Thursday, February 14, 2013
Msongamano wa magari Dar
Jijini Dar msongamano wa magari ni mkubwa na ni kero. Hii inasababishwa na mambo mengi moja ni ujenzi wa barabara unaofanyika hasa barabara ya mabasi yaendayo kwa kasi!
Kanisa la Magomeni -Sura Mpya
Ilipo Wizara ya Maendelo ya Mifugo na Uvuvi
Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania
Ujuzi popote
Wednesday, February 13, 2013
Uchaguzi wa Kamati Kuu ya CCM
Huenda akawa Baba Mtakatifu
Tuesday, February 12, 2013
Vyoo vya Highway hotel Korogwe
Hili ni jengo la vyoo vya Highway hotel Korogwe. Vyoo hivi ni visafi sana na huduma ya maji hupatikana wakati wowote inapotakiwa na wasafiri. Ni moja ya hotel zinazotoa huduma bora za vyoo kwa wasafiri hapa nchini.
Hawa ni ndugu
Ali Mhanndo na Abdallah Mhando ni ndugu wanaoishi Arusha lakini ni Wazaramo. Ndugu hawa wamejaliwa kipaji cha kunyoa (Barbers) kwa sasa Bw. Abdallah anafanya kazi katika Barber shop moja ijulikanayo kwa jina la Big L jijini Arusha karibu kabisa na Hospitali ya KKT pale Selian.
Papa Benedict XVI ajiuzulu
Tarehe 11 Februari, 2013, Pope Benedict XVI kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kuanzia tarehe 28/02/2013.
(Picha kwa hisani ya Reuters)
(Picha kwa hisani ya Reuters)
Monday, February 11, 2013
Nje ya uwanja wa TAIFA-Dar Es Salaam
Uwanja wetu mzuri wa Taifa umeanza kutuletea mafanikio, ndani ya uwanja huo ulipo kwenye Manispaa ya Temeke Jijini Dar, Zambia na Cameroon zimechinjwa!
Nigeria Bingwa 2013
Bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ni Nigeria. Imetwaa ubingwa baada ya kuilaza Burkinafaso bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Sunday Mba katika kipindi cha Kwanza. Kocha mzawa Stephen Keshi aliyewahi kuichezea Super Eagles mwaka 1994 na kutwaa ubingwa wa Afrika ndiye aliyeiongoza Nigeria katika michuano hiyo.
Wakulima wafuatwe shambani
Bi. Mary Ndomba (kulia) ni mtafiti wa kituo cha Utafiti wa Kilimo Tumbi, Tabora. Wakati wa mafunzo yake ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Ndomba alifanya utafiti shambani mwa wakulima.
Vyama vya Siasa vyenye sauti Tanzania
CCM na CHADEMA ni vyama vyenye sauti kubwa na mvuto nchini Tanzania.Lolote au chochote wakifanyacho hupewa nafasi kubwa na vyombo vya habari. Jana CHADEMA walikuwa jijini Dar pale TEMEKE mwisho wakati CCM wao wako DODOMA ni katika harakati za kuchukua DOLA!
Thursday, February 7, 2013
Tutumie makazi yetu kuotesha mboga
Tukitumia makazi yetu vizuri tunaweza kuotesha mboga mboga kwa ajili ya chakula na kuongeza kipato pia ni njia nzuri ya kuwafanya watoto wetu wapende kazi hasa za kilimo.
Aliyeiua Cameroon
Huyu ndiye Mbwana Samata (aliyemiliki mpira) aliyeiua Cameroon jana kwenye uwanja wa Taifa. Siku zote ninasema hakuna kisichowezekana na si kweli kuwa nchi nyingine za Kiafrika hata dunia zinatupita sana kiuchezaji. Tatizo tulikuwa hatujajipanga, hatujitambui na hatujiamini. Sasa tumeanza kujipanga, tunajitambua,tunajiamini. Na ndiyo maana katika kipindi kifupi tumeweza kuzifunga Zambia na Cameroon zinazosemekana kuwa ni vigogo wa soka barani Afrika. Ndiyo, tuanze sasa kuvaa sare za akina Mbwana Samata, Frank Dumayo, Juma Kaseja na wengine. T
uwatangaze wachezaji wetu na kutangaza soka la Tanzania.
uwatangaze wachezaji wetu na kutangaza soka la Tanzania.
Adha ya kuendesha gari jijini Dar
Hakuna kinachokera jijini Dar kama kuendesha gari kwenye msururu mrefu wa magari. Inachosha, inasababisha mafuta kutumika kwa wingi, inasababishwa kuchelewa sehemu uliyokusudia kwenda, wakati mwingine wezi hupata fursa ya kuiba ndani ya magari endapo ukijisahau.
Limetoka bandarini
Malori haya yametoka bandarini yakiwa yamebeba shehena ya bidhaa zinazosafirishwa kwenda nchi za nje. Bandari yetu ikitumika vizuri na kufanya kazi kwa tija itaongeza pato la Taifa na kuinua uchumi wa nchi.
Kuna mategemeo ya kula nazi
Iko siku nitakula nazi kutoka mnazi huu. Hivi sasa bei ya nazi jijini Dar haikamatiki, ni kati ya Tshs 600/= hadi Tshs 1000/= kwa nazi moja. Wali na maharagwe yaliyoungwa kwa nazi ni mtamu sana hasa kipolo chake ambacho ndugu zangu Waluguru wanakiita 'bandula!'
Hospitali ya Mbagala Rangi3
Hospitali hii ya kisasa imezunduliwa rasmi mwaka jana baada ya kuboreshwa kwa msaada Kutoka Serikali ya Korea Kusini. Hospitali hii iko kando ya barabara ya Kilwa maeneo ya Zakhem.
Nimejaribu kupanda mboga za maboga
Hapa Kisemvule nimejaribu kupanda mboga za maboga ingawa si eneo kubwa kwa sababu mimi ni mpenzi sana wa mboga ya maboga iliyochangwa na bamia.Waswahili wanasema raha jipe mwenyewe!
Mboga kutoka bonde la Chang'ombe
Kwa miaka mingi bonde la Chang'ombe limekuwa likistawisha aina mbalimbali za mboga zikiwemo bamia, mboga za mabgoa, na mchicha. Wakazi wengi wa Jiji la Dar Es Salaam hutegemea bonde la Chang'ombe kwa mboga. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikiandaa Mpango Mkakati wa Kilimo mzuri wa jinsi ya kulitumia bonde hilo kwa shughuli za bustani mabadiliko makubwa ya uzalishaji wa mboga zilizo na ubora na uwingi wa kutosha kwa matumizi ya wakazi wa jiji la Dar utapatikana. Hii pia itawaongezea kipato wazalishaji wa mazao ya bustani katika bonde hilo.
Mbagala R3
Acha kabisa. Mbagala ya sasa siyo ile ya zamani. Ghorofa zimeanza kuchipuka na barabara iboreshwa, foleni za magari hutokea kwa nadra sana.Tunaweza kusema kuwa Mbagala Rangi 3 ni kichocheo cha maendeleo ya mikoa ya kusini.
Hapa ndipo 'Kempski'
Siku za kazi wakati wa mchana ukinipigia na nikakujibu kuwa niko 'Kempsiki' basi ni hapa.Ukiwa 'Kempsiki' unapata vyakula vya leoleo. Kuanzia samaki aina ya changu,kibua pamoja na mboga za maboga, tembele, kisamvu, bamia na maharage, nyama za kukaanga, wali kwa nazi na ugali wa kuviringwa. Huduma zake ni poa pia hapa hakuna daraja! Bei zake pia ni kivutio cha wateja. 'Kempsiki' inapatikana karibu kabisa na yalipo Makao Makuu ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wailaya ya Temeke, maeneo ya Veterinary ni jirani pia na ofisi za usafirishaji ya Kampuni ya DANDHO.
Bahari yetu ya Hindi
Tanzania tumebahatika kuwa na bahari ya Hindi (Indian Ocean). Bahari hii hutumika kusafirisha abiria pia bidhaa ndani na nje ya nchi.Bahari ni makazi ya viumbe wa majini kama vile samaki ambao hutupatia kitoweo pamoja na kuingiza kipato. Bahari ni kivutio cha watalii. Maji ya bahari hutumika pia kutengeneza chumvi. Faida tuzipatazo kutokana na bahari ni nyingi hizi ni baadhi tu.
Wednesday, February 6, 2013
Bakhresa anavyotangaza bidhaa zake
Hivi ndivyo Mohamed Bakhresa anavyotangaza bidhaa zake. Bango hili linaonekana pale TAZARA - Traffic lights
Nyumba za TAZARA
Hivi ndivyo Banzi wa Moro alivyozikuta nyumba za TAZARA pale Temeke Veterinary jijini Dar. Zimechoka ile mbaya. Hakuna kupaka rangi wala nini. Lakini enzi zake walipokuwa wanakaa Wachina zilikuwa babukubwa. Nasikia nyingi kama si zote zimeshauzwa kwa wafanyakazi wa TAZARA.
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Wizara ya Kilimo inapatikana jijini Dar, wilaya ya Temeke kandokando ya Barabara ya Mandela karibu kabisa na Stesheni ya Tazara.
Friday, February 1, 2013
Hatufuatilii mijadala
Pamoja na kuwa na luninga zenye ving'amuzi majumbani kwetu lakini nibaini kuwa tulio wengi hatufuatilii mijadala inayoendeshwa luningani.
Tunachambua mbaazi
Mbaazi mbichi ni mboga nzuri sana hasa ikipikwa na nazi na kisha ukala na wali ni utamu mpaka kisogoni. Lakini mbaazi zikikumaa halafu ukala na ugali wa mtama hapo shughuli ni pevu na kwakweli chakula hiki mimi sikipendi!
Dar kweupe
Kuna mitaa katika jiji la Dar Es Salaam, Tanzania haina msongamano wa watu hasa siku za mapumziko kama Banzi alivyoukuta mtaa huu maeneo ya posta tofauti kabisa na hali ilivyo kwenye mtaa wa Kongo pale Kariakoo.
Alipokuwa 'Form One'
Mwaka huu 2013 Catherine Banzi ameingia 'Form II' Pichani Cathy alipokuwa 'Form I' Kweli miaka inakwenda. Mwezi Januari umekuwa mchungu kwa wazazi wengi kwa ajili ya kulipia gharama za watoto wao wanaosoma. Hata hivyo tusisikitike sana kwani ni muhimu kuhakikisha kuwa watoto mtoto wako anapata elimu nzuri itakayomsaidia kumudu maisha yake.
Gari yahitaji kukaguliwa
Baadhi yetu wanamiliki na kuendesha magari lakini ni wangapi wanapata muda wa kukagua magari yao ili kuhakikisha kuwa ni salama? Mara nyingi ajali nyingi hutokea kwa kuwa magari ya hitilafu fulani. Ni vyema kukagua, tairi,mafuta, oil, maji, na betri kabla ya kuanza kuendesha gari.
Subscribe to:
Posts (Atom)