Tuesday, August 15, 2017

Huyu ndiye Haruna Niyonzima-Fundi

Haruna Niyonzima-Fundi amekwenda kucheza mpira Simba Sports Club. Asante Niyonzima.Hakika umeanza kuonyesha vitu vyako.

Mluguru katikati ya Wazungu

Fr. Kunambi Gega akiwa amezingirwa na wazungu huko Italia

Dafu la kwanza nyumbani Kisemvule Mkuranga


Kisemvule nyumbani kwetu raha sana. Ona mke wangu na mwanetu Sisty wakikata kiu kwa maji ya dafu. Hii ilikuwa mwaka 2012 tulipoanza kuonjam dafu la kwanza kwa minazi tuliyoipanda.

Prof. Ndalichako na maendeleo ya Elimu Mkuranga

Jiwe la Msingi la moja ya majengo ya Shule ya Sekondari Nasibugani iliyopo wilayani Mkuranga likiwekwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Joyce Nadilichako. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Sanga na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  Mhe.Abdalah Ulega.Shule ya Nasibugani sasa ni mpaka kidato cha sita. Hakika, wakati viwanda vinazidi kujengwa wilayani Mkuranga, elimu  lazima iboreshwe kwani viwanda vinahitaji wataalamu.