Monday, January 21, 2013
Magomeni bwana!
Jiji la Dar Es Salaam kila mmoja hujenga anavyopenda kutokana na uwezo wake pia.Unaweza ukajenga ghorofa na nyumba nyingine zikawa za kawaida kabisa hivyo wa ghorofani huona matukio yote kwenye nyumba za chini. Hapa ni Magomeni.
Hongera shemeji!
Ndivyo anavyosema Bw. L.Mkude wakati wa sherehe za kumuaga shemeji yake Hamisa Kasiba ndani ya ukumbi wa Deluxe, Sinza
Mzee Kasiba alizawadiwa shati
Ni nadra sana akina baba kutunzwa wakati wa sherehe za sendoff. Lakini kwa mzee Kasiba mambo yalikuwa tofauti kabisa, yeye alitunzwa shati wakati sherehe za kumuaga bintiye Hamisa ndani ya ukumbi wa Deluxe, Sinza.Angalia jinsi alivyokumbatia zwadi yake (Pichani-Mzee Kasiba aliyeketi na amefunga tai)
Kutunzwa imo
Mama Kasiba akiweka sawa kitenge alichotunzwa na mmoja wa marafiki zake siku ya kumuaga mwanae Hamisa. Katika sherehe kabambe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Deluxe- Sinza kijiweni, Dar Es Salaam, tarehe 11/01/2013.
Kibanda cha MC
Hapa MC alijengewa kibanda special kwa kujikinga na mvua pamoja na jua. Katika shughuli hii MC alikuwa mwanamke!
Hapa hakuna kadi ya mwaliko
Shughuli zetu za vijijini hazina ukumbi na wala hakuna kadi ya mwaliko. Hakuna cha kulalamika kuwa hujapata kinywaji.Unatakiwa kufika shughulini kuangalia na ikiwezekana kucheza. Hapa ni Kisemvule wakati wa shughuli iliyofanyika kwa jirani yangu.
Wednesday, January 16, 2013
Asante MC
Ukumbi wa Deluxe - Sinza Kijiweni na shughuli ile ya tarehe 11/1/2013 ya kumuaga Bi Hamisa Binti Kasiba inahitaji MC chakaramu kama huyo aliyeshika microphone!
Tuesday, January 15, 2013
Hamisa hii ndiyo Kamati yako ya Maandalizi
Hii ndiyo kamati iliyoandaa 'send off 'ya Hamisa Binti Kasiba iliyofanyika kwenye ukumbi wa Deluxe- Sinza Kijiweni, jijini Dar-Tanzania tarehe 11/1/2013.
Waalikwa sherehe ya Hamisa
Hawa ni baadhi ya waalikwa kwenye sherehe ya Send Off ya Bi. Hamisa Kasiba iliyofanyika katika ukumbi wa Deluxe - Sinza kijiweni jijini Dar, Tanzania, siku ya Ijumaa tarehe 11/01/2013.
Kuna waliokutana
Send off ya Hamisa imewakutanisha wengi kama hawa wanaonekana pichani.Kaka Mkude, dada na Mrs. Nancy Banzi ndani ya Deluxe Hall-Sinza kijiweni tarehe 11/1/2013.
Watoto wanasehemu yao
Si vyema kuandika kwenye kadi kuwa watoto hawaruhusiwi. Watoto wanasehemu yao katika sherehe ni burudani tosha wanashrehesha sherehe. Angalia hawa walivyopendeza wakiwa katika 'colours of the day' kama Banzi wa Moro. Safi sana. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye hafla ya kumuaga Bi. Hamisa binti Kasiba kwenye ukumbi wa Sinza Kijiweni jijini Dar - 11/1/2013. Tumejifunza nini hapa?
Wakati wa kukatika katika kati kati!
Ndiyo, ukihudhuria sherehe basi wakati wakukatika kati kati haya! Usione haya usijikunyate changamka jimwage! Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye ukumbi wa Deluxe- Sinza wakati wa hafla ya kumwaga Bi. Hamisa Kasiba siku ya Ijumaa tarehe 11/1/2013.
Hapo sasa!
Definitely hii ni bakurutu tu!
Mama na mwana
Hawa walinifurahisha sana pale ukumbuni Deluxe. Zai ni mdogo wa Hamisa na mtoto wa dada yao Salama (mwenye cap). walicheza kwa furaha. Lakini kilichonifurahisha zaidi kwa sare zao za wekundu wa msimbazi (colour of the day).
Mr.Mkude alikumbuka enzi zake
Ulipofika wakati wakujimwaga uwanjani Mr. Mkude na mkewe Sango walijimwaga katika ukumbi wa Deluxe - Sinza kijiweni na kuserebuka. Mkude ni shemeji wa Hamisa na Bi. Sango ni dada wa Hamisa. Hongereni sana kwa kufanikisha shughuli!
Hawakujivunga
Ilipofika muda wakupata chakula, Bi Hamisa alimtafuta wa ubani na kwenda kuchukua chakula. Kweli walikula kwa raha zao kile walichopenda hawakujivunga.
Monday, January 14, 2013
Mzee Kasiba na Wakeze
Kama kuna mtu aliyekuwa na furaha siku ya tarehe 11/1/2013 pale Deluxe -Sinza kijiweni. Basi ni Mzee Kasiba siku alipomuaga rasmi binti yake Hamisa Kasiba kuanza maisha mapya ya ndoa.
Siku ya kuagwa Hamisa Kasiba
Tarehe 11/1/2013 itakuwa ni moja ya kukumbukwa na Bi.Hamisa Kasiba mtoto kutoka Kigoma alipofanyiwa sherehe fupi ya kumwaga na familia yake tayari kuanza maisha mapya ya ndoa. Sherehe zilifanyika katika ukumbi maarufu wa Deluxe - Sinza Kijiweni Jijini Dar. Shughuli ilifana sana. Kutoka kulia Bi. Hamisa akiwa na Matron wake wametulia tuli.
Migomba imeleta mifugo
Kilimo cha Migomba kimeongeza miradi mingine katika nyumba ya Bi. Elizabeth Norbert na mumewe kutoka kijiji cha Endanoga wilayani Babati Mkoani Manyara. Sasa wana mradi wa ng'ombe wa maziwa aina ya Fresian pamoja na mbuzi wa maziwa (Picha zote na Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)
Mtaalamu shambani kwa mkulima
Afisa Kiungo wa Kanda (ZIELO) ya Kaskazini Bw. Jeremiah Sembosi hufanya kazi shambani na wakulima. Yeye ni kiungo kati ya wakulima watafiti na wagani. Huelezwa matatizo ya wakulima na kuyaweka katika lugha inayoeleweka ili watafiti wayapatie ufumbuzi. Hutambua teknolojia inayotakiwa na wakulima isambazwe na wagani.Hiyo ndiyo kazi ya Afisa Kiungo wa Kanda pamoja na Timu yake. Pichani anaonekena mkungu wa ndizi aina ya Williams na baadaye anaongea na mkulima Elizabeth akiwa na mumewe wakazi wa kitongoji cha Ngarenaro A, kijiji cha Endanoga, kata ya Gallapo wilayani Babati mkoani Manyara wakieleza mafanikio waliyoyapata kutokana na kilimo cha migomba ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba ya kisasa, kusomesha watoto wao na kuongeza miradi mingine ya ng'ombe wa maziwa na mbuzi wa maziwa
Ndizi za chakula na biashara
Umaarufu wa zao la ndizi unazidi kuenea kwa kasi zaidi kutokana na juhudi za watafiti kuingiza aina mpya za migomba kutoka Jamaica aina hizo ni ndizi ziitwazo grandnaine, williams na cavindish ambazo zimeibuka kupendwa sana na wakulima pamoja na walaji kwa sifa zake za kuzaa kwa muda mfupi, umbile zuri, utamu kwa chakula, utamu kama tunda,kuhifadhika kwa muda mrefu bila kuharibika na faida inayopatikana kwa biashara ya zao hilo. Mkungu mmoja unaweza kuwa na chani za ndizi hadi kufikia hadi 20!Hapa nchini ndizo hizo zimeenea katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Pwani, Dar Es Salaam, Lindi, Unguja, Pemba Ruvuma na Mtwara. Mjini Arusha kwa sasa mkungu kama huo ulipo pichani huuzwa kwa shilingi 30,000/= lakini shambani kwa mkulima huuzwa kati ya shilingi 15,000/= hadi 20,000/= wilayani Babati.(Picha imetumwa na Livingstone Mwedipando - ARI-Selian, Arusha)Picha inaonyesha mkungu awa ndizi aina ya Williams
Friday, January 11, 2013
Zahanati ya mimea bila jengo
"Niliposikia zahanati ya mimea niliwaza na kufikiri kuwa inahitaji mambo mengi sana na makubwa kumbe kinachohitajika ni daktari wa mimea na vifaa vyake,mwavuli, meza ndogo,na viti." Anabainisha Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha aliyetuma picha hii. Chini ya mwavuli huu, wakulima huleta sampuli za mimea yenye matatizo aidha magonjwa , wadudu na hata dalili za upungufu wa virutubisho. Daktari wa mimea hutoa huduma za kutambua na kushauri. Kwa njia hii daktari mmoja anao uwezo wa kuhudmia wakulima wengi kwa siku kulingana na mahitaji. Picha hii inaonyesha zahanati ya mimea iliyopo kwenye soko la Sadala wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
Thursday, January 10, 2013
Ndani ya Sebule ya mfugaji wa Kimasai
Hivi ndivyo ilivyo sebule ya mfugaji Kimani Marende Ipanga wa kijiji cha Alkatan wilayani Monduli mkoani Arusha alipowakaribisha wajumbe kutoka sekretarieti ya huduma za uchumi na uzalishaji mkoa wa Arusha wakiburudika kwa kuangalia program ya TV pamoja na familia ya Kimani.
Bidhaa zitokanazo na ngozi
Wasindikaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi mkoani Arusha wameanza kutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na ngozi bora zinazouzwa na wafugaji. Pichani bidhaa za ngozi kama vile malapa, mikoba na sofa sets katika duka moja jijini Arusha (Picha na Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)
Subscribe to:
Posts (Atom)