Thursday, January 21, 2016

Watu wanavyoiibia DAWASCO

Ona jinsi baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam wanavyoiibia DAWASCO na kusababisha wakazi wengine kukosa maji na huyu jamaa akiendesha biashara ya kuuza maji.

Mtafiti Abubakar Mzandah akiwa shambani

Watafiti wa Kilimo nchini Tanzania wanaendelea kutoa mchango mkubwa katika kuinua kilimo nchini kwa kugundua teknolojia mbalimbali za kilimo zinazotumika katika kuleta tija. Pichani Mtafiti Abubakar Mzandah  kutoka kituo cha Utafiti Ilonga akiwa shambani.

Karafuu kijijini Konde-Matombo-Morogoro

Pengine wengi wetu tunafikiri kuwa Karafuu inastawi visiwani Pemba na Unguja tu. Hapana, huko Morogoro vijijini katika kijiji cha Konde tarafa ya Matombo, karafuu hustawi pia. Hii ni karafuu iliyooteshwa kijijini hapo. Wakulima wa Konde wameanza kufaidika na kilimo cha karafuu na kubadili maisha yao kutokana na kilimo cha zao hilo.

Dr.Shein enzi hizo

Dr. Shein enzi hizo Baba wa familia hakujua kama siku moja atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

Ibra Ajibu wa Simba anapoweka mpira kimiani

Kwa sasa habari ya mujini ndani ya klabu ya Simba ni mchezaji kijana Ibrahimu Ajibu (Mwenye jezi nyekundu karibu na goli). Ni mshambuliaji anayesumbua sana ngome za wapinzani. Akipata wawili wa kusaidiana naye, Simba itakuwa hatariiii!

Hii ndiyo CT-SCAN

Hiki ndicho chombo kinachoitwa CT-SCAN ambacho ni muhimu kuwepo kwenye maabara kwa ajili ya vipimo maalumu. Ni chombo ghari sana. Walio kwenye sekta ya tiba wanaweza kutujuza zaidi umuhimu wa chombo hiki.

Hata mimi ningechagua sambusa

Kama ningekuweko kwenye tukio hili hakika ningechagua sambusa. Napenda sana sambusa za nyama na si za kunde! Angalizo, ukila sambusa zilizo chacha jiandae kusumbuliwa na tumbo.

Waziri Mkuu alipotua Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuuwa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa wakati wa mapokezi. Kulia ni mke wa Waziri Mkuu, Bi. Mary Majaliwa (Mbawala).

DAR ES SALAAM ya leo siyo ya jana






Hivi ndivyo ilivyo kwa sasa Dar. Mji unakua kwa kasi ya kutisha. Sekta ua Ujenzi inaongoza. Picha hizo zinaonyesha hali hali kandao ya barabara ya Uhuru sehemu za Ilala (picha za Juu) na hizi za chini ujenzi unaoendelea kando ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Kawawa pale Morocco.

Jengo la UWT katika ubora wake


Hili jengo (Mfano wa Meli) ni Kitega Uchumi cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Lipo kando ya makutano ya Barabara ya Kawawa na Ally Hassan Mwinyi pale Morocco, Dar Es Salaam. Jengo hili kwa kweli ni zuri na linavutia. Ni ubunifu mkubwa umetumika katika kuchora mchoro wa jengo hili. Ndani ya jengo hili kuna ofisi za mashirika mengi ya binafsi, serikali na ya kimataifa. Hapa ndipo yalipo makao makuu ya Kampuni ya simu ya Airtel-Tanzania. Aidha hapa  ndipo yalipo makao makuu ya "Presedential Delivery Bureau"  (PDB) ya Big Results Now.

Friday, January 15, 2016

Sijachelewa-Happy New Year

Kweli sijachelewa. Heri na Baraka za mwaka mpya 2016. Nilishindwa kabisa kuwaaga. Ah, mambo mengi bwana. Mwaka 2015 haukuwa mzuri sana kwangu. Misiba, na kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme kumezorotesha mawasiliano yangu kupitia Blog hii, Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2015 niliweza kuning'iniza posts 257 tu ukilinganisha na posts 956 mwaka 2014. Sababu nyingine kubwa ni kuibuka kwa njia nyingine ya mawasiliano hasa Facebook. Mwaka 2015 nimeweza kuweka posts nyingi kupitia facebook za group mbalimbali.Wakati mwingine nimetumia muda mwingi kujishughulisha na Whatsapp. Kilichonipa nguvu kwenye facebook na whatsapp ni kupata feedback kutoka kwa wadau ukilinganisha kwenye blog ambapo ni nadra kupata feedback.

Hata hivyo mwaka 2015 mafanikio haykukosekana kwangu binafsi na kwa familia. Nimeweza kukutana na ndugu na jamaa kupitia vikundi mbalimbali hasa 'Africana Group'   (Pichani). Nimeweza kushiriki shughuli za Kanisa
Kura nilipiga na kushangilia  nyumbani kwangu Kisemvule na kumpata Rais, Mbunge na madiwani.
Nilipata fursa ya kutaniana na uncles kama vile Junior a.k.a 'Davido' pichani
Nawatakia mwaka mpya wa mafanikio na pia tuimarishe mawasiliano kwani maisha ni kuwasiliana.