Monday, September 30, 2013
Vipimo ni vya aina nyingi u sahihi je?
Kila aina ya kipimo kina matumizi yake. Lakini nina mashaka kama wadau wanafahamu jinsi vinavyotumika.Anayefahamu ni mpimaji. Kwa mfano hata mimi wakati mwingine huwa nachanganywa na hicho kipimo chenye rangi nyekundu. Uzito (jiwe) scale (ruler) vyote hutumika kwa pamoja. Kwa kweli hapa ni rahisi kuibiwa hasa kwa wakulima wetu. Ni vyema wadau wakaelimishwa.
T-shirts kutoka Tanzania
T-shirt kutoka Tanzania, ni nzuri na ujumbe unaeleweka.Hivi ni kwanini Watanzania hatupendi chetu. Penda chako hata kama ni kibaya.
Mkaa kutoka maganda ya Karanga
Je tunazo karanga za kutosha za kukidhi mahitaji ya mkaa kutoka maganda ya karanga? Watafiti nipeni jibu. Pichani mkaa wa karanga ukiwa juu ya meza kwenye maonyesho ya wakulima kitaifa yaliyofanyika Dodoma viwanja vya Nzuguni 2013.
Phillips ya kulia 'feki'
Mtaalamu wa kutambua bidhaa feki sokoni hasa za viwandani amebainisha kuwa hiyo bulb ya energy server iliyoko kulia ni feki lakini zote ni Phillips
Ufuta aina ya Lindi 02 hutoa magunia 15 ya kilo 100 kwa hekta
Siajabu kwa mkulima kuvuna magunia 15 ya ufuta yenye kilo 100 kila gunia kwa hekta. Hii inawezekana kwa kulima ufuta aina ya Lindi 02 ambayo hukomaa kati ya siku 100-110 tangu iote.Aina hii ya ufuta ina asilimia 55 ya mafuta. Hii ni habari njema kutoka kwa watafiti wa Kilimo kutoka kituo cha Utafiti Naliendele,Mtwara.
Machungwa matamu
Tanzania imebahatika kuwa na hali ya hewa inayoweza kustawisha mazao mbalimbali yakiwemo machungwa. Pichani vijana wa kisemvule wakijishughulisha na biashara ya machungwa kwenye kituo cha mabus hapo kijijini.
Maji bwelele Kisemvule
Wakati wengine wana shida kubwa ya maji, wananchi wa kijiji cha Kisemvule wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani nchini Tanzania maji si tatizo ukichimba kidogo unapata maji ya kutosha tena siyo ya chumvi.Hii pengine ndiyo sababu ya wawekezaji wa viwanda kupenda eneo hili na hivi sasa kuna viwanda vingi kikiwemo cha sementi ambacho kinatumia maji mengi.
Wanawake watafiti wa Kilimo
Ishika Mshaguley na Vidah Mahava ni Watafiti wa Kilimo wanawake kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Hapa wako kwenye kikao kazi cha Kupelemba na Kutathmini shughuli za Utafiti wakiwa kwenye sekretarieti ya Kikao hicho.Kila mmoja wao ana kidadavuzi mpakato!
Fr. Jinu akifanya mawasiliano
Mmoja wa Mapdri wa Parokia ya Vikindu, Fr.Jinu Joseph akifanya mawasiliano kwa kutumia simu yake ya mkononi huku masista wa Carmel wakifuatilia kwa makini matukio ya sherehe ya Mt.Vinsenti wa Paulo iliyofanyika tarehe 29/9/2013 kwenye viwanja vya parokia ya Vikindu.
Mkereketwa wa St.Vincent de Paul Vikindu
Mtoto huyu anapendwa na wazazi wake. Wazazi ni waumini wa Kanisa Katoliki St.Vincent De Paul, Vikindu wamemnunulia T-shirt nzuri ya Mt.Vinsenti wa Paulo.Ona alivyofurahi!
Wanakwaya wa Mt.Veronica kigango cha Kariakoo
Hii ndiyo kwaya ya Mt.Veronica kigango cha Kariakoo, Jimbo kuu la Dar Es Salaam waliokuja kuwapa shavu marafiki zao wa Kwaya ya Mt.Vinsenti wa Paulo wakizindua Album yao ya Video "Inanibidi Nikeshe" iliyozinduliwa tarehe 29/09/2013
Je, umeshawahi kumuona Ngongoti?
Kigango cha Malela Parokia ya Vikindu walileta Ngongoti kusherehesha sikukuu ya Somo wa Kanisa Mt.Visenti wa Paulo tarehe 29/9/2013.
Album ya Video-Inanibidi Nikishe yazinduliwa
Jana tarehe 29/9/2013 Kwaya ya Mt.Vinsenti wa Paulo, Vikindu ilizindua album yake ya kwanza ya Video inayojulikana kwa jina la "Inanibidi nikeshe." Uzinduzi ulikuwa wa kufana sana. Pichani mgeni rasmi Bw. Peter Vava akizindua ALBUM hiyo.
Friday, September 27, 2013
Kumwagiana tindakali ni unyama
Hivi Watanzania tumefikia hatua hii ya kinyama? Mtun kama akikukosea, uungwana ni kumuuliza kwanini amekutendea hivyo. Hakuna haja ya kufanyiana visa kama hivi vya kumwagiana tindikali.Pichani Frateri Richard Haki akimsaidia Padri Anselmo Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Zanzibar aliyemwagiwa tindikali hivi karibuni.
Kuku wetu wa asili au wa kienyeji ni watamu!
Kuku wa kienyeji wakitunzwa vizuri wanakuwa katika hali hii na utashangaa kuambiwa kuwa ni kuku wa kienyeji. Hakika kuku wetu wa kienyeji au wa asili ni watamu.Tufuge kuku kwa bidii angalau kuku wa tano wa asili kwa kila nyumba.
Ndizi zinaweza kumtoa lakini mtaji mdogo
Mwanamama huyu mchuuzi wa ndizi anahitaji mtaji mkubwa zaidi aweze kuuza ndizi zake kwa faida na kumsaidia huyo anayemtegemea aliyelala kifuani kwake. Wanawake wa aina hii wako wengi wanajitegemea. Wamekimbiwa na wanaume waliowazalisha lakini sikumoja watafanikiwa.Kuna haja ya Taifa kuwangalia na kuwawezesha akina mama wa aina hii.
Pombe ya asili
Kuwawezesha wanawake kuongeza thamani ya mazao
Wanawake hawa wamejifunza jinsi ya kupanga nyanya vizuri ili zisihabribuike tayari kwa kusafirishwa. Nyanya hizi haziwezi kuharibika kirahisi hivi kutunza ubora wake kwa muda mrefu. Ni vyema kuwajengea uwezo wanawake katika kuongeza ubora wa mazao ya kilimo.
Hatujafanya vizuri katika Ufugaji wa samaki wa mabwawa
Tanzania hatujafanya vizuri katika ufugaji wa samaki kwa kupitia mabwawa licha ya fursa zilizopo. Kuna kutajirika kwa kufuga samaki pia ni njia rahisi ya kujipatia lishe.
Furaha ya Power Tiller
Kweli ni furaha ya Power Tiller. Hakuna anayependa kulima kwa mkono. Kilimo cha mkono kinachosha,tija ni ndogo na pia hakivutii vijana. Je, powertillers zilizokuwa gumzo mwaka 2010 zinaendeleaje huko vijijini waliko wakulima?
Tuesday, September 24, 2013
Watawa kwenye sherehe ya Mt. Monica
Jumuiya Ndogondogo ni pamoja na watawa. Pichani watawa wa Parokia ya Vikindu wakiwa kwenye sherehe ya Jumuiya ya Mt. Monica
.
.
Fr. Mathayo akiendesha Ibada ya Misa Takatifu
Mashindano ya soka kijijini Kisemvule
Kuna mashindano ya mpira wa soka yanayoendelea kijijini Kisemvule hivi sasa. Mshindi hajapatikana lakini hapa kuna vipaji kwakweli kuna vijana wanaoweza kuuchezea mpira wapendavyo!
Kijana akijaanda kuiba mafuta kutoka kwenye lori la mafuta
Kuna vijana wenye mazoea ya kufuatilia malori yanayosafirisha mafuta kwa lengo la kuyaiba kupitia mifuko ya rambo. Ni hatari kwa uhai wao na pia mafuta wanayoiba mara nyingi ni mabaki ya mafuta kwa hiyo kuna hatari kwa wanaouziwa kutumia mafuta yaliyo chini ya kiwango. Tujihadhari na mafuta ya vidumu.
Friday, September 20, 2013
Niko kwenye banda la Utafiti -Viwanja vya Nzuguni Dodoma
Hapa niko Dodoma kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane Nane Dodoma kwenye banda la Utafiti Mradi wa Kuongeza uzalishaji na Tija katika Kilimo Afrika Mashariki (EAAPP). Mbele yetu ni aina mbalimbali za ngano.
Reaction from Dr. Zacharia Malley
Watafiti wanapokutana kila mtu anajinafasi kutokana na elimu yake, uwezo, ujuzi, maarifa na uzoefu. Mambo yote kwa uwazi kabisa. Hii ndiyo knowledge sharing. Pichani Mkurugenzi wa Utafiti Kilimo, Kanda ya Kati Dr. Zacharia Malley akielezea jambo kwenye kikao kazi cha kutathmini taarifa za 'monitoring na evaluation' kutoka kwenye kanda saba za utafiti nchini kwa mwaka 2013. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Edema mjini Morogoro.
DR.Zacharia Malley - Mkurugenzi wa Kanda Utafiti Kilimo-Nyanda za Juu Kusini, ARI- Uyole |
Mambo ya Edema-Moro
Tuesday, September 17, 2013
NARCO na mikato ya Nyama
Sipendi kula nyama yenye vipande vya magogo. Basi Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) inatumia vifaa vya kisasa kukata nyama.Na kila aina ya nyama ina jina lake. Ukitaka kufahamu nunua nyama kutoka NARCO.
Pendo na Naliendele 92-Mbegu za karanga
Pendo na Naliendele ni aina za karanga.Soma sifa zake ili uweze kulima kilimo cha karanga chenye tija.
Sarah Habib Kondo
Sarah amekuwa Askari kamili baada ya kupata Kipaimara mwishoni mwa mwezi Agosti 2013. Ukisoma St.Mathew wote ni sawa. Angalia vazi la Kipaimara. Simple!
Hongera Sarah kupata sakramenti ya Kipaimara
Ray akimkumbatia nduguye Sarah kwa kupata Sakramenti kwenye Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Shule ya Sekondari St.Mathew iliyopo katika wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.
Nami nilivaa joho la mwanangu
Nakumbuka sikuvaa joho wakati nilipohitimu elimu yangu ya Sekondari. Tarehe 14/09/2013 nilibahatika kuvaa joho la mwanangu Sisty Banzi. Na hapa najipongeza huku mwanangu Maria akiniangalia.
Nampongeza mwanangu Sisty Banzi
Baada ya miaka minne ya masomo ya Elimu ya Sekondari. Nampongeza mwanangu kwa kumaliza elimu yake ya Sekondari.Sasa anasubiri kufanya mtihani mwezi Novemba 2013.
SISTY BANZI-Amehitimu Kidato cha NNE
Tuesday, September 3, 2013
Kitanda 'Six BY six'
Ukiweza kumudu kununua kitanda kikubwa kama hiki Sita kwa sita basi wewe ni mmoja wa wajanja.Ni kitanda kinachotengezwa na vijana wa JKT kitengo cha Chang'ombe. Mbao imara na godoro safi!
Soseji za samaki kutoka Bukoba
Hapa nilipata bahati ya kula soseji za samaki kwenye banda la soseji za samaki. Mama mjasiriamali wa kutoka Bukoba Mary Karega.Alipohojiwa na kituo cha Televeshini cha ITV changamoto anazozipata kwenye biashara yake alisema kikwazo ni ukiritimba wa kupata idhini ya ubora wa bidhaa kutoka Tanzania Bureau of Standards (TBS)
Samani inayotengenezwa na JKT
Ng'ombe kilo 950
Rampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imeweza kufuga ng'ombe mwenye kilo 950. Ng'ombe huyu alikuwa kivutio kwenye maonyesho ya wakulima ya Taifa yaliyofanyika Dodoma mwezi Agosti 2013.
Subscribe to:
Posts (Atom)