Vyakula ni vingi sana mkoani Ruvuma. Karanga,maharagwe vinapatikana kwa wingi katika soko la Songea.
(Picha kwa hisani ya Dkt. Louis Kasuga wa ARI-Naliendele, Mtwara)
Monday, July 29, 2013
Matunda na viungo bila madawa
Mapapai, vitunguu na nyanya zikiwa sokoni Songea. Asilimia ya mazao haya hayajazalishwa kwa kutmia mbolea wala madawa.
Mama mfanyabiashara sokoni Songea
Akina mama wa Tanzania wamechangamka katika ujasiriamali. Mtafiti Dr. Louis Kasuga kutoka kituo cha Utafiti Naliendele, Mtwara alinasa picha ya mwanamama huyu akiwa katika soko la mjini Songea akifanya biashara ya mazao mbalimbali.
Dagaa sokoni Songea
Dagaa sokoni Songea.Nafikiri hawa ni dagaa kutoka ziwa Nyasa (Picha kwa hisani ya Dr. Louis Kasuga wa ARI-Naliendele)
Thursday, July 25, 2013
Baada ya msiba maisha yanaendelea
Baada ya msiba wadogo zangu walinipitisha katika eneo la mashamba ya baba zetu na kunionyesha mipaka. Inabidi tutunze raslimali zetu kwanza kwa kuzitambua na pili kuweka mikakati ya kuzitunza na kuziendeleza.Hii ni sehemu ya mashamba yetu yaliyopo katika kijiji cha Nige, Kariakoo-Matombo, Morogoro.
Usafi wa mazingira ndani na nje baada ya mazishi mila ya Kiluguru
Usafi wa ndani na nje ya mahali pa msiba unafanywa baada ya kuzika. Hii ni moja ya mila na desturi za Waluguru ambayo wengi hatuifahamu na pia hatuizingatii. Tulipomzika mama mkubwa Fortunata pale kijijini kwetu Nige, Kariakoo, Matombo-Morogoro nilishuhudia kinadada wakifanya shughuli hii ya usafi. Mgawawanyo wa kazi unazingatiwa hata kwenye misiba. Baba mdogo alionekana kuchoma kuku (Gender issue!)
Tukishazika siku inayofuata tuna choma kuku na kula
Waluguru siku moja baada ya kuzika kuna kitu kinachoitwa moto ndugu. Moja ya vitu vinavyofanyika asubuhi ni kubanika kuku kwenye moto na kisha wanandugu kugawa nyama kidogo kidogo na kuzila bila kutafuna mfupa.Tunaamini kuwa kwa kufanya hivyo tunafukuza kifo kwenye familia.
KARIBU MKOA WA MOROGORO
Mkoa wenye watu wapole, wanawake na wanaume wazuri,wenye heshima, wavumilivu na wachapakazi,wapenda michezo hasa mpira wa miguu pamoja na muziki. Moro kwenye mabonde na milima,mbuga, na maji yanayotiririka mwaka mzima,Bwawa la Mindu, Chuo Kikuu cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Waislamu, Chuo Kikuu Mzumbe, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Cholima Dakawa,Kituo cha Utafiti Kilimo Ilonga, Kituo cha Utafiti wa Kilimo KATRIN Ifakara, Taasisi ya Utafiti wa Malaria-Ifakara, Bwawa la kuzalisha umeme-Kidatu,Chuo cha wakulima Mkindo,Chuo cha Ualimu Ilonga, Chuo cha Ualimu Mhonda, Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI), TV ABOOD, ABOOD BUS SERVICED, HOOD BUS SERVICES.
Vyakula vingi kama mpunga,mahindi,mtama,muhogo,maboga,viazi vikuu,magimbi. Mboga za mwidu,derega,mchunga,bwasali, bamia,nyanya chungu,tunguja,nyanya maji,mwage,matango
Matunda ya machungwa,ndizi,maembe,pasion,mafenesi,mashelisheli,tikitimaji. MORO SAFI SANAAA! KARIBU
Tuesday, July 23, 2013
Nilikabidhi msiba kwa baba zangu
Mazishi ya mama mkubwa Fortunata Epimark
Jumatatu ya tarehe 17/6/2013 ni siku ya msiba kwa familia ya akina Banzi wakati mama mkubwa Fortunata Epimark mke wa baba yetu mkubwa Mwl. Ephrem Ephrem Mbiki alipofariki jijini Dar na kuzikwa kijijini Matombo, Morogoro. Pichani jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa kwenye kanisa Katoliki, Parokia ya Mavurunza, Kimara Dar Es Salaam kwa Ibada ya kumuombea kabla ya kusafirisha mwili kwenda kijijini.
Nakagua bustani ya vijana Kisemvule
Mwanzo mgumu. Miche ya matikitimaji imeanza kuota kwenye bustani ya vijana iliyopo kijijini Kisemvule.Nitawasaidia vijana hawa ili wasonge mbele na kutimiza ndoto zao. Vijana wengine tuige mfano wa vijana hawa watatu.
Kisima kitakachotumika kumwagilia bustani ya mbogamboga Kisemvule
Maji mengi yaliyopo kijijini Kisemvule yamewahamasisha vijana kuja na wazo la kulima bustani ya mbogamboga.Hawa watafanikiwa.
Wameamua kulima bustani ya mboga kijijini Kisemvule
Kisima cha 'mdundiko' kijijini Kisemvule
Kisima hiki kiko katika kijiji cha Kisemvule wilayani Mkuranga. Kimetengenezwa na mwanakijiji anayejulikana kwa jina la Kite.Maji ya kisima hiki hayana chumvi, ni baridi hakika yana ladha nzuri.Hivi majuzi nilipata kumtembelea Bw. Kite na kujaribu kusukuma maji kutoka kisimani.
Kiwanda cha Cement ya Rhino-Kisemvule, Mkuranga
Hiki ndicho kiwanda cha cement ya Rhino kilichopo kwenye kijiji cha Kisemvule, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.
Mapadri wapya Kanisa Katoliki nchini Tanzania
Zamani ilikuwa si rahisi kuwapata mapadre kama ilivyokuwa vigumu kuwapata wasomi ngazi ya PhD, Madaktari wa binadamu pamoja na wahandisi. Hivi sasa jimbo linaweza kutoa mapadri saba kwa wakati mmoja kama ilivyotokea hivi karibuni kwa jimbo kuu la Dar Es Salaam. (Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi)
Thursday, July 18, 2013
Mwali amepanda 'bodaboda'
Hawa ndio wali wa kiume wa Kizaramo
Zamani wali wa kiume wa Kizaramo walikuwa wakivalishwa kanzu wakati wanapochezwa (tafrija). Wali hawa wametia fora angalia walivyopendeza wakiwa ndani ya suti kali!
Wali wa kike wa Kizaramo
Kama kuna kabila linaloendeleza utamaduni wao basi Wazaramo ni mojawapo hasa inapokuwa masuala ya unyago kwa wasichana waliovunja ungo. Mara wanapopoata mafunzo wanayostahili hufanyiwa tafrija na hapa motto anazawadiwa zawadi mbalimbali na hasa nguo. Pichani wali waliochezwa kijijini Kisemvule hivi karibuni.
Tathmini ya pamoja ya Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo
Wakulima, wagani na watafiti ni muhimu wakafanya kazi kwa pamoja kuanzia kupanga, kutekeleza na kutathmini shughuli. Pichani wataalamu wa kilimo wakiwa ndani ya ofisi ya Afisa kilimo wa Wilaya ya Kilosa mapema mwezi Julai, 2013.
Nyumba ya Kisasa ya wageni mjini Kilosa
Kilosa sasa kumekucha hakuna shida ya nyumba za wageni kama ilivyokuwepo miaka 10 iliyopita.Nyumba nyingi mpya na za kisasa zimejengwa mjini Kilosa.
Wanauza pepeta kwenye kivuko cha mto Kilombero
Utafiti wa mpunga klituoni KATRIN-Ifakara
Wataalamu wa kilimo wakipata maalezo ya utafiti wa mpunga kutoka kwa mtafiti wa KATRIN-Ifakara walipotembelea shamba la majaribio la kituo lililopo katika mto Lumemo-Ifakara mapema mwezi Julai 2013.
Wednesday, July 17, 2013
Ufunguzi wa Kituo cha Utafiti KATRIN -Ifakara
Vifaa vya umwagiliaji katika shamba la utafiti Ilonga
Mhasibu Mwandamizi Christopher Gibbson wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika akishangaa mabomba ya umwagiliaji katika shamba la utafiti Ilonga.
Shambani Lumemo - Ifakara
Toyota-Landcruiser, gari hili linafaa sana kwa shughuli za shambani kama vile za utafiti kilimo. Bw . Omari Kizito na Shuhu Jr wamekuwa wakiendesha gari la aina hii wakiambatana na watafiti vijijini. Hapa wapo kwenye shamba la Utafiti KATRIN katika mto Lumemo-Ifakara.
Utafiti wa zao la mtama na alizeti kituo cha Utafiti Ilonga
Utafiti wa alizeti na mtama umeandelea kufanywa kwa miaka mingi katika kituo cha utafiti Ilonga. Matokeo mazuri yamepatikana kama vile mbegu bora zinazozaa kwa wingi zinazovumilia ukame na magonjwa.
Ushindi ARI-Ilonga
Vikombe vilivyonyakuliwa na kituo cha Utafiti Ilonga ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki.
Friday, July 12, 2013
Utafiti wa mtama kituoni Ilonga
Maelezo kutoka kwa watafiti wa mpunga Cholima-Dakawa
Teknolojia za kilimo cha Kichina kituo cha Dakawa
Mtaalamu wa Kichina wa kituo cha teknolojia za kilimo za Kichina akiwaonyesha wajumbe wa timu A ya kupelemba na kutathmini kanda ya Mashariki mwaka 2013 plot ya maonyesho ya vitunguu.
Pepeta za Ifakara!
Pepeta nazo ni tamu - kwa kiingereza zingeweza kuitwa 'Rice flakes' ni sawa kabisa na corn 'flakes'Nilipofika kwenye kivuko cha mto Kilombero nilinunua pepeta kiasi cha kilo tatu kwa gharama ya Tshs 4,500/=.
Subscribe to:
Posts (Atom)