Monday, August 31, 2015

Kutoka 1980-2015 Wana TOSA wakutana

Schoolmates- TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL- Kutoka kushoto Packshard Mkongwa, Nicodemus Mboje na John Banzi. Tulipokutana Double View Hotel, Sinza tarehe 29/08/2015. Ilikuwa siku nzuri sana ajabu. Lengo ni kumpongeza John Mboje kwa kufunga ndoa na binti mrembo -cheupe (picha ya chini). Tuliwapongeza kwa niaba ya TOSA alumni. Asanteni sana. Watoto wameshakuru na kufurahi kwa mzigo!
(pichani)

Wataalamu nje ya nchi

Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakiwa mafunzoni-Mananga, Swaziland

Bwawa la kuogelea-Chuoni Mananga

Pembezoni  mwa mabweni, ukumbi wa starehe na dinning hall kuna bwawa la kuogelea ambalo husafishwa na kujaza maji safi kila siku. Hapa ni chuoni Mananga- Swaziland

Familia inapowapa "company"

Waafrika tuna mapenzi makubwa. Tulipotembelea Afrika ya Kusini, dereva wetu pamoja na familia yake (mke na mtoto pichani- wengine ni wa Tz Dr. Nkuba na Bw. Mjema) walisafiri nasi na kutuelekeza kila tulichotaka kuelewa wakati wa safari hiyo. Binti huyo mdogo anaitwa Nashera.. kuna wakati aliponiona nakuja akaongea kwa Kiswati .....'mkulu' akiwa na maana mkubwa au mzee anakuja  alifurahi kwamba sasa safari itaanza kuendelea kama kawaida kwani mkulu ameshaingia ndani ya gari. Hata kwa Kiliguru 'mkulu' ina maana ni mkubwa kweli Waafrika wengi ni Wabantu!

Nje ya nyumba ya asili ya Waswati

Tulipotembelea Mantenga Cultural Village nchini Swaziland, nilivutiwa na nyumba hii ya asili. Ni nyumba imara isiyovuja na imejengwa kwa ustadi mkubwa huko ulinzi ukipewa kipaumbele bila kusahau kuwapanga watu kwa jinsi wakati wa kulala humo ndani na huku bibi akilala kati kati.Haki wazee wetu walikuwa na lojik na falsafa zao katika maisha.

Moja ya sehemu za maduka jijini Mbabane

Nchini Swaziland watu wengi hupendelea kununua mahitaji yao kwenye maduka makubwa. Hata wanafunzi hufurika kwenye maduka hayo wakati wa jioni. Unaweza kuliona kwa mbali duka moja linalouza bidhaa za Mr. Price hasa nguo.

King Mswati wa III hutawala na mama yake

Nchi ya Swaziland inaongozwa na Mfalme - King Mswati wa III. Huyu huongoza nchi yake kwa kushirikiana na Mama yake  kwa hiyo kimadaraka kwanza ni King halafu Mama na anayefuata ni Waziri Mkuu ambaye pia huteuliwa na King. Angalia jinsi picha zilivyobandikwa.

Kuelekea Afrika ya Kusini




Kundi letu tulipata bahati ya kutembelea mji wa Afrika ya Kusini ambao hauko mbali sana na Swaziland. Mji huu unaitwa Nelspruit ni makao makuu ya jimbo la Mpumalanga. Nilivutiwa na barabara nzuri. Na kweli kwa mwendo wa masaa takribani mawili sikuweza kuona ajali barabarani!

Mazingira murua ya kujifunza chuoni Mananga



Mara nyingi nilikuwa mimi na facilitator wangu darasani mwangu nikiwa na vifaa muhimu ikiwemo kompyuta mpakato kwa kuwa nilitengenezewa moduli ya peke yangu kwa kile nilichotaka kujifunza. Pichani ni mmoja wa facilitator, Mr. Vincent Loveday

Agosti - Kwa Mswati III

Wiki mbili za mwezi Agosti nilikuwa nchini Swaziland  kwa mafunzo ya muda mfupi kuhusu Project Management kwenye chuo cha Mananga pale Ezwilini. Mafunzo yaliyoniongezea utaalamu kuhusu menejimenti za miradi pamoja na masuala mtambuka kama jinsia na mazingira.