Tuesday, October 3, 2017
Shukrani iliyoniliza
Ilikuwa zaidi ya shukrani. Pale Dada Slyvia Daulinge, mtoto kitinda mimba wa Bw & Bi. Nestory Daulinge alipotoa shukrani kwa wote waliomhangaikia marehemu Baba yao Mzee Nestory Daulinge hadi kuzikwa kwake. Ilituliza wengi hata kama ni kimyakimya. Hii ilikuwa kabla ya mazishi tarehe 5 Septemba 2017 kule Matombo, Morogoro
Tuesday, August 15, 2017
Prof. Ndalichako na maendeleo ya Elimu Mkuranga
Jiwe la Msingi la moja ya majengo ya Shule ya Sekondari Nasibugani iliyopo wilayani Mkuranga likiwekwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Joyce Nadilichako. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Sanga na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe.Abdalah Ulega.Shule ya Nasibugani sasa ni mpaka kidato cha sita. Hakika, wakati viwanda vinazidi kujengwa wilayani Mkuranga, elimu lazima iboreshwe kwani viwanda vinahitaji wataalamu.
Subscribe to:
Posts (Atom)