Friday, November 23, 2012
Na hii ni harusi ya Kihaya
Hivi ndivyo ilivyokuwa reception ya Bw. Dianus Mutta iliyofanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill Temeke tarehe 27/10/2012.
Safari yenye bahati
Dada Appia alibahatika kushuhudia zoezi hili la kutoa mahari kwa kaka yake Macarios kabla ya kusafiri usiku wa tarehe 11/11/2012 kurudi Norway anakoishi hivi sasa
Mzee Mdimi alifurahi
Ujumbe kwenda Gongolamboto kwa lengo lakutoa mahari ya Bw.Macarios Banzi ilikuwa chini ya ushauri wa Mzee Mangengesa Mdimi. Wakati wote wa shughuli yeye alifurahi sana kwani shughuli zilikwenda kama tulivyopanga.
Vinywaji vilikuwepo
Waluguru wanasema shughuli 'mbwali.' Ndivyo ilivyokuwa wakati wakutoa mahari ya Bw. Macarios ilikuwa nipe nikupe pande zote zilifurahi na kupongezana kwa chakula na vinywaji!
Thursday, November 22, 2012
Kilichofuata baada ya kutoa mahari
Mama Cathy a.k.a Mrs Banzi wa Moro akizirudi na shemjie Dikupatile!
Renatus Banzi a.k.a bepari akifurahia tukio na kujimwaga uwanjani
Mshenga Bw. Lawrence Mkude akicheza kwa furaha baada ya kukamilisha shughuli.
Vimbwanga vya kwenye mahari
Kwenye kutoa mahari kulikuwa na vituko vya aina yake lakini hivi vyote vilifanywa kwa nia nzuri tu ya kusherehesha shughuli. Dada wa Macarios (Helmina Mwenda na Eddy Daulinge)walijitokeza na kumuonyesha Martina kuwa wao ndiyo wanawake zake Macarios na hawana habari yoyote ya kuchumbuiwa kwake.Fuatilia picha hizi kwa makini upate uhondo.
'Mke mkubwa' Helmina Mwenda akimlalia 'mumewe' Macarios Banzi akionyesha yeye ndiye zaidi
Ilibidi shangazi P.Mloka na kaka Inno waokoe jahazi, la sivyo shughuli 'ingeharibika'!
Wanajiandaa kuwasilisha mahari
Shangazi P.Mloka na Mshenga Bw. L.Mkude wakijiandaa kuwasilisha mahari ya Bw. Macarios Banzi mapema mwezi Novemba 2012 huko Gongolamboto.
Mmoja wa negotiatiors tuliokuwa nao kwenye msafara huo ni Baba yetu Mangengesa Mdimi (mwenye T-shirt nyeupe)mmmoja wa wandishi wakongwe hapa nchini.
Ufuta Je?
Hapa tuliambiwa kuleta ufuta pia uhusiano wake katika mahari mimi sijui lakini nafaikiri una maana yake. (Nitauliza baada ya mdogo wangu kufunga ndoa!)
Kukabidhi mablanketi
Moja ya vifaa tulivyotakiwa kutoa kwenye mahari ni mablanketi pichani shangazi wa Bw. Macarios Banzi Mama P.Mloka anakabidhi mablanketi.
Akina dada rukhsa
Akina dada wanaruhusiwa kuwa kwenye timu ya majadiliano wakati wa kutoa mahari. Pichani kutoka kushoto Eddy Daulinge na Suzy Banzi wakifuatilia kwa makini shughuli ya utoaji mahari kwa kaka yao Macarios Banzi huko Gongolamboto tarehe 11/11/2012
Timu yetu
Timu yetu ya majadiliano kwenye mahari ya Bw. Macarios Banzi iliongozwa na Bw. Lawrence Mkude wa Mbezi (Mwenye shati nyekundu)
Tunajipanga
Kabla ya kwenda kutoa mahari ya Macarios Banzi, kikao kilifanyika kwenye baa ya Mgaereza iitwayo 'Recreation' pale Gongolamboto ili tuweze kujipanga vizuri.
Tuesday, November 13, 2012
Chereko- Baba kapata Mama!
Baada ya shughuli ya mahari kwenye shughuli ya Macarios ilibidi ndugu waserebuke pichani kutoka kushoto dada Mwenda na Dada Appia wakicheza kwa furaha
Subscribe to:
Posts (Atom)