Monday, March 30, 2015
Monday, March 23, 2015
Tulipotembelea Kivule
Tupo Dar lakini wakati mwingine familia hazitembeleani. Jumamosi iliyopita familia yangu iliitembelea familia ya Dr. Julius Manandota waliohamia Kivule hivi karibuni. Ni mara yangu ya kwanza kufika Kivule lakini familia ilifurahi kwa kweli ni sehemu nzuri na watu wa Dar wanajenga aiseh. Nilichokiana ni Jiji kuimarisha miundo mbinu hasa barabara pamoja na DAWASA na TANESCO kupeleka huduma za maji na umeme.
Peter Massawe - Daktari bingwa wa Vipando vya korosho
Sekta ya kilimo kuna madaktari bingwa waliobobea katika fani mbalimbali. Mmojawapo ni Dkt.Peter Massawe-Daktari Bingwa wa Vipando (Plant Breeder) aliyebobea katika zao la korosho. Massawe ni Mratibu wa Utafiti wa Taifa wa zao la korosho. Utafiti wa zao la korosho hapa nchini unaratibiwa katika kituo cha Utafiti cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Idara ya Utafiti na Maendeleo. Mwaka huu Kamati ya Taifa ya Mbegu imeidhinisha aina 24 za mbegu bora korosho chotara zilizotafitiwa na watafiti wa zao hilo chini ya uongozi wa Dkt.Massawe. Hongera Dkt. Massawe na timu yako.
Eti Linaitwa 'Zebra Rock'
Jiwe hili linavutia. Nimelipata kwenye ukurasa wa fb wa TANAP. Eti linaitwa 'Zebra Rock' linapatikana mkoani Kilimanjaro (waliokwisha panda mlima Kilimanjaro watanieleza ni wapi hasa jiwe hili liliko). Ni moja ya kivutio cha watilii. Hapa ukiwa mchoraji unaweza kuchora picha nyingi ukilitathmini kwa makini jiwe hili. Kinachonisikitisha ni kwamba limepewa jina eti 'Zebra Rock!'
Friday, March 13, 2015
Makeke ya uncle 'Junior'- The Davido
Leo asubuhi nimebahatika kumkuta uncle Junior nyumbani kwao Buguruni -Maghorofani akijiandaa kwenda shule . Makeke yake yalikuwa kama unavyoona pichani.
Alinionesha gari lake |
Na hii ndiyo sare ya michezo shuleni kwako St Joseph Kindergarten |
Alinionesha vidole vitatu sikufahamu maana yake |
Umahiri wa kudaka mpira je? Huenda atakuwa goalkeeper wa Taifa Stars |
Hakika mapenzi yake kwa football ni dhahiri na inawezekana anaipenda Barcelona! |
Uliwadia wakati wa kwenda shule |
Na hapa ndipo nilipomuelewa kuwa ni peace - Huenda ni CHADEMA! |
Alinionyesha bag la shule lenye rangi ya njano! Kumechisha nini? |
Inapotakiwa kwenda shule ni makeke mengi tu |
Toys kibao kwa raha zake |
Angekuwa na gari yake nadhani uncle Junior angeendesha kwenda shule! |
TAZARA Sokoni-Mahakama ya ndizi
Ukitokea kituo cha mabas cha TAZARA kama unaelekea Temeke, jijini Dar kituo kinachofuata kinaitwa SOKONI. Soko hili ni maarufu kwa biashara ya ndizi mbivu wengine mahali hapa hupaita 'mahakama ya ndizi.' Kituo hiki kiko karibu na Makao makuu ya TAZARA na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Leo asubuhi nimebahatika kununua ndizi moja nzuri kwa bei ya shilingi 150/= unajua nilinunua ngapi? Kumi na mbili (12).
Azam - Tazara
Ni asubuhi, barabara ya Mandela jijini Dar. Kwa mbali nayaona majengo ya Azam, zamani National Milling Coorporation. Imenikumbusha mbali wakati huo serikali ilipokuwa inamiliki shirika hilo la umma la usagishaji na usindikaji wa nafaka. Hapo ndipo ilipokuwa ikisindikiwa mikate mizuri tuliyokuwa tukiikimbilia kila inapoonekana na kupanga foleni.
Wednesday, March 11, 2015
Wadau wa EAAPP wanavyoridhishwa na njia za kupata teknolojia
'Eastern Africa Agricultural Productivity Project' (EAAPP) ni mradi unaolenga kuongeza uzalishaji na Tija kwenye Kilimo kwa nchi za Mashariki ya Afrika. Maradi huu unatekelezwa katika nchi 4 nazo ni Tanzania (Mpunga);Kenya(Ng'ombe wa Maziwa;Uganda (Muhogo) na Ethiopia(Ngano). Mazao yaliyo kwenye mabano yanaonyesha zao kuu linaloshughulikiwa katika nchi hiyo ambapo vituo mahiri vya mazao hayo vinaimarishwa (Regional Centres Of Excellence). Hapa Tanzania, kituo mahiri cha zao la mpunga kiko katika kituo cha Utafiti wa Kilimo-KATRIN, Ifakara. Moja ya viashiria vya mradi huu ni kupima kiwango cha wadau kuridhika na upelekekaji wa teknolojia za kilimo kwa kutumia njia tofauti kama vile radio,TV, vipeperushi,mafunzo na maonyesho ya kilimo. Kwa kuzingatia chart hiyo hapo juu, inaonyesha kuwa wadau hadi kufikia mwaka huu (2015) wadau wameridhika kwa asilimia 67 ukilinganisha na asilimia 20 iliyokuwepo mwaka 2010.Haya ni mafanikio makubwa.
Hawa waling'ara tarehe 8/3/2015
Kutoka kushoto Ajibu, Okwi na Ndemla. Wachezaji hawa wasimba waling'ara siku ya mechi ya Simba na Yanga tarehe 8/3/2015 ambapo Simba iliibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi. Kwa ushindi huo Simba sasa iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi 2015 wakiwa na pointi 26 huku Young Africans ikiongoza kwa point 31.
Monday, March 9, 2015
Miwa ya kutafuna
Hapa ni Kingolwira, Morogoro. Miwa inauzwa. Hii ni miwa ya kutafuna. Kuna aina mbili za miwa.Moja ni ile ya kutafuna na ile inayotumika kutengeneza sukari. Kwa kawaida miwa ya kutengeneza sukari ni miyembamba na migumu. Miwa ya kutafuna ni laini. Hii imenikumbusha wakati nikisoma shule ya msingi nyumbani Matombo wakati wa mapumziko wanafunzi tulikuwa tukitafuna miwa kwa sana tu hadi matumbo kujaa maji mengi ukikimbia yanalia-kubwakubwkubwakubwa. Ha Moro ina kila kitu.
Iliyokuwa Abood Soap Industries-Moro
Hapa ni Msamvu Morogoro, ndipo kilipokuwa kiwanda cha kutengeneza sabuni za 'Abood Soap'. Sabuni hizi zilikuwa maarufu si kwa Moro tu bali nchi nzima. Utengenezaji wa sabuni hizi umesitishwa miaka mingi iliyopita. Kilichobaki ni majengo na sidhani kama mitambo bado ipo (sijaingia ndani ya kiwanda). Abood mwenyewe sijui anasema nini kuhusu kiwanda chake. Wakazi wa Moro waliokuwa wakifanya kazi kwenye kiwanda hiki sasa hawana ajira kwa hiyo familia zilizokuwa zikitegemea kiwanda hiki kwa kipato zimeathirika sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)