Tuesday, July 5, 2011

EKARISTI TAKATIFU

Tarehe 26/6/2011 Wakatoliki waliazimisha sikukuu ya Ekaristi Takatifu. Pichani chombo kinachong'aa ni 'MONSTRANCE' kule kwetu Matombo tunaiita 'Monstrandi'

Friday, July 1, 2011

Taasisi ya Utafiti Kizimbani -Zanzibar




Hapa ndipo Makao makuu.Utafiti wa Mpunga - NERICA unaendelea.Na mahojiano yalifanyika pia ofisini kwa Mkurugenzi wa Taasisi - Dr. Salehe Haji

Mwanakwerekwe


Na hapa ndipo Mwanakwerekwe. Ni mahali maarufu Zanzibar.

Na hizi amejenga mtoto wa Karume


Mhe. Amani Abeid Karume alifuata nyayo za baba yake na kujenga flats hizi.

Makutano ya Legezamwendo na Bubu


Hapa barabara mbili zinakutana. Moja ni Legezamwendo na nyingine ni Bububu. Ukienda Kizimbani sharti upite hapa.

Bahari imetulia


Bahari ikitulia unaweza hata kufanya kazi na Laptop!

Bahari ikichafuka!



Bahari ikchafuka. Abiria chomboni ni kama uonavyo.

Flats alizojenga Sheikh Abeid Amani Karume

Majengo haya ni kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume. Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la mapinduzi Zanzibar hapa ni Michenzani-Unguja.

Wanafurahia boat

Kama hakuna mawambi ni raha kusafiri na boat.

Hiyo ndiyo bahari ya Hindi

Bahari ya hindi imetulia tuli!

Ndani ya boat

Nje ya boat juu kwa mbele.

Nje ya Boat Je?

Azam Marine


Unaposafiri kwenda Unguja kwa kutumia boat. Boat yenye uhakika na raha na Azam Marine na hii ndiyo ofisi yao - Dar

Tunamuandaa kuwa Miss Tanzania


Dada Irine Kibena tunamuandaa kuwa mlimbwemde wa Tanzania miaka michache ijayo. Angalia pozi yake akiwa kwao Kola, Morogoro.

Kwetu sisi ndizi ni kitafunwa tu


Kwa wenyeji wa Morogoro kawaida ndizi huliwa zikiwa mbivu au kama vitafunwa (kwa kunywea na chai). Huwezi ukapikiwa ndizi halafua ukasema kuwa leo nimekula chakula. Hata kama watachanganya na nyama bado ni vitafunwa tu. Chakula cha heshima kwetu ni wali! Angalia mikungu ya ndizi nyuma ya nyumba - Kola, Morogoro mjini.

Pikipiki inapovaa 'helmet'



Kwa kawaida waendesha pikipiki wanatakiwa kuvaa helmet (kofia za kujikinga na kichwa) waendeshapo vyombo hivyo. Banzi wa Moro ilinyaka scene hii pale Kola-Morogoro wakati mwendesha pikipiki alipodondosha helmet na baadaye kuifunga nyuma ya pikipiki. Angalia picha pmbili ya juu na kushoto.

Malongoza mtaalamu wa kuandaa chakula cha shughuli - Morogoro






Mpishi Malongoza wa Morogoro ni maarufu kwa kupika chakula cha shughuli. Hana papala na anajali muda. Anatayarisha chakula kwa umakini mkubwa hatua kwa hatua na ukimuuliza atakupa sababu. Nilishangaa nipoona anamwagia mafuta sufuria la kupikia. Akanieleza kuwa sababu yake iwe rahisi wakati wa kuosha. Lakini sikumuelewa pale aliponieleza kuwa anamwaga chumvi pembeni ya jiko ili chakula kiwe kitamu! Huyu ndiye Malangoza mtaalamu wa maakuli -Morogoro.

Kuna wazungu na Africana pia


Ndiyo kwenye familia yetu kuna sisi weusi na wenzetu weupe lakini sote tumetoka kibanda kimoja Africana! Pichani Banzi na mtoto wa mjomba Beatus nyumbani Morogoro.

Mkude wa Morogoro


Huyu ni ndugu 'mtoto' wangu anaitwa Mkude. Kwa kuzingatia taratibu za mila za Kiluguru mimi ni Baba Mkude. Lakini mimi ni Banzi au Jaka, Zinga na dada zangu wanaitwa akina Kimbiki ni watoto wa Wambiki. Watoto wangu wanastahili kuitwa akina Mkude, Mizambwa, Mdoti, Midahuli.. (wanaume) na ikiwa mwanamke anaitwa Mwenda au Mlamwenda. Kwa hiyo huyo ni ndugu yangu na ni mtoto wangu. Morogoro akina Mkude,Banzi, Mloka, Mwenda, Mbiki,Mbena, Luanda, Mtonga tukiwa nyumbani tunatumia jina la kwanza kutotofautisha!

Familia ya Morogoro


Familia yangu ni kubwa sana. Hapa ni Morogoro- Kola, nyumbani kwa Babu yangu-Unaowaona ni dada zangu na wadogo zangu watoto wa wajomba zangu. Tulikuwa kwenye 40 ya mama mdogo na dada.