Monday, October 3, 2011
Maji ya Baraka
Paroko Sowa wa Parokia ya Matombo ndiye aliyeendesha ibada takatifu. Pichani anaonekana akinyunyiza maji ya baraka.
Binti akimlilia baba yake
Ndiyo kwanza amewasili kutoka Songea anakoishi. Felista, mtoto wa nne wa marehemu Jerome Hugo akimlilia baba yake mbele ya jeneza. Majonzi, majonzi, majonzi.
Jeneza linasubiri kuingizwa kanisani
Kanisa la mtakatifu Paul-Parokia ya Matombo, jimbo la Morogoro ndimo ilimofanyika ibada ya misa takatifu ya marehemu Jerome Hugo. Kanisa hili ndilo marehemu alilolitumikia kwa miaka mingi katika maisha yake. Amebatizwa ndani ya kanisa hili, amepata ekaristi takatifu ndani ya kanisa hili na Kipaimara pia. Amefunga ndoa yake ndani ya kanisa hili na kuagwa ndani ya kanisa hili. TUMSIFU YESU KRISTU.
Let us Talk Mathematics
Ninawakumbusha Africana
Kutoka Matombo hadi Kisemvule
Tulizungumza sana tukikumbuka enzi zetu kule nyumbani Matombo. Mashindano ya sabasaba ambapo yeye alikuwa bingwa wa kukimbia mita 100 nafikiri ingekuwa kwa wenzetu hivi sasa angefananishwa na H.BOIT.Stori za 'solono' (kupiga mbizi) mtoni mfizigo hazikukosekana pia. Tuliwakumbuka wazee maarufu, walimu waliotufundisha hata, wanafunzi watukutu walevi wa kijijini waliokuwa wanawasumbua, sikukuu za kanisa hasa ekaristi kuzunguka kijiji cha Kiswira na hata wasichana watanashati waliotetemesha pale kijijini enzi hizo wengine hawapo tena nasi duniani.
Kade ndani ya Kisemvule
September haikuwa nzuri kwangu
Friday, August 19, 2011
Banzi wa Moro
Tuesday, August 16, 2011
Lugaluga wanalima na kuuza
Kama tunataka wakulima wetu wasinyonywe na wakione kilimo kinalipa wazalishe na kuuza wenyewe huku wakimiliki zana za usalishaji na ikiwezekana na miundo mbinu. Lugaluga wameshaanza kufanya hivyo. Kinachowakwimisha ni miundo mbinu ya umwagiliaji na barabara safi za mashambani. Hilo linatakiwa kufanyiwa kazi.
Lugaluga walikuwepo 8/8
LugaLuga Agricultural Marketing and Cooperative Society kulikuwepo kwenye maonyesho ya wakulima ya mwaka 2011 kwenye uwanja wa maonyesho-Morogoro. Walioneysha zana wanazotumia (matrekta madogo na makubwa) ambayo wanamiliki wanachama kupitia Ushirika wao. Bidhaa wanazozalisha- Mpunga, alizeti na mahindi. Hao ndiyo Lugaluga waliojizatiti kuondoa umaskini kupatia Ushirika.
Wakorea wanataka kuibadilisha Pangawe
Katika muda wa miaka mitano ijayo, Wakorea wanataka kukibadilisha kijiji cha Pangawe kilichopo wilaya ya Morogoro vijijini kuoenakana cha kisasa zaidi kikiwa na miundombinu ya umwagiliaji, barabara za mashambani, shule bora ya msingi, maji safi huduma ya afya, umeme na huduma nyingine. Tusubiri tuone. Kazi hiyo inafanywa na KOICA-Korea Interanational Cooperation Agency.
Subscribe to:
Posts (Atom)
