Wote hawa wanafurahi mdundo wa ngoma ya Kiluguru iitwayo shilingi 2. Hii ngoma ilitumbuiza siku ya harusi ya Bw na Bibi Macarios Banzi. Kikundi hiki ni cha watu sita na kila mmoja hupiga,huimba na kucheza. Kwa kawaida hupiga ngoma kwa muda mrefu na hubadilisha midundo mumo kwa mumo. Unacheza upendavyo. Hiyo ndiyo shilingi 2 mdundo bila umeme wala amplifier!
Saturday, February 27, 2016
Sh2-Mdundo bila umeme
Wote hawa wanafurahi mdundo wa ngoma ya Kiluguru iitwayo shilingi 2. Hii ngoma ilitumbuiza siku ya harusi ya Bw na Bibi Macarios Banzi. Kikundi hiki ni cha watu sita na kila mmoja hupiga,huimba na kucheza. Kwa kawaida hupiga ngoma kwa muda mrefu na hubadilisha midundo mumo kwa mumo. Unacheza upendavyo. Hiyo ndiyo shilingi 2 mdundo bila umeme wala amplifier!
Harusi ya Macarios Banzi- Watu walicheza sana
Harusi ya Macarios- Kila mmoja aliyekuwa ukumbuni alicheza jinsi alivyogusa kuna wale waliogswa na ngoma ya asili ya shilingi 2 kuna sisi vijana wazamani tulioguswa na old is gold na vijana walicheza bongo flava na kwaito. Woo kwa kweli hapakukalika. Hebu check picha ya chini kabisa mimi mambatsa mu moko pamoja na Mr.Mkude tukiyarudi magoma!
Meza moja na marafiki zangu wa Tosamaganga
Picha ya Juu. Tangu mwaka 1978 hadi leo, kutoka Tosamaganga hadi Dar miaka zaidi ya 36 sasa. Banzi, George Mnyitafu (Ngi) na Chris Kalanje (aliyevalia miwani) kushoto kwake Mrs.George. Walisafiri hadi Vikindu kunipa tough na kumpongeza dogo Macarios kwa kufunga ndoa. . Pembeni yao na marafiki wapya maisha mapya Vikindu. Asanteni sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)