Ni mara yangu ya kwanza kula supu ya kwale. Wengine wamekula mayai ya kwale kwa sababu zao, lakini mimi pamoja na familia yangu tarehe 26/12/2015 baadhi yetu tulibahatika kuonja supu ya kwale (tamu sana!). Pamoja na vitafunio vingine yakiwemo mayai na mkate lakini tuliokula supu ya Kwale kwa kweli tunachakuongea siku ya kufungua mabox ya mwaka huu!
Monday, December 28, 2015
Supu ya Kwale nyumbani kwa Mkude
Ni mara yangu ya kwanza kula supu ya kwale. Wengine wamekula mayai ya kwale kwa sababu zao, lakini mimi pamoja na familia yangu tarehe 26/12/2015 baadhi yetu tulibahatika kuonja supu ya kwale (tamu sana!). Pamoja na vitafunio vingine yakiwemo mayai na mkate lakini tuliokula supu ya Kwale kwa kweli tunachakuongea siku ya kufungua mabox ya mwaka huu!
Chrsitmass ya marafiki watatu- Mbezi Msakuzi
Mkude, Luanda na Banzi ni marafiki wa siku nyingi. Urafiki wao ulianza baada ya kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza Njombe Sekondari mwaka 1974. Wote watatu wanatoka Matombo Morogoro kama majina yao ynavyosomeka. Hivi sasa wote wanafamilia zao. Kutoka kushoto ni John Banzi na mkewe Nancy, Lawrence Mkude na mkewe Sango na Bw. Michael Luanda na mkewe Mama Adela. Bw na Bibi Luanda Desemba mwaka huu wametimiza miaka 30 ya ndoa. Pongezi na vigelegele kwa upendo na maisha ya uvumilivu katika ndoa. Hapa tupo nyumbani kwa akina Luanda, Mbezi-Msakuzi jijini Dar (25/12/2015).
Bw na Bibi Michael Luanda miaka 30 ya ndoa
Hongereni Bw. na Bibi Michael Luanda wa Mbezi Msakuzi kwa kutimiza miaka 30 ya ndoa yenu. Michael Luanda ni rafiki yangu na ndugu yangu. Tunatoka wote Matombo, Morogoro tumesoma wote shule ya msingi Matombo. Sekondari Njombe tulikuwa sote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha Nne. Wazazi wetu (wote marehemu) walikuwa wanafahamiana toka udogo wao na wote wameishi jijini Dar. Michael ndiye baba wa ubatizo wa mwanangu Sisty Banzi na Mama Luanda ni mama wa ubatizo wa binti yangu Catherine Banzi. Ni udugu wa familia na kiroho pia.
Thursday, December 17, 2015
Maabara ya udonngo kituo cha Utafiti Kilimo Mlingano
Jukumu Kuu la kituo cha Utafiti wa Kilimo Mlingano kilichoko wilaya ya Muheza mkoani Tanga nchini Tanzania ni kufanya utafiti wa udongo kwa ajili ya ustawishaji wa mazao mbalimbali hapa nchini. Kituo hiki kina maabara kubwa ya utafiti wa udongo tunaweza kuiita ni maabara ya rufaa kwa rutuba ya udongo nchini Tanzania. Hapa unaweza kupata majibu ya aina ya udongo na ushauri wa zao gani la kustawisha ili kuongeza uzalishaji na tija.
Wednesday, December 16, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)