Saturday, May 5, 2012
Walikuwepo
Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika walikuwepo Magadu Leaders' Club siku ya Send off party ya Bi Adela Ng'atigwa mfanyakazi mwenzao.
Friday, May 4, 2012
Keki kutoka Mgeta-Morogoro
Amini usiamini, keki hii imetengenezwa na wataalamu kutoka Mgeta-Morogoro. Ina mchanganyiko wa magimbi, viazi, njegere, muhogo, ndizi, na ngano ndiyo aliyoikata Bi Adela Ng'atigwa siku ya kuagwa kwake pale Magadu Leaders Club Morogoro.
Magadu Leaders' Club
Mabadiliko Morogoro! Siku hizi shughuli zote kali (harusi, send off parties) katika mji wa Morogoro hufanyika katika viwanja vya Magadu Leaders' Club vilivyoko Mzinga-Morogoro hapa pametulia. Uwanja umezungukwa na milima na mandhari ya kuvutia. Hapa ndipo alipoagwa dada Adela Ng'atigwa hivi karibuni.
Monday, April 30, 2012
Huko ndiko kuagwa
Ukiona sanduku, ujue safari imeiva. Pichani Bw. George Ng'atigwa, akimuaga dada yake Adela Nga'tigwa wakati alipowakabidhi rasmi ukoo wa Kavia (mume mtarajiwa) katika ukumbi wa Magadu ulipo ndani ya Kambi ya Jeshi la Wananchi-Mzinga siku ya tarehe 28/4/2012.
Bw na Bibi Ng'atigwa
Hawa siyo maharusi bali wazazi wa Bi Adela Ng'atigwa Bw. Na Bibi Ng'atigwa wakiwa pamoja kwenye sherehe ya kumuaga binti yao iliyofanyika katika ukumbi wa Magadu Leaders Club mjini Morogoro tarehe 28/4/2012
Dada Adela Ng'atigwa akiingia ukumbini
Dada Adela Nga'tigwa akiwa na mpambe wake Imaculata Banzi wakiingia ukumbini Magadu Leaders Club Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 28/4/2012 tayari kwa sherehe ya sendoff.
Tuesday, April 24, 2012
Jirani wa Chuo cha Nelson Mandela -Arusha
Jirani huyu amejenga karibu kabisa na Chuo cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.Ni nyumba nzuri na ya kisasa huenda atapata wateja!
Uanikaji nguo maghorofani
Ni tabia iliyozoeleka na baadhi yetu kuanika nguo ovyo ovyo. Juma la jana Banzi wa Moro alifanikiwa kunasa jengo hili likiwa na nguo zilizoanikwa barazani. Hili ni jengo la ghorofa, ni kubwa na zuri lililoko kati kati ya jiji la Dar Es Salaam. Hivi kweli hii ni tabia nzuri ya kuanika kila kitu nje? Huu nao ni uchafu.
Uvunaji wa maji ya mvua
Shule ya Msingi Kisemvule iliyoko wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imebahatika kuwa na mradi wa uvunaji maji. Maji haya hutumika kwa shughuli mbalimbali yanafaa pia kwa kunywa ila inashauriwa kuwa ni vizuri kuyachemsha kabla ya kunywa.
Ukitaka kwenda Kigogo
Juzi nilitembelea maeneo ya Kigogo. Barabara ya Kigogo kwa sasa ni nzuri na mabus yanayotumia njia hiyo ni mazuri na makubwa. Pichani ni njiapanda ya Kigogo. Hapa ndipo unapoweza kuunganisha mabus ya kwenda Kigogo, Mburahati na hata Manzese.
Monday, April 23, 2012
New Kisemvule Butchery
Mwekezaji amewahi Kisemvule. Sasa tuna duka la nyama. Zamani ilitubidi kupata kitoweo pale Vikindu au Mbagala. Sasa hivi nyama wakati wowote. Haya ni maendeleo yanayokuja kwa kasi katika kijiji ninachoishi, Kisemvule-Mkuranga.
Friday, April 20, 2012
Doreen Nyanjura

Msichana Doreen Nyanjura wa Uganda hivi karibuni alitawala vyombo vya habari vya Uganda na Afrika Mashariki baada ya kukamatwa na kutiwa ndani kwa sababu ya kuandika kitabu kiitwacho "Is it The Fundamental Change?"
Doreen ana umri wa miaka 22 na ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Sifahamu kilichoondikwa ndani ya kitabu hicho kwani sijakisoma. Lakini kutokana na makala ya Padri Privatus Karugendo (Raia Mwema Aprili 18- 24,2012 baadhi ya nukuu ambazo zimenisisimua kwenye kitabu hicho kama alivyonukuu Karugendo ni "Maisha yanaelekea mwishoni, siku tunapokaa kimya kwa mambo ya msingi" na "Dunia inateseka, si kwasababu ya vurugu na maasi ya watu wabaya, bali ni kwa sababu ya ukimya wa watu wema".
Nimesisimka kuona msichana wa miaka 22 kuandika ambacho kinaanza kuleta changamoto! Hongera sana Doreen Nyanjura na pole kwa kutiwa kolokoloni!
Tunawachia nini watoto hawa?
Vituko vya Iddi Amin Dadah
Wednesday, April 18, 2012
Ah, magogo tena!
DARLIVE yetu
Uchafu karibu na KTM ya zamani
Huu si ustaarabu
Subscribe to:
Posts (Atom)

