Friday, October 30, 2015
Monday, October 26, 2015
Friday, October 23, 2015
Niliosoma nao Kirusi-Tashkent
Hili ndilo kundi nililosoma nalo lugha ya Kirusi nikiwa Tashkent, Uzbekstan ( former republic of USSR). Hapa naweza kuwakumbuka wachache kwa majina. Kushoto kwangu ni Osama kutoka Syria anayefuata ni Dada Aurelia kutoka Madagascar (Huyu alikuwa ni mkali wa computer, Hesabu na Kirusi) wengine ni madada kutoka Nicaragua. Ilikuwa ni mwaka 1987 katika Kitivo cha Maandalizi ya Wanafunzi.Baadaye niliendelea na masomo yangu katika mji wa Simferepol huko Ukraine mji ambao Russia umeuchukua tena kama sehemu ya nchi yao.
Unapokuwa na watoto unajifunza lugha kwa wepesi zaidi
Nilipokuwa katika mji wa Tashkent huko Uzbekstan ambako nilipangiwa kujifunza lugha ya Kirusi kabla ya kuendelea na masomo yangu ya uchumi kilimo, niliweza kujifunza lugha hiyo kwa kuongea kuongea na wananchi wa aina mbalimbali ili kupata uzoefu. Pichani niko na mwanafunzi mwenzangu kutoka Kigoma, Tanzania (jina nimelisahau) tukiwa na wanafunzi wa shule ya msingi. Tuliwaomba kupiga picha wakati wakirudi nyumbani kwao wakitoka shuleni. Tuliweza kuzungumza nao kwa kirusi na kutuelewa. Wakati huo tulikuwa tumetimiza miezi mitatu tu tangu tutoke nyumbani Tanzania mwaka 1987.(Picha kutoka Maktaba ya John Banzi)
Ezrome Magagula- Facilitator Mananga
Ezrom Magagula ni Mwalimu wangu wa masuala ya Menejimenti. Ezrome ana kipaji kikubwa kwenye masuala ya Menejimenti akikufundisha Human Resource Mgt utampenda, Monitoring and Evaluation yumo sana, Gender and Environment Mgt safi sana. Project Management zaidi sana. Ukibahatika kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi Mananga Centre for Regional Integration and Management Development unaweza kukutana naye kama hajaenda kutafuta "malisho ya kijani"
Mimi Kipaumbele changu ni Kilimo
Hivi bila shibe utasoma? Kwanza chakula, Elimu baadaye. Nakumbuka nilipokuwa Tosamaganga High School (Kidato cha 5-6) Mkuu wa Shule Mpogole alikuwa anatupatia chakula kizuri. Kila siku mchana sisi tulikuwa tunakula wali na nyama, mara moja kwa juma tunapata karanga za kukaanga (nusu kilo). Kweli tulikuwa na upungufu wa waalimu wa Chemistry na Biology lakini tulifundishana wenyewe kwa wenyewe hadi tulipopata walimu hao tukiwa kidato cha sita. Ajabu tulifaulu wote na sasa wengine ni maprofesa vyuo vikuu na wengine ni mabingwa katika fani mbalimbali kwa sababu tulishiba na si kushiba tu tulipata balanced diet. Muulize George Nyaupumbwe a.k.a Ngi wa TRA.
Upendo wa Waafrika
Tulipokuwa nchini Swaziland kwa mafunzo ya muda mfupi mtoto huyu,mama yake na baba yake ambaye ni mfanyakazi wa Mananga Centre for Regional Integration and Management Development walikuwa nasi kwenye safari ya kutembelea mji wa Nelspruit nchini Afrika ya Kusini. Angalia jinsi Waafrika walivyo na upendo. Hii ni nadra sana kutokea huko Ulaya.
The Mantenga Cultural Group-Swaziland
Tanzania tuna vikundi vingi vya aina hii, lakini miaka ya hivi karibuni naona vimedorora. Tuna nafasi kubwa ya kuendeleza vikundi vya utamaduni kujenga uzalendo nchini na pia kutangaza nchi yetu. Ni moja ya chanzo cha ajira kwa vijana wetu.
Zamani Motel Agip
Hotel Agip, zamani Motel Agip kama ilivyokutwa na JB jana wakati nikiwa AFC (Azania Front Cathedral). Miaka ya themanini Motel Agip ilikuwa ndiyo mpango mzima. Vijana walikutana hapo kwa mipango mbalimbali hasa starehe. Disco la nguvu lilikuwa likipigwa hapo. Sikuhizi licha ya kubadilisha jina na kuwa Hotel ni cha mtoto kabisa sikuhizi kuna Hotel za viwango vya juu ikiwemo Serena!
Mara ya mwisho ya kula chakula na Mangengesa Mdimi
Katikati ni mjomba wetu Charles Pius Hugo kushoto akichekesha,mama Dolorosa Mdimi na kulia ni Mzee Chrispin Mangengesa Mdimi ( R.I.P.) hii ni picha ya ukumbusho wa chakula cha pamoja na Mzee Mdimi wakati wa kupokea mahali ya binti wake wa mwisho Bi.Hellena Mdimi pale External-Makuburi jijini Dar. Mzee Mdimi alifariki tarehe 12/10/2015 na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 15/10/2015.
Vijana wanapopenda vitu ghali!
Kijana wangu Sisty Banzi anapenda sana magari. Angalia jinsi alivyodiriki kupiga picha mbele ya gari ya babu yake Dr. Gregory P.Mluge (R.I.P). GMC ni gari ya kimarekani.Ni gari zuri na la kifahari lakini matumizi yake ya mafuta utachoka mwenyewe hata bei ya vipuri ni ghali sana. Lakini kupanga ni kuchagua. Akitaka kumiliki gari kama hili lazima ajitume katika kazi na kuingiza kipato cha kutosha. Vinginevyo ataishia kupiga picjha mbele ya gari ya babu!
Subscribe to:
Posts (Atom)