Monday, June 8, 2015

Hebu tuone familia ya Shirika la Masista wa Carmel

Shirika la Masista wa Kikatoliki la Mlima wa Carmel limetapakaa duniani kote kama mti huo unavyoonesha. Wako katika bara la Afrika, Asia, Ulaya na Amerika. Hawa ndiyo wamiliki wa Carmel Pre & Primary School Vikindu iliyopo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. Shule hii ni moja kati ya shule zinazoongoza wilayani na mkoani Pwani.

Ilibidi waeleze jinsi figo inavyofanya kazi

Wanafunzi hawa wenye vipaji wa shule ya Msingi ya Carmel iliyopo Vikindu wilaya ya Mkuranga, walikuwa na mada ya kueleza jinsi figo inavyofanya kazi. Nilipofika kwenye meza yao tarehe 6/6/2015 nilishangaa uwezo wa vijana hao katika kuelezea figo. Wanafunzi hawa wanajengwa  kuipenda sayansi kivitendo wakiwa wangali wadogo kabisa.

Katika orodha ya wanasayansi wa dunia Afrika haimo

Sikushangaa kuona orodha ya wanasayansi ndefu iliyokosa waafrika. Mwanafunzi huyu wa shule ya Carmel iliyopo Vikindu, Mkuranga mkoa wa Pwani alikuwa na mada ya kwaeleza wazazi na wadau wa shule hiyo orodha ya wanayasansi wa dunia ambao wavumbua vitu mbalimbali.

Inawezekana wakawa madaktari




Wanafunzi hawa wa shule ya msingi ya Carmel ya Vikindu inayomilikiwa na Masista wa Kikatoliki la Mlima wa Carmel kwa ujasiri na uelewa mkubwa walielezea jinsi moyo unavyofanya kazi. Haya yalifanyika siku ya tarehe 6/6/2015 kwenye maonesho ya watoto wenye vipaji shuleni hapo. Hongera! Kwa njia hii  huenda tukawapata madaktari wengi.

Wanafunzi hawa wanafahamu manufaa ya Olivera



Mimea ina manufaa mengi kwa mwanadamu. Ona jinsi mmea wa olivera unavyoweza kutumika kutengeneza sabuni, dawa ya meno na dawa nyingine. Haya tulielezwa na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Carmel ya Vikindu, Mkuranga.

Pluto ni sayari iliyo mbali sana na jua kuliko zote


Nilikwisha sahau kuwa  sayari ya Pluto ndiyo iliyo mbali zaidi  na jua takribani kilometa 5900 milioni. Sayari yetu ya Dunia ni ya tatu kutoka sayari ya jua ambayo ni umbali wa kilometa 150 milioni. Haya nilikumbushwa kwenye maonyesho ya sayansi ya 'Carmel Convent Pre & Primary School - Vikindu-Mkuranga, Pwani. Wanafunzi huyu mwenye kipaji alinielezea kwa ufasahau mkubwa sayari zinazozunguka jua. Maonesho hayo yalifanyika tarehe 6/6/2015 shuleni kwao.

Usitupe betri iliyokwisha nguvu ina manufaa mengine

Je, unafahamu kuwa unga wa betri (dry carbon part) ukichanganya na 'methanol' na kisha kupilizia uturi (perfume) unaweza kupata 'black shoe polish' ?. Mwanafunzi Maria Banzi (Pichani)wa Carmel Convent Pre & Primary School alionesha kuwa inawezekana kwenye maonesho ya sayansi yaliyofanyika shuleni hapo tarehe 6/6/2015

Maonesho ya Carmel Pre & Primary School-Vikindu 2015









 Juzi Jumamosi tarehe 6/6/2015 nilihudhuria maonesho ya sayansi ya 'Carmel Convent Pre & Primary School' iliyoko Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani. Shule hii inaendeshwa na Masista wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Mlima wa Carmel. Wanafunzi wakishirikiana na walimu wao waliandaa maonesho hayo. Watoto wenye vipaji waliochaguliwa walionesha uwezo na umakini mkubwa katika kuelezea vitu walivyoviandaa na pia kutuuliza maswali. Hongera sana walimu na wanafunzi.Mimi ni mmoja wa wazazi waliojifunza na kujikumbusha mengi katika maonesho hayo.













Africana yakutana Temboni Dar




Jana tarehe 7/06/2015 umoja wetu wa Africana tulikutana huko Kimara Temboni. Kwenye kikao hicho tulitaarifiwa kuwa mdogo wetu Christian Mkoba anatarajia kufunga ndoa mwezi Julai mwaka huu na vikao vya maandalizi ya sherehe ya harusi vimeshaanza hivyo michango inatakiwa. Aidha mradi wa kuuza T-shirt  kwa bei ya shilingi 15,000/= unaendelea na pia khanga zinachapishwa.Wanachama walikumbushwa kutoa michango yao ya kila mwezi.

Monday, June 1, 2015

Anauza mihogo ya kutafuna akiwa na simu

Biashara ya mihogo ya kutafuna inaenea kwa kasi jijini Dar. Mihogo hii ya kutafunwa waauzaji wake wengi ni wanawake. Mara nyingi huuza  na nazi kavu ya kutafuna (mbata). Uchunguzi nilioufanya wateja wengi wa bidhaa hii ni madereva wa daladala. Pichani anaonekana dada akiandaa mihogo hiyo huku akiongea na simu. Teknolojia popote!

Ilipo St. Anthony Sekondari

Hapa ni Mbagala Sabasaba ilipo St. Anthony Sekondari School inayomilikiwa na Kanisa Katoliki-Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Sekondari hii ina kidato cha tano na sita pia. Iko kando ya barabara ya Kilwa, wilaya ya Temeke, Dar Es  Salaam. Haifanyi vizuri sana miaka ya hivi karibuni, kulikoni?

Kazi ya 360 camera

Hivi ndivyo 360 camera inavyofanya kazi. Unaweza kuitoa picha kama vile imechorwa. Picha hii imepigwa maeneo ya Mbagala Rangi 3.Hongera teknolojia!

Ujenzi hauna Jumapili

Jana tarehe 31 Mei ilikuwa ni siku ya Jumapili, hata hivyo Banzi wa Moro aliwanasa wajenzi wakiendelea kujenga jumba hili la ghorofa pale Mtoni Mtongani.

Shule ya msingi Mtoni-Dar

Kando ya barabara ya Kilwa- jijini Dar ndipo ilipo Shule ya Msingi Mtoni kama inavyoonekana pichani. Wengi waliokulia sehemu za Mtoni Mtongani na kwa Aziz Ally wamesoma katika shule hii.

Usafiri Dar



Usafiri Dar uko wa aina nyingi. Kuna wanaotumia pikipiki,pikipiki za magurudumu matatu a.k.a Bajaj, mabus,taxi, na magari binafsi aina nyingi kama inavyoonekana pichani. Changamoto, baada ya mvua nyingi kunyesha barabara nyingi zimeharibika kwa hiyo si salama kwa abiria kwani husababisha ajali.

Barabara ya Kilwa matengenezoni

Sehemu ndogo ya barabara ya Kilwa kutoka kwa Aziz Ali hadi Mtoni Mtongani, ipo kwenye matengenezo na hii husababisha foleni kubwa ya magari wakati wa asubuhi na jioni. Kasi ya matengenezo ni ndogo sana. Wajenzi waharakishe kwani ni kero kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Hapa ndipo shambani kwangu

Hapa ni Temeke - Kilimo Complex, eneo la Kilimo II. Hapa ndipo lilipo shamba langu. Nimelima hapa tangu mwaka 1998.

Huyu ndiye Celesti Frank Mdimi



Binti yetu Celesti  Frank Mdimi (mwenye vazi jeupe) aliyepokea komunio ya kwanza tarehe 31Mei 2015 akiwa na mpambe wake Miss Thom (mtoto wa dada Janet Mluge)nyumbani kwa Babu na Bibi Mdimi - Makuburi-Mabibo, jijini Dar ambako alipokelewa kwa shangwe na ndugu zake  na kufanyiwa tafrija kabambe ya kumpongeza.

Napata fursa ya kuongea na Mangengesa na Mama Beaty

Jana tarehe 31 May 2015 nilikuwa nyumbani Makuburi-Dar kwa Wazee wangu Baba na Mama Mangengesa Mdimi. Nikiwa hapo nilipata fursa ya kuongea na Mzee Mdimi na Mama Beatrice P. Mhango (kulia). Hapa tunasubiri wageni ili shughuli ya kumpongeza binti yetu Celesti Frank Mdimi ianze.

Waalikwa wengine walikuja na mpira wao

Wapwa zangu Emma na mdogo wake wa kutoka Bunju wao waliingia kwenye shughuli ya komunio ya Celesti Frank Mdimi siku ya Jumapili 31 Mei 2015  pale nyumbani kwa babu Mangengesa Mdimi wakiwa na mpira na siyo Biblia. Kazi kwelikweli!

Norbert Macarios Banzi ndani ya shughuli

Watoto wetu walikusanyika kwa wingi kumpongeza dada yao Celesti. Hapa Norbert Macarios Banzi  akiwa na mama yake wageni waalikwa kwenye shughuli ya kumpongeza Celesti Frank Mdimi kupokea komunio ya kwanza siku ya jana 31 Mei 2015.

Naongea na Mama zangu


Cheki tulivyofurahi. Jana tarehe 31 Mei 2015 nilikutana na mama zangu na shangazi zangu na kupeana michapo mingi. Hapa wananiuliza vipi Kisemvule. Mimi najibu- Poa tu huku tukigongeana. Safi sana. Hapo tuko nyumbani Makuburi -Mabibo, Dar Es Salaam.

Celesti Frank Mdimi ametuita Makuburi!

Da Meab Mdimi na dogo Macarios Banzi 

Mzee Mangengesa Mdimi (mwenye koti la kitenge) Mama Dolorose Mdimi, Aunt Restituta Mluge (anayecheka) na Aunt Frida Mluge (aliyenipa mgongo)

Da Meab Mdimi na Da Suzy Banzi (Mrs. Mwanadota)

Naongea na Mama Doro (Mrs. Mangengesa Mdimi) wengi ni shem Thom aunt Fridah Mluge na Dada Meab Mdimi (gauni nyeupe)

Binti yetu Celesti Frank Mdimi kwa  mara ya kwanza amepokea sakramenti ya Ekaristi Takatifu ndani ya Kanisa Katoliki Makuburi-Dar Es Salaam siku ya Jumapili tarehe 31/05/2015. Kwa furaha hiyo ndugu tulikusanyika nyumbani kwa Mangengesa Mdimi  pale Makuburi, Dar kumpongeza.Tukio hilo limetukutanisha ndugu na jamaa wengi

Naongea na wapwa zangu

Jana tarehe 31 May nilikuwa nyumbani Makuburi, Mabibo-Dar. Kulikuwa na shughuli ya kumpungeza binti wetu Celesti Frank Mdimi kupokea komunio ya kwanza. Hapa naongea na wapwa zangu waalikwa kwenye shughuli!