hii, walaji hawawezi kupata madhara yanayotokana na kemikali yanayotumiwa na wazalishaji wengine wa nyanya.Utafiti huo hufanywa na Kituo cha Utafiti wa Mboga na Matunda - HORTI-Tengeru, Arusha. (Picha na maelezo kutoka kwa Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Hivi ni kweli?

Mtafiti shambani

Mtafiti Peter Xavier wa Kituo cha Utafiti Selian-Arusha akimuhoji mfugaji nyumbani kwake katika mazingira yake. Hivi ndivyo mtafiti anavyotakiwa kuwa. Watafiti wengine wanapika taarifa ofisini! (Picha kwa hisani ya Livingstone Mwedipando- ARI-Selian, Arusha)

Wamekwenda kumsalimia Monduli

Warembo wanaoutaka u Miss Tanzania (Redds) kwa mwaka 2012 wamemtambelea Mhe. E.Lowasa nyumbani kwake Monduli hivi karibuni (Picha kwa hisani ya gazeti la DailyNews 11/10/2012)

Tuesday, October 9, 2012

Mahikwi chanzo cha maji kwa mifugo

Sehemu ambazo maji kuhna uhaba mkubwa wa maji, mifugo huathirika zaidi. Si rahisi mtu kunywesha mifugo yake huku yeye hana maji. Utafiti uliokwishafanywa wa kutumia mahikwi (pichani) umedhihirisha kuwa wanyama wanaweza kutumia maji kutokana na mahikwi hivyo kutatua tatizo la maji kwa mifugo.

Monday, October 8, 2012

'MPINGO HOUSE'

Jengo la Makao MakuU ya Wizara ya Mali ya Asili na Utalii- 'MPINGO HOUSE' Jengo hili lipo jijini Dar karibu kabisa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali maeneo ya Keko- barabara ya Nyerere. Ni moja ya Wizara chache iliyopo nje kidogo ya jiji.

Nani zaidi?

Vitabu vilitolewa na mashindano ya kusoma yalianza. Nani zaidi? Kisemvule au Bunju?

Ndugu wamekutana

Jana tarehe 7/9/2012 niliwatembelea ndugu zangu waishio Bunju. Kule kuna dada zangu wawili wameolewa. Watoto wetu walikutana na walifurahi mno. Ni vizuri kuwaunganisha watoto wetu wafahamiane.

Shoppers Plaza

Moja ya maduka makubwa jijini DAR linalopatikana sehemu za Mikocheni. Enzi za utoto wangu marehemu shangazi yangu alikuwa akilima mpunga kwenye bonde lilikoibuka -Shoppers Plaza ama kweli hakuna kisichowezekana!

Hata na 'Diamond'!

Watoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa DAR-LIVE uliopo Mbagala hufurahia kupiga picha sambamba na picha za wasanii zilizobandikwa ndani ya ukumbi huo. Hawa waliona fahari kupiga picha na super star Diamond!

Au 'Linah'!

Unaweza pia kupiga picha na 'Linah' ukiwa DAR-LIVE

Waweza kupiga picha na 'Juma Nature'

Ukiwa DAR-LIVE unaweza kupiga picha na 'Juma Nature'

Vitu vya DAR-LIVE

'Pilot' wa kwanza wa kike Mluguru!

Huenda akawa pilot wa kwanza Mluguru. Hiki ndicho alichopenda mwanangu Maria Banzi alipotembelea DAR-LIVE - MBAGALA siku ya Jumamosi