Wednesday, June 12, 2013

Bibi Josephine Mutahangarwa asalimiana na Kardinali Pengo

Bibi Josephine Mutahangarwa a.k.a. Bibi Jeshi (aliyeshikiliwa) wa Vikindu akisalimina na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo. Bibi Josephine ndiye aliyetoa ardhi ya kujenga Kanisa la Parokia ya Vikindu. Mmoja wa wageni waalikuwa katika sherehe ya ufunguzi wa Seminari ya Vicentian, Vikindu

Waliosimamia ujenzi wa Parokia ya Vikindu

Kutoka kushoto Mama Warioba, Mama Janet Kahama, Sir George Kahama na Brigadier Mbena.Wageni waalikwa kwenye ufunguzi wa Seminari ya Vikindu 9/6/2013.

Zawadi ya Waseminari

Waseminari wa kwanza wa Vikindu wakiwachezea ngoma ya Kiluya wageni waalikwa.

Igizo kutoka nyumba ya malezi masista wa Carmel Vikindu

Dada wadogo walioko kwenye nyumba ya malezi, shirika la Masista wa Carmel walicheza igizo wakati wa ufunguzi wa seminari ya Vikindu linaloelezea uinjilishaji barani Afrika.

Tenzi kwa Waseminari

Masista wa Shirika la Mt.Visenti wa Paulo waliwaimbia utenzi waseminari wa Kwanza wa Seminari ya Vikindu.

Fr.Jinu Rector wa Kwanza Vicentian Seminary Vikindu

Rector wa Kwanza wa Seminari ya Vikindu, Fr.Jinu akitoa utambulisho kwa wageni.

Seminari ya Vikindu yafunguliwa rasmi

Vicentian Seminary, Vikindu ilifunguliwa rasmi na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo tarehe 9/6/2013. Seminari hii ni ya Kwanza hapa Afrika kwa shirika la Visenti na limeanza na waseminari 7 (5 Kenya, 2 Uganda).Wosia wa Kardinali Pengo kwa Seminari hiyo ni kuwalea waseminari kwa misingi ya kanisa bila kuleta aibu kwa kanisa kama ambavyo imeshawahi kutokea katika seminari nyingine.Wasiofaa waondoke mapema.

Pokea zawadi

Fr.Mathayo, Paroko wa Parokia ya Mt.Visent wa Paulo, Vikindu akimkabidhi Muadhama Polycarp Kardinali Pengo zawadi ya Parokia.

Kardinali Polycarp Pengo azungumzia imani ya Kanisa Katoliki

Kanisa inaamini juu ya Utatu Mtakatifu:- Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ndiyo muhimili wa Kanisa. Muadhama Kardinal Polycarp Pengo aliyasema hayo kwenye ibada ya misa takatifu ya kutoa sakramenti ya Kipaimara kwenye Parokia ya Mt.Visent wa Paulo-Vikindu tarehe 9/6/2013.

Muadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia kanisani Vikindu

Pengo na askari wapya wa Parokia ya Mt. Visent wa Paulo-Vikindu

Muadhama Kardinali Polycarp Pengo (Aliyeshika fimbo)-Askofu Mkuu Kanisa Katoloki Jimbo Kuu la Dar Es Salaam katika picha ya pamoja na waliopata sakramenti ya kipaimara Parokia ya Vikindu tarehe 9/6/2013

Friday, June 7, 2013

Waliopata kuingoza Kilimo-Uyole

Kuanzia Uyole Agricultural Centre (UAC)hadi sasa mfumo wa Kanda Uyole imeongozwa na viongozi mbalimbali.Kiongozi wa sasa ni Mkurugenzi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dr.Zacharia Malley. Bango linaonyesha viongozi waliopata kuiongoza Kilimo-Uyole.

Ukarabati wa barabara Iringa - Mbeya kiwango

Ukarabati wa barabara kutoka Iringa kwenda Mbeya unafanyika kwa kiwango cha hali ya juu kama unavyoona moja ya culvert lililojengwa.

Mahindi ya kuchoma

Ukarabati wa barabara ya kwenda Mbeya kutoka Iringa umewaongezea kipato kwa baadhi ya wakazi wanaoishi kando ya barabara hiyo kwa kuuza bidhaa mbalimbali yakiwemo mahindi ya kuchoma.

STJ 933 taabani

Gari tulilosafiri-nalo kwenda Mbeya -STJ 933 lilipata hitilafu ya 'clutch' na kukosa nguvu.Tulipofika Ilula, Iringa ilibidi kutengenezwa.

Ajali Kitonga mlimani

Wakati tunaelekea Mbeya siku ya Jumanne tarehe 5/6/2013 mlimani Kitonga tuliona gari lililopata ajali.

Wachagga hawasahau utamaduni wao

Wanapoitwa kucheza ngoma hii ya kushikana mikono haikosekani ( utani- wanaogopa kusachiana!)

Shughuli ni ndafu!

Harusi ya Kichagga haikosi ndafu. Pichani Bw. harusi Adam Mandara akikata ndafu!

Professor Mainen Moshi

Professor Mainen Moshi Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe ya Mapokezi ya Maharusi Bw. na Bibi Adam Mandara akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Twiga huko Mbezi Beach tarehe 1/6/2013.

Hivi ndivyo tulivyojifunza kusoma ramani

Nilipokuwa shule ya msingi nilipenda somo la jiografia kwa sababu ya kuchora ramani. Hii imeniwezesha pia kuchukua combination ya CBG(Chemistry, Biology and Geography) nikiwa A level pale Tosamaganga.Ramani hii ya Africa imechorwa kwenye moja ya jengo la Shule ya Msingi ya Carmel, Vikindu. Hakika hapa atapatikana CBG mwingine.

Baadhi ya shughuli za Harris Kapiga

Harris Kapiga akiwa kazini.

MC- Harris Kapiga

Ukimtaka MC- Harris Kapiga- uwezo wake ni huu.Huyu pia ni Mtangazaji wa Clouds Radio.

Mambo yalivyokuwa kwenye harusi ya Adam Mandara

Bw na Bibi Adam Mandara

Adam & Judith Ukumbini

Maharusi Bw Adam Mandara na mkewe Bi Judith wakiingia ukumbini huko Mbezi - Social Centre siku ya tarehe 1/6/2013.

Kamati Ukumbini

Professor M.Moshi (Mwenyekiti wa Kamati)akiongoza Kamati ya Maandalizi ya mapokezi ya maharusi Bw na Bibi Adam Mandara yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Social Centre - Mbezi Twiga Hall tarehe 1/6/2013.

Hii ndiyo CARMEL CONVENT PRE AND PRIMARY SCHOOL - VIKINDU,MKURANGA

Shule ya Awali na Msingi (English Medium) inayomilikiwa na Kanisa Katoliki na kusimamiwa na Masista wa Shirika la Carmel limeanza imeanza kupata sifa kwa kiwango cha elimu inayotoa,nidhamu,vifaa pamoja na vyombo vya usafiri. Kwa mara ya kwanza mwaka huu wanatarajia kutoa wahitimu wa darasa la saba.

Vifaa vya michezo mashuleni

Vifaa vya michezo mashuleni huvutia wanafunzi na wazazi pia. Shule ya awali na Msingi ya Carmel iliyopo Vikindu ina vifaa hivyo na viwanja vya michezo.

Shule ngapi za msingi zenye 'Vision' na 'Mission'?

Ni shule chache zenye Vision na Mission. Carmel Pre and Primary School inayo. Shule nyingine zinaweza kujifunza kutoka hapa.

Welcome to Carmel Pre and Primary School Vikindu

Unapoingia ndani ya shule ya awali na Msingi (English medium) ya Carmel iliyopo Vikindu unakaribishwa hivi.