Hili ni group langu la masomo nilipokuwa nchini Urusi kwa masomo yangu.Katika Group hili nawakumbuka wachache kwa majina hasa hao waafrika kutoka kushoto Mamadu (Mali) Mohamed Barrie (Sierra Leone), Mansary (Sierra Leone) na Alex Konte (Siera Leone). Mimi niko mkono wa kushoto wa Mamadu. Hapa ilikuwa ni Crimea, Simferopol mwaka 1989. Nadhani wa kwanza kushoto ni Kutryova na kushoto kwangu ni Svetlana.
Wednesday, September 28, 2016
Miaka 80 ya Simba Sports Club nilikuwepo uwanjani
Nilikuwepo uwanjani pamoja na mashabiki lukuki wa Simba nikimshuhudia mnyama akimrarua AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar Es Salaam. Wote tukiimba kila mtu 'Mavugooo'. Mchezaji huyu wa Kimataifa kutoka Burundi, Laudit Mavugo alitupia bao katika mechi yake ya kwanza akiichezea SSC. Ilikuwa raha sana. Nimeweka kumbukumbu ya kuhudhuria mechi ndani ya uwanja wa Taifa wakati Simba inatimiza miaka 80 tangu ianzishwe.
Thursday, September 22, 2016
Kunywa maziwa kutoka Meatu
Nadhani somo limeeleweka na limekubalika. Mkuu wa Mkoa wa Shimiyu Mhe. Anthony Mtaka akionyesha maziwa ya Meatu. Hakika inafurahisha na inapendeza. Cha kufurahisha Maziwa hayo yanatengenezwa na mradi wa vijana. Hivyo ni moja ya vyanzo vya ajira na mapato kwa vijana.(Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)
Thursday, September 15, 2016
Unapoitaja Matombo unagusa matunda na machenza
Machungwa na machenza ya Matombo, Morogoro ni matamu sana. Tatizo
wafanyabiashara wameingilia kati biashara hii na kuyauza machenza na
machungwa wakati bado hayajafikia kukomaa kibailojia (Yanakomaa yakiwa
mtini). Kibaya zaidi huchanganya machungwa au machenza mazuri na mabaya.
Mlaji akibahatika hula chenza tamu na ikiwa hana bahati unaweza kula
chenza chungu. Hii ni kuharibu biashara na umaarufu wa machungwa au
machenza ya nyumbani Matombo. Kwa kawaida machungwa huanza kuvunwa kuanzia mwezi machi hadi Juni.
Tuangalie ugonjwa wa nyanya kuoza kitako (Blossom endrot)
Baadhi ya wakulima wa nyanya wamekuwa wakipata tatizo la nyanya zao kuungua chini ya kitako na kuharibu kabisa ubora wa nyanya hizo. Wanataalamu wanatueleza kuwa ugonjwa huo unaitwa kuoza kitako (Blossom endrot). Hii husababishwa na mmea kukosa maji ya kutosha au kutofuata ratiba ya umwagiliaji kwa zao hilo.Unakuta siku nyingine unamwagilia asubuhi siku nyingine mchana au unamwagilia Jumamosi halafu unarudia tena kumwagilia siku ya Jumanne huko ndiko kutozingatia ratiba ya umwagiliaji. Hiki ndicho chanzo kikuu cha ugonjwa huo wa kuoza kitako.
TIBA
Ondoa matunda yote yaliyo athirika halafu anza kufuata na kuzingatia ratiba ya umwagiliaji wa shamba lako.
(Hii nimeinyaka kutoka fb wafanyakazi wa kilimo Mifugo na uvuvi na kuikarabati kidogo na kuirusha kwani ni wengi wanalima nyanya na hasa na kuwaona wanamwagilia maji kiubabaishaji tu).
Ondoa matunda yote yaliyo athirika halafu anza kufuata na kuzingatia ratiba ya umwagiliaji wa shamba lako.
(Hii nimeinyaka kutoka fb wafanyakazi wa kilimo Mifugo na uvuvi na kuikarabati kidogo na kuirusha kwani ni wengi wanalima nyanya na hasa na kuwaona wanamwagilia maji kiubabaishaji tu).
Wednesday, September 14, 2016
Bus la Yutong la Wachina
Hili ni bus la Yutong la kutoka Uchina. Utawapenda tu. Wachina ni wazuri kwa teknolojia. Hutengeza kuteka matakwa ya mdau. Hapa Tanzania kwa sasa naweza kusema kuwa asilimia 80 ya mabus ni ya Kichina. Inasemekana ni bei poa ukilinganisha na mabus aina ya Scania au Marcopolo. Kingine wanachofanya Wachina ni kuongeza thamani ya bidhaa. Ukipanda mabus yao yalivyorembwa na kuwekewa vikorombwezo vingine hakika hutoacha kulipanda tena. Sisi tutaanza lini kuunda mabus yetu?
Haya ni machenza kutoka Matombo - Morogoro
Machungwa na machenza ya Matombo, Morogoro ni matamu sana. Tatizo wafanyabiashara wameingilia kati biashara hii na kuyauza machenza na machungwa wakati bado hayajafikia kukomaa kibailojia (Yanakomaa yakiwa mtini). Kibaya zaidi huchanganya machungwa au machenza mazuri na mabaya. Mlaji akibahatika hula chenza tamu na ikiwa hana bahati unaweza kula chenza chungu. Hii ni kuharibu biashara na umaarufu wa machungwa au machenza ya nyumbani Matombo. Kwa kawaida machungwa huanza kuvunwa kuanzia mwezi wa Machi hadi Mei.
Subscribe to:
Posts (Atom)