Monday, June 4, 2012

Matokeo ya kutomuaga mkeo

Baadhi ya wanaume wanatatabia yakutoka majumbani kwa bila kuwaaga wake zao. Tabia hii huwachukiza sana wanawake, hasira wanazokuwa nazo kwa wale wasiokuwa na busara hufanyiwa alichofanyiwa afande 'kulakula' (Picha kwa hisani ya Cartoonist NOAH YONGOLO)

Friday, June 1, 2012

Wanamwita 'Mwabeshi'

Huyu anaitwa Shabani. Lakini hapa kijijini kwetu Kisemvule ni maarufu sana kwa jina la 'Mwabeshi' likiwa na maana ni mtu kutoka Ethiopia! Kwa maelezo yake mwenyewe ni kwamba, jina hilo amelipata hapo Kisemvule kwa kuwa alikuwa anafanya kazi kwa mtu aliyefananishwa na waethiopia lakini kumbe alikuwa ni mchangayiko wa damu ya kihindi na watu kutoka Tabora. Shabani kazi yake ni biashara ndogondogo hasa matunda kwa kuzingatia msimu kuna wakati anauza embe, kuna wakati mwingine machungwa. Hapa alikuwa anauza mahindi ya kuchoma. Huyo ndiye Shabani 'Mwabeshi' ameoa na ana watoto watatu

Nyumba hadi nyumba

Ndivyo inavyofanya kazi Jumuiya Ndogondogo za Kikristu. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mgaya wa Soweto-Vikindu. Jumuiya Ndogondogo zinaimarisha upendo, kutambuana na pia hutumika kulieneza Neno la Mungu.Jumuiya Ndogondogo ikitumiwa vizuri huleta maendeleo.

Shemeji zangu

Wote wawili ni akina Binti Pembe, hawa ni shemeji zangu msiulize maswali mengi - period!

Alama za kiwanja

Unaponunua viwanja vizsivyopimwa ni vizuri kuweka alama za kudumu na zinazoeleweka ili kuepusha mgangano wa mipaka ya viwanja hapo baadaye

Na hii ndiyo misemo ya Waluguru

1. 'Bita ako si miyage' - Si vizuri kuacha mtu akafanya kitu kivyake vyake 2. 'Chikwili ng'awingagwa na Seko'- Huwezi kumfukuza mnyama anayeitwa 'Chikwili' huku ukiwa unacheka 3. 'Chimbulumbulu kokwila mti gwagumanyile'- Mnyama anayeitwa Chimbulumbulu hupanda mti anaoufahamu. Tafakari kuhusu semi hizi za Kiluguru!

Miundo Mbinu ya Umwagiliaji

Kuendesha kilimo cha umwagiliaji inahitaji miundo mbinu ya uhakika
Banio la Umwagiliaji liloloko mto wa Ruaha- Ruaha Mbuyuni, Kilolo.
Banio la umwagiliaji maji kijiji cha Itimba
Mfereji wa umwagiliaji unaotunzwa vizuri
Baada ya kuvuna mahindi, shamba limepandwa maharage (Kijijini Itimba, Utengule-Mbeya vijijini). Hii inawezekana kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Hapa ni Umalila-Mbeya

Isangati Agricultural Development Organization (IADO) kijijini Santilya, Umalila, Mbeya Vijijini. AIDO ni Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) linalofanya kazi katika wilaya ya Mbeya Vijijini. AIDO wamewezeshwa na ASDP kupitia DADPs katika kuleta mageuzi ya kilimo wilayani Mbeya. Baadhi ya Miradi ya Kilimo inayosimamiwa na IADO ni:- Upandaji wa Miche Bora ya Kahawa, Ufugaji wa Ng'ombe wa Maziwa, Ufugaji bora wa Nguruwe, Uboreshaji wa Kuku wa Asili, Ufugaji wa samaki. Aidha IADO hutoa mafunzo ya Utawala Bora yanayowawezesha wanavijiji kufuatilia matumizi ya fedha za umma ngazi ya kijiji.
Uboreshaji wa kuku wa asili
Nje ya Ofisi ya IADO
Tunapata taarifa ya IADO kutoka kwa uongozi wa shirika.
Ukaguzi wa banda la machinjio kijijini Santilya, Mbeya vijijini.

Thursday, May 31, 2012

Hivi ndivyo chai inavyooteshwa

Wengi wetu tumeshakunywa chai lakini ni wachache sana wameshauona mmea halisi wa chai. Pichani ni kitalu cha kuotesha mchai kilichopo kijijini Kidabaga, wilaya ya Kilolo, mkoa wa Iringa.

Tunapata taarifa ya miradi ya kilimo kijijini

Unapoingia kwenye ofisi ya kijiji cha Msosa unakuta matangazo mbalimbali ukutani ambayo yanatosha kukupa hali halisi ya kijiji hicho. Hata hivyo ilibidi tuzungumze na baadhi ya wakulima wa kijiji cha Msosa wakiongozwa na mwenyekiti wao.

Kilimo cha Vitunguu kijijini Msosa

Tulipotembelea kijiji cha Masosa kilichopo katika wilaya ya Kilolo tulishuhudia bonde kubwa linalolimwa vitungu aaina ya Red Bombay kwa njia ya umwagiliaji. Kilimo cha vitunguu kimeboresha maisha ya wakazi wa Msosa.Nyumba za kisasa zimeanza kujengwa na vijana zaidi ya 10 wamerudi kijijini kutoka mijini kushiriki katika shughuli za kilimo kwa muda wa miezi 3 mkulima ana uhakika wa kupata shilingi 350,000 kwa eneo la robo eka tu.
Shamba la vitunguu kijijini Msosa.
Baada ya mazungumzo na wanavikundi kijijini ilibidi tufike shambani

Mradi wa Ufugaji wa Kuku wa asili-Msosa

Moja ya vijiji vinavyopiga hatua ya kasi katika kilimo ni kijiji cha Msosa kilichoko wilaya ya Kilolo, mkoa Iringa. Kijiji hiki kiko karibu sana na barabara kuu ya Tanzania - Zambia sehemu maarufu ya Ruaha Mbuyuni. Licha ya wakazi wake kujikita katika kilimo cha vitunguu, sasa wameanzisha mradi mwingine wa ufugaji wa kuku wa asili. Mwaka 2010 kikundi kijulikacha JIPE MOYO kiliwezeshwa jumla ya shilingi 1,900,000 ambazo ziliwezesha kikundi kujenga banda la kuku na kuku wa kufuga na wanakikundi walichangia jumla ya shilingi 180,000/=. Kikundi kina jumla ya wanachama 21 wengi wao ni wanawake (17). Mradi huu kwa sasa hutumika kama shamba darasa la ufugaji bora wa kuku. Lengo ni kuboresha kuku wa asili. Wakulima hufundishwa lishe ya kuku, tiba, ujenzi wa banda bora na jinsi kuweka kumbukumbu za ufugaji ili kuweza kufuga kwa faida.

Wednesday, May 30, 2012

Skimu ya umwagiliaji kijiji cha Mkungugu

Ujenzi wa Bwawa la Mkungugu, lilipo katika kijiji cha Mkungugu wilaya ya Iringa Vijijini lilianza kujengwa msimu wa mwaka 2009/10 chini ya Progamu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) lengo ni kukusanya maji ya mvua kwa lengo la kuendesha kilimo cha umwagiliaji.Litakapokamilika, bwawa hili litakuwa na uwezo wa kumwagilia hekta zipatazo 80.Mazao yanayatarajiwa kumwagiliwa ni yale ya bustani pamoja na mahindi. Banzi wa Moro imeshuhudia sehemu kubwa ya bwawa hilo likiwa limekamilika isipokuwa miundo muhimu ya umwagiliaji haijatengmeaa kama vile matanki, pump na mifereji ya umwagiliaji.

Shule ya Sekondari ya Kata - Magozi, Iringa vijijini

Kuongezeka kwa kipato cha wanakijiji wa Magozi kumewezesha kuchangia shule ya Sekondari ya Kata ya Magozi. Shule hii ina kisima cha maji, umeme wa solar, na mabweni ya kulala wanafunzi.

ASDP imeleta mabadiliko kijiji cha Magozi

Kijiji kina 'powertillers' zipatazo 10, vijana wameanza kurudi kijijini kutoka mjini na kushughulika na kilimo cha umwagiliaji
Nyumba bora za kisasa zimeanza kujengwa

Skimu ya umwagiliaji kijiji cha Magozi-Iringa Vijijini

Miaka 21 iliyopita kijiji cha Magozi, wilaya ya Iringa vijijini kila mwaka kilikuwa kikipata msaada wa chakula kutoka na hali ya ukame wa maeneo hayo. Kupitia 'Disitrict Agricultural Develpment Plan (DADP) kijiji kimejenga mfereji wa umwagiliaji kuanzia mwaka 2007 na sasa wanazalisha mpunga kwa wingi. Kwa wastani mkulima sasa anaweza kuvuna magunia 20 ya mpunga kwa eka moja.

Mbwa wetu 'Kijenge'

Mbwa wetu aitwaye 'Kijenge' tunampenda sana. Hubaka kwa nguvu kuashiria tukio hasa nyakati za usiku, anatulinda. Kijenge hula ugali na dagaa la kuchemsha, huogeshwa mara moja kwa wiki kujikinga na kupe. Hunywesha dawa za minyoo angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu. Hivi ndivyo tunavyomtunza 'Kijenge.'Lakini kuna kundi la watu wanaiba mbwa kijini kwetu Kisemvule. Wengine wanasema wanawauzia Wachina kwa bei ya shilingi 40,000 kwa mbwa mmoja. Sina uhakika na hilo.

SHEREHE YA KUMPONGEZA DOLORES

MC alikuwa ni Maria 'Bonge' kutoka DADAZ
Dolorose Kamsopi a.k.a EKA akilishwa keki na shangazi yake Hellena Mdimi
Ni zamu ya Baba Joseph Kamsopi Mdimi kulishwa keki na bintiye
Mama akilishwa keki na mwanawe
Babu (Mzee C.M.Mdimi)alilishwa keki
Tulisakata miondoko ya 'gospel songs'
Mjomba Msechu alifungua champaigne
Keki ilikatwa

Dolorose apata Kipaimara

Siku ya tarehe 25/5/2012 itakuwa ya ukumbusho mkubwa kwa Bi Dolorose J.Kamsopi Mdimi a.k.a EKA kwa kupata kipaimara ambayo ni moja ya Skaramenti muhimu katika Kanisa Katoliki. Kipaimara kinakupa ujasiri kupitia Roho Mtakatifu kuweza kueneza neno la Mungu. HONGERA SANA DOLOROSE.

Keki jamvini

Na hii ndiyo keki ya Catherine ya miaka 14