Thursday, October 31, 2013
Gari la maharusi
Gari lililowachukua Bw & Bibi Joe Mutahangrwa mara baada ya kufunga ndoa Kanisani Vikindu- Tarehe 26/10/2013.
Kampa amapofurahia utamaduni wa kwao
Ukimuona mtu mzima anaingia ndani ya uwanja basi tambua kwamba imemkuna. Pichani Mkurugenzi wa TANDAN FARMS ya Vikindu-Kisemvule Bw. Kampa ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe ya kuwapongeza Bw & Bi Joe Mutahangarwa baada ya kufunga ndoa yao akicheza ngoma ya asili ya Kihaya.
Bw & Bibi Joe Mutahangarwa wakitoka kanisani
Bw & Bibi Joe Mutahangarwa wakitoka kanisani mara baada ya kufunga ndoa tarehe 26/10/2013 kanisani Vikindu.
Mr & Mrs Joe Mutahangarwa vyeti vya ndoa
Mambo yamekuwa mambo. Bw na Bibi Joe Mutahngarwa wakionyesha vyeti vyao vya ndoa siku ya tarehe 26/10/2013
Wazazi wa Daphrosa
Bw. na Bibi Nangeda wazazi wa Bi Daphrosa wakishudia ndoa ya mtoto wao kanisani Vikindu. Tarehe 26/10/2013.
Sir George Kahama Kanisani
Bibi Josephina Mutahangarwa, Bi. Janet Kahama na Sir Clement George Kahama wakiwa Kanisani Vikindu wakifuatilia Ibada ya ndoa ya Bw. na Bibi Joe Mutahangarwa iliyofanyika tarehe 26/10/2013.
Joe Mutahangarwa akifurahia Ibada
Bw. Joe Mutahangarwa na Mkewe Daphrosa wakiwa na furaha wakati wa Ibada ya ndoa yao Kanisani Vikindu.
Dada Kanisani
Dada zake Joe wakifutialia kwa makini Ibada ya ndoa ya Bw. na Bibi Joe Mutahangarwa iliyofanyika tarehe 26/10/2013 kanisani Vikindu.
Joe naye alimvisha pete mkewe
Bw. Joe Mutahangarwa akimvisha mkewe Daphrosa Nangeda pete ya ndoa alama ya uaminifu na kitu kimoja sasa anakuwa Mrs. Mutahangarwa! Tukio lililofanyika katika Kanisa la Mt. Vinsenti wa Paulo-Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Tarehe 26/10/2013
Kwaya ya Mt. Vinsenti wa Paulo ikitumbuiza kanisani
Kwaya ya Mt. Vinsenti wa Paulo - Parokia ya Vikindu, ilitoa burudani ya kutosha katika ibada takatifu ya misa ya ndoa ya Bw & Bi. Joe Mutahangarwa iliyofungwa tarehe 26/10/2013.
Siku Joe Mutahangarwa alipovishwa pete kanisani
Tarehe 26/10/2013 ndani ya Kanisa la Mt. Vinsenti wa Paulo-Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Bw. Joe Mutahangarwa alivishwa pete ya ndoa na mkewe Daphrosa Nangeda (Pichani) na baadaye tafrija ya nguvu ilifanyika huko Jesus Town Vikindu, TANDAN Restaurant.
Thursday, October 24, 2013
Mwanamke mlemavu mjasiriamali
Wengi wetu tumekamilika kimwili lakini hatupendi kufanya kazi ili tuweze kujipatia mkate wetu wa kila siku.
Lakini mama huyu, licha ya ulemavu wake ameamua kufanya biashara ya ndizi akiwa katika baiskeli yake. Hivi ndivyo inavyotakiwa.
Lakini mama huyu, licha ya ulemavu wake ameamua kufanya biashara ya ndizi akiwa katika baiskeli yake. Hivi ndivyo inavyotakiwa.
Ajali pikipiki yangu
Pikipiki chni ya uvungu wa gari iliyogonga |
Pikipiki baada ya ajali |
Tuesday, October 22, 2013
Gari moshi la Tanzania- Tija Je?
Gari moshi (Train) la Tanzania. Tanzania tumebahatika kuwa na njia mbili za reli. Reli ya kati na Tanzania-Zambia. Lakini nina mashaka kama matumizi ya reli hizi zinaleta tija nchini.
Ukiwa na baskeli hukosi kuziba pancha
Unatakiwa kuwa na viraka vya mpira, gundi, spanners, kopo na maji ili uweze kuziba pancha ya gurudumu la baiskeli!
J.M.Kikwete ndani ya shati la mbio za mwenge 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ndani ya sare ya mbio za Mwenge 2013. Amependeza kwa kuwa imeshonwa vizuri. Kila kitu 'Made in Tanzania.' Watanzania tuna vingi vizuri tupende vya kwetu!
Unga wa Muhogo kwenye viroba
Viazi mviringo chakula wanachopenda watoto
Ukitaka kuwafurahisha watoto basi wananulie chips hata kama ni chips kavu wataweka tomato sauce na siku ikawa nzuri kwao. Tanzania imebahatika kuwa na mazingira yanayoweza kustawisha aina mbalimbali ya mazao. Kwa mfano mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya ni maarufu kwa kilimo cha viazi mviringo (Picha kwa hisani ya IITA).
Mbegu bora za muhogo
Usiokote pingili ovyo za muhogo na kwenda kuzipanda shambani. Unaweza kueneza magonjwa kwenye shamba lako la muhogo, unaweza kupanda aina ya muhogo ambao ni mchungu. Pata mbegu bora kutoka kwenye vituo vya kilimo vinavyotambulika au wazalishaji wa mbegu wanaotambulika. (Picha kwa hisani ya kijarida cha IITA).
Mashine ya kupandia muhogo
Si mahindi tu yanayoweza kupandwa na mashine bali hata muhogo unaweza kutumia mashine kwa kupandia ikiwa una shamba lenye eneo kubwa. Pichani trekta ikivuta mashine ya kupandia muhogo. (Picha kwa hisani ja kijarida cha IITA)
Tengeneza fedha kwa kulima muhogo
Muhogo umekuwa mali. Licha ya kutumiwa kama chakula pia muhogo ni zao la biashara tembelea masoko ya Tandale, Buguruni, Tandika na Mbagala biashara ilivyoshamiri. Muhogo umekuwa mkombozi kwa akina mama katika jiji la Dar Es Salaam. Akina mama hao huuza muhogo mbichi (mtamu) kwa kutafuna, huchemsha na hutengeneza chips za muhogo (chips dume!)
Aflatoxin
What is aflatoxin?
- Aflatoxin is a poison produced by a fungus called Aspegillus flavus
- This fungus reside in soil and dead/decaying matter in the field
- It is very dangerous to humans and animals
- Aflatoxins affects many aother crops such as cassava, yam and rice
How does aflatoxin harm us?
- Aflatoxin causes liver cancer, suppresses the immune system, and retards the growth and development of children
- Aflatoxin-infected crops are forced into low value markets or destroyed
- Aflatoxin damages our health and business opportunities
Can we see aflatoxin?
- Aflatoxin cannot be seen - it is colorless chemical
- Aspergillus flavus is green in colour (right on the maize cob)
- Grains without visible signs of A. flavus may also have high amounts of aflatoxin.
- Laboratory tests determine contamination levels
Monday, October 21, 2013
Familia ya Madenge - Matukio siku ya kupanda msalaba
Tarehe 12/10/2013. Familia ya Mzee Madenge wa Sinza ilihitimisha msiba wa Mama yao mzazi kwa Ibada ya Misa takatifu iliyofanyika katika Parokia ya Sinza baadaye kusimika msalaba huko Sinza Makaburini. Haya ni baadhi tu ya matukio muhimu ya siku hiyo.
shughuli ziliendelea makaburini
Masista wa Parokia ya Sinza walihudhuria ibada ya asubuhi |
Dada Julieth Madenge na ndugu wengine wakiwa kanisani |
Bus maalum liliwaleta wanandugu kanisani |
Bw. Henry Elias Henrish Kobelo akielekeza jambo |
Dada Julietha Madenge akilia mbele ya kaburi la Baba yake Mzee Elias Henrish Madenge |
St. Vincent Dispensary-Vikindu - Masaa 24
Zahanati ya Kanisa Katoliki St. Vincent iliyopo Vikindu mkoa wa Pwani sasa inafanya kazi masaa 24 na inapoke Bima ya NHSF. Zahanati hii iko pembezoni mwa barabara iendayo Mtwara karibu kabisa na Kanisa Katoliki Parokia ya Vikindu- St. Vincent de Paul
Maandalizi ya harusi ya Joe Mutahangarwa
Maandalizi ya harusi ya Bw. Joseph Mutahangarwa a.k.a Joe yanaendelea huku Vikindu- TANDAN FARMS - RESTAURANT. Harusi itafanyika tarehe 19/10/2013 kwenye kanisa la Mt. Vinsenti wa Paulo Vikindu siku ya Jumamosi kuanzia saa 9.00 jioni. Pichani mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bw. Kampa akihesabu fedha za michango iliyotolewa na wadau wa sherehe hiyo huku Bw.harusi mtarajiwa (kulia) akiangalia kwa makini.
Serikali ya Kijiji Kisemvule wafurahi mahafali ya watoto wao
Himili Mbawala - Pongezi kwa kupata CPA
Wajumbe wa Africana kikaoni - Chang'ombe
Siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa - Mwl. J.K.Nyerere (14/10/2013) Kikundi cha Africana kilifanya kikao chake cha Mwezi huko Chang'ombe jijini Dar. Kikao cha mwezi Novemba kitanyika Ursino Estate, Dar Es Salaam. Wanachama mtatarifiwa tarehe kamili.
Madadaz-Ceasar Mloka, Slyvia Daulinge na Ghana Kunambi |
Silyvester Jakka na Anthony Kunambi |
Christian Mkoba,Suzy Kobelo na Maria Mkoba |
Dada Ghana Kunambi |
Dada Suzy Banzi |
Mapambo kwa raha zako!
Wakati mwingine tunakuwa na gharama zisizo za lazima kwa ajili ya mapambo. Utasiki mapambo Tzs 1,600,000/=. Ona mapambo haya yalitengenzwa kwa ajili ya harusi moja kijijini Kisemvule- Mapambo maputo, makuti, vitambaa na mkeka mambo kwisha na harusi imefanyika na ndoa inaendelea kwa mapenzi ya bashasha hadi leo!
Rhino Cement inatoka hapa
Hiki ndicho kiwanda cha Cement aina ya Rhino inayotengenezwa kijijini Kisemvule- Mkuranga mkoa wa Pwani. Cement ni nzuri, kiwanda kimeleta ajira kwa Watanzania. Je, kinasaidia nini jamii inayokizunguuka mazingira je? Hili liangaliwe ili wananchi wanafuike.
Vijana wa Kise Kids
Vijana hawa wa Timu ya soka ya kijijini Kisemvule iitwayo kwa 'Kise Kids Soccer Club' wamepania kuleta mabadiliko katika soka la Tanzania.
Matunda - Fahari ya Tanzania
Tanzania imebarikiwa kuwa na hali ya hewa na udongo mzuri unaoweza kustawisha mazao ya aina mbalimbali yakiwemo machungwa na ndizi. Angalia ndizi na machungwa yakiuzwa Mabagala Rangi tatu jijini Dar Es Salaam.
Vijana wajenzi wa nyumba Kisemvule
Kijiji cha Kisemvule mkoa wa Pwani kinakua kwa haraka sana. Karibu kila siku nyumba mpya zisizopungua 10 zinajengwa hapo kijijini. Hii imewafanya vijana wengi wa kijijini hapo kujifunza kazi ya ujenzi wa nyumba.
Subscribe to:
Posts (Atom)