Friday, February 21, 2014

Askofu Athony Banzi wa Jimbo la Tanga


Mhashamu Baba Askofu Anthony Banzi wa Jimbo la Tanga akiwa  kwenye vazi la Kiaskofu kwenye maandamano kuingia kanisani.

Polycarp Kardinali Pengo akiwa na Askofu Banzi

Polycarp Kardinali Pengo  (mwenye mkanda mwekundu) akiwa na Askofu Anthony Banzi wa Jimbo la Tanga

Askofu Anthony Banzi akiwa na mapadri

Mhashamu Baba Askofu Athony Banzi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga akiwa na mapdre wakijaandaa kwa maandamano kuingia Kanisani tayari kwa Ibada

Askofu Athony Banzi akitoa Neno

Askofu Anthony Banzi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga akitoa neno kwenye ibada ya kutoa daraja la Upadri ajimboni.

Friday, February 7, 2014

Vijana katika ujenzi

Tuwapatie vijana ujuzi wa aina mbalimbali kama huu wa uwashi

Upendo wa Jumuiya ya Mt. Joseph Parokia ya Vikindu

Wanajumuiya ya Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Vikindu wakirudi majumbani kwao baada ya kumfariji mwanajumuiya mwenzao Mzee C.Semgalawe wa Kisemvule aliyevamiwa na majambazi mwishoni mwa mwezi Januari 2014. Angalia upendo ulioje. Wakubwa kwa watoto, vijana wake kwa waume wote kwenye jumuiya.

Nyumbani kwa mwanajumuiya-Vikindu

Wanajumuiya ya Mt. Joseph  Mfanykazi, Parokia ya Vikindu wakiwa  nyumbani kwa Bw. C.Semgalawe kwa ajili ya kumfariji baada ya kuvamiwa na majambazi mwishoni mwa mwezi Januari 2014.

Pole kwa Familia ya Semgalawe

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mt. Joseph  Mfanyakazi , Parokia ya  Vikindu  Bw. Eric Mwambeleko akikabidhi pole kwa familia ya C.Semgalawe baada ya kuvamiwa na majambazi nyumbani kwao Kisemvule.

Mama Semgalawe na Bibi Josephine Mutahangarwa

Mama Semgalawe akimkubatia Bibi Josephine alipomtembelea nyumbani kwake Kisemvule tarehe 1/02/2014.

Bibi Josephina Mutahangarwa nyumbani kwa Semgalawe

Tarehe 1/2/2014. Jumuiya ya Mt. Joseph ya Parokia ya Vikindu iliitembelea familia ya Bw. Charles Semgalawe  wa Kisemvule kwa lengo la kusali pamoja na pia kumpa pole baada ya kuvamiwa na majambazi. Pichani mmoja wa wana Jumuiya Bi Josephine Mutahangarwa (a.k.a Bibi Jeshi) akikaribishwa na mwenyeji wake Mzee  Semgalawe.

Urafiki utotoni

Watoto wakipendana ni raha tupu. Hawa ni watoto wa Kisemvule, Mkuranga.

Ujenzi Kisemvule

Huyu anakribia kumaliza

Huyu anaanza
Miaka ya hivi karibuni kijiji cha Kisemvule kimekuwa kikua kwa kasi ya haraka kutoka na uwekezaji unaofanyika katika kijiji hicho kama vile kiwanda cha cement cha Rhino, Gypsum cha Wachina. Pia Kijiji cha Kisemvule kina sifa ya upatikaji wa maji mengi na mazuri pamoja na miundombinu ya barabara na umeme.Huduma za shule na hospitali na sehemu za kuabudu kwa madhehebu mbalimbali.

Vijana kazini

Macarios Banzi na rafiki yake wakiwa katika harakati za ujenzi huko Kisemvule

Mtoto wa Kisemvule

Omari Dino wa Kisemvule anafurahi mazingira ya nyumbani kwake

Mazingira yanapendeza

Minazi,migomba, nyumba  huku nguo zimeanikwa. Usafi ndani na nje. Mazingira yanapendeza