Wednesday, October 19, 2016
Wednesday, September 28, 2016
Hili ni group langu nililosoma nalo nchini Urusi
Hili ni group langu la masomo nilipokuwa nchini Urusi kwa masomo yangu.Katika Group hili nawakumbuka wachache kwa majina hasa hao waafrika kutoka kushoto Mamadu (Mali) Mohamed Barrie (Sierra Leone), Mansary (Sierra Leone) na Alex Konte (Siera Leone). Mimi niko mkono wa kushoto wa Mamadu. Hapa ilikuwa ni Crimea, Simferopol mwaka 1989. Nadhani wa kwanza kushoto ni Kutryova na kushoto kwangu ni Svetlana.
Miaka 80 ya Simba Sports Club nilikuwepo uwanjani
Nilikuwepo uwanjani pamoja na mashabiki lukuki wa Simba nikimshuhudia mnyama akimrarua AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar Es Salaam. Wote tukiimba kila mtu 'Mavugooo'. Mchezaji huyu wa Kimataifa kutoka Burundi, Laudit Mavugo alitupia bao katika mechi yake ya kwanza akiichezea SSC. Ilikuwa raha sana. Nimeweka kumbukumbu ya kuhudhuria mechi ndani ya uwanja wa Taifa wakati Simba inatimiza miaka 80 tangu ianzishwe.
Thursday, September 22, 2016
Kunywa maziwa kutoka Meatu
Nadhani somo limeeleweka na limekubalika. Mkuu wa Mkoa wa Shimiyu Mhe. Anthony Mtaka akionyesha maziwa ya Meatu. Hakika inafurahisha na inapendeza. Cha kufurahisha Maziwa hayo yanatengenezwa na mradi wa vijana. Hivyo ni moja ya vyanzo vya ajira na mapato kwa vijana.(Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)
Thursday, September 15, 2016
Unapoitaja Matombo unagusa matunda na machenza
Machungwa na machenza ya Matombo, Morogoro ni matamu sana. Tatizo
wafanyabiashara wameingilia kati biashara hii na kuyauza machenza na
machungwa wakati bado hayajafikia kukomaa kibailojia (Yanakomaa yakiwa
mtini). Kibaya zaidi huchanganya machungwa au machenza mazuri na mabaya.
Mlaji akibahatika hula chenza tamu na ikiwa hana bahati unaweza kula
chenza chungu. Hii ni kuharibu biashara na umaarufu wa machungwa au
machenza ya nyumbani Matombo. Kwa kawaida machungwa huanza kuvunwa kuanzia mwezi machi hadi Juni.
Tuangalie ugonjwa wa nyanya kuoza kitako (Blossom endrot)
Baadhi ya wakulima wa nyanya wamekuwa wakipata tatizo la nyanya zao kuungua chini ya kitako na kuharibu kabisa ubora wa nyanya hizo. Wanataalamu wanatueleza kuwa ugonjwa huo unaitwa kuoza kitako (Blossom endrot). Hii husababishwa na mmea kukosa maji ya kutosha au kutofuata ratiba ya umwagiliaji kwa zao hilo.Unakuta siku nyingine unamwagilia asubuhi siku nyingine mchana au unamwagilia Jumamosi halafu unarudia tena kumwagilia siku ya Jumanne huko ndiko kutozingatia ratiba ya umwagiliaji. Hiki ndicho chanzo kikuu cha ugonjwa huo wa kuoza kitako.
TIBA
Ondoa matunda yote yaliyo athirika halafu anza kufuata na kuzingatia ratiba ya umwagiliaji wa shamba lako.
(Hii nimeinyaka kutoka fb wafanyakazi wa kilimo Mifugo na uvuvi na kuikarabati kidogo na kuirusha kwani ni wengi wanalima nyanya na hasa na kuwaona wanamwagilia maji kiubabaishaji tu).
Ondoa matunda yote yaliyo athirika halafu anza kufuata na kuzingatia ratiba ya umwagiliaji wa shamba lako.
(Hii nimeinyaka kutoka fb wafanyakazi wa kilimo Mifugo na uvuvi na kuikarabati kidogo na kuirusha kwani ni wengi wanalima nyanya na hasa na kuwaona wanamwagilia maji kiubabaishaji tu).
Wednesday, September 14, 2016
Bus la Yutong la Wachina
Hili ni bus la Yutong la kutoka Uchina. Utawapenda tu. Wachina ni wazuri kwa teknolojia. Hutengeza kuteka matakwa ya mdau. Hapa Tanzania kwa sasa naweza kusema kuwa asilimia 80 ya mabus ni ya Kichina. Inasemekana ni bei poa ukilinganisha na mabus aina ya Scania au Marcopolo. Kingine wanachofanya Wachina ni kuongeza thamani ya bidhaa. Ukipanda mabus yao yalivyorembwa na kuwekewa vikorombwezo vingine hakika hutoacha kulipanda tena. Sisi tutaanza lini kuunda mabus yetu?
Haya ni machenza kutoka Matombo - Morogoro
Machungwa na machenza ya Matombo, Morogoro ni matamu sana. Tatizo wafanyabiashara wameingilia kati biashara hii na kuyauza machenza na machungwa wakati bado hayajafikia kukomaa kibailojia (Yanakomaa yakiwa mtini). Kibaya zaidi huchanganya machungwa au machenza mazuri na mabaya. Mlaji akibahatika hula chenza tamu na ikiwa hana bahati unaweza kula chenza chungu. Hii ni kuharibu biashara na umaarufu wa machungwa au machenza ya nyumbani Matombo. Kwa kawaida machungwa huanza kuvunwa kuanzia mwezi wa Machi hadi Mei.
Friday, July 1, 2016
Tuesday, June 21, 2016
Kilimo cha bamia kama ufugaji wa kuku wa mayai!
Kitu ambacho nilikuwa sifahamu ni jinsi unavyoweza kuvuna bamia. Bamia linaweza kuvunwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. Kuna mtu ameninong'oneza. Bamia wakati wowote hukua, tena kwa haraka ukichelewa linakomaa na hivyo kuwa gumu na kutofaa kuliwa kama mboga labda kulitunza kwa mbegu.Hivi sasa navuna bamia katika sehemu ndogo niliyolima pale nyumbani kwangu Kisemvule. Kweli kilimo cha bamia ni kama ufugaji wa kuku wa mayai.
Thursday, May 19, 2016
Tanzania imepania kuongeza uzalishaji wa mpunga
Mpunga ni zao linalostawi vizuri katika sehemu nyingi za nchi yetu hasa ukanda wa pwani na mabonde yanayozunguka maziwa yetu na inakopita mito mikubwa. Wakulima wengi huzalisha wastani wa tani 2 kwa hekta ambapo ni kidogo sana. Utafiti uliokwishafanyika hapa nchini unaonyesha kuwa kwa kutumia teknolojia bora za kilimo cha mpunga, uzalishaji unaweza kufikia tani 8
kwa hekta. Hivi sasa serikali inaboresha kilimo hicho kupitia miradi mbalimbali hasa kwenye skimu za umwagiliaji.
kwa hekta. Hivi sasa serikali inaboresha kilimo hicho kupitia miradi mbalimbali hasa kwenye skimu za umwagiliaji.
Ni changamoto
Wapenzi wa Banzi wa Moro nimerudi kuwajuza.
Inapotokea kuwa na njia mbalimbali za kupeana habari na msambazaji habari ni huyohuyo ni changamoto kwa kweli. Kuingia kwa facebook na whatsapp kwa kweli kumeimomonyoa blog yangu. Inakuwa vigumu kupost kwenye blog. Naweza kupost kutoka whatsapp kwenda facebook tukio hilohilo lakini siwezi kufanya hivyo kwenda kwenye blog. Uzuri wa whatsapp na facebook ni rahisi kupata feedback hivyo kukufanya kuandika na kupost. Hata hivyo nimerudi, nitaanza kuning'iniza kadri ninavyoweza nipatapo wasaa.
Dereva Mwandamizi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Ndg.Shushu Kondowe akiwasilisha taarifa ya mafunzo kwa mratibu wa mafunzo Bw. John Banzi
Inapotokea kuwa na njia mbalimbali za kupeana habari na msambazaji habari ni huyohuyo ni changamoto kwa kweli. Kuingia kwa facebook na whatsapp kwa kweli kumeimomonyoa blog yangu. Inakuwa vigumu kupost kwenye blog. Naweza kupost kutoka whatsapp kwenda facebook tukio hilohilo lakini siwezi kufanya hivyo kwenda kwenye blog. Uzuri wa whatsapp na facebook ni rahisi kupata feedback hivyo kukufanya kuandika na kupost. Hata hivyo nimerudi, nitaanza kuning'iniza kadri ninavyoweza nipatapo wasaa.
Dereva Mwandamizi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Ndg.Shushu Kondowe akiwasilisha taarifa ya mafunzo kwa mratibu wa mafunzo Bw. John Banzi
Thursday, March 31, 2016
Wednesday, March 2, 2016
Wataalamu wa ERPP ofisini Mvomero
Mradi wa kuongeza uzalishaji wa Mpunga (ERPP) umeshaanza. Mradi huu utatekelezwa katika wilaya tatu za mkoa wa Morogoro (Mvomero,Kilosa na Kilombero). Skimu za umwagiliaji zitahusika nazo ni Kigugu, Mbogo-Kamtonga, Mvumi, Njage na Msolwa. Pichani wataalamu wakielezea jinsi mradi huo utakavyotekelezwa ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo Halamshauri ya Mvomero (Haonekani).
Padri Abdoni Antipas Nzegesela akisoma Injili
Padri Abdoni Antipas Nzegesela ni Paroko wa Parokia ya Ilonga iliyoko Kilosa- Kanisa Katoliki jimbo la Morogoro. Pichani anaonekana akisoma Injili ndani ya Kanisa Katoliki Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Ndiye aliyefungisha ndoa ya Bw. Macarios Banzi na Bi. Martina Jeremias siku ya tarehe 6/02/2016
Bango bora la Shule ya Msingi Kisemvule
Huenda likawa bango bora kabisa kwa shule za msingi za wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Ni shule ya msingi Kisemvule. Kila kitu kiko wazi.Huu ni ubunifu wa mwalimu mku wa shule hiyo ambaye amehamishiwa hapo shule hivi karibuni. Nilipouliza gharama ni Tshs 150,000/= na kiasi kikubwa cha fedha kimetolewa na Serikali ya Kijiji cha Kisemvule. Hongera Mwenyekiti na Kamati yako ya Kijiji. Kujitangaza ni maendeleo pia!
Skimu ya umwagiliaji ya Msolwa kuboreshwa
Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakikagua skimu ya umwagiliaji ya Msolwa iliyoko wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro ambayo kupitia Mradi mpya wa " Expanded Rice Production Project" ulioanza kutekelezwa mwaka 2015/16 ni moja ya skimu zilizo kwenye mpango wa kuziboresha ili ziweze kuongeza uzalishaji wa mpunga nchini.
Samaki-Faida inayoweza kupatikana kwenye skimu za umwagiliaji
Hivi karibuni nilitembelea skimu ya umwagiliaji ya kijiji cha Msolwa kilichoko wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro. Nilishangaa kuwaona watoto hawa wakivua samaki kwenye skimu hiyo. Hii ina maana kuwa kwenye skimu za umwagiliaji, wakulima wanaweza kutenga sehemu na kuwa na mabwawa ya kufuga samaki na kujipatia kitoweo pamoja na mapato kwa kuuza samaki hao.
Saturday, February 27, 2016
Sh2-Mdundo bila umeme
Wote hawa wanafurahi mdundo wa ngoma ya Kiluguru iitwayo shilingi 2. Hii ngoma ilitumbuiza siku ya harusi ya Bw na Bibi Macarios Banzi. Kikundi hiki ni cha watu sita na kila mmoja hupiga,huimba na kucheza. Kwa kawaida hupiga ngoma kwa muda mrefu na hubadilisha midundo mumo kwa mumo. Unacheza upendavyo. Hiyo ndiyo shilingi 2 mdundo bila umeme wala amplifier!
Subscribe to:
Posts (Atom)