Wednesday, June 27, 2012

Sayansi ipo kituo cha Utafiti Mikocheni

Sayansi ipo Mikocheni.Hii ni maabara bora kabisa ya baiteknolojia hapa nchini chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.Kwa sasa watafiti katika kituo hiki wanaendelea na tafiti za kupata mbegu bora za muhogo zinazohimili magonjwa hatari ya muhogo.

Karibuni LRC-Tanga

Ndivyo anavyosema Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo- Dr. Julius Bwire. Hapa tulipta maelezo ya shughuli zilizofanyika kwa mwaka 2011/12 kuanzia utafiti, ukarabati wa majengo, ununuzi wa vifaa, na mafunzo. Hakika LRC kwa kipindi kifupi imebadilika kabisa kuna ubunifu mkubwa wa shughuli za utafiti na miundo mbinu imeanza kukarabatiwa.

Tanga-Mombasa ni kuteleza!

Barabara ya kutoka Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kwa kiasi kikubwa imekamilika hivi ndivyo alivyoikuta Banzi wa Moro akiwa kwenye shughuli za kikazi wilayani Mkinga mkoa wa Tanga. Tanga-Mombasa sasa ni kuteleza tu!

Utafiti wa mbolea kwenye mahindi

Utafiti huu unafanyika wilayani Handeni kwa ushirikiano wa wakulima na watafiti wa kituo cha utafiti cha Mlingano kilichoko mkoani Tanga. Hapa tulipata maelezo kutoka kwa wakulima kuwa mbolea ya DAP imeonyesha matokeo mazuri ukilinganisha na mbolea nyingine. Jaribio halijafikia tamati. Watafiti watatuandikia kuhusu jaribio hili pindi watakapomaliza utafiti wao.

Nyumbani kwa mkulima Handeni

Hivi karibuni tulikuwa tunatathmini shughuli za utafiti kanda ya mashariki hususan mikoa ya Tanga na Pwani.Pichani tupo kijijini Magamba wilayani Handeni mkoa wa Tanga nyumbani kwa mkulima. Nyumba ni bora,anafuga mbuzi na kuku pia hulima muhogo na mahindi kwa chakula na biashara. Tunataka wakulima wetu angalau wafikie hatua hii.Vijana wataacha kukimbilia mijini.

Utafiti shambani kwa mkulima - Muheza

Ndivyo wafanyavyo watafiti wa kituo cha Utafiti Mlingano Tanga (soma bango) wakulima na watafiti wanashiriki kwa pamoja katika utafiti na kutoa tathmini yao kutokana na walichokiona

WASIFU WA DR.GREGORY P.C.MLUGE

Picha ya ukumbusho wa Dr. Gregory P.C.Mluge (katikati)enzi za uhai wake akiwa na mkewe Restituta (wa kwanza kushoto) wakitambulishwa na mpwa wao Inno Banzi wakati wa sherehe za komunio ya kwanza ya watoto wake nyumbani kwao Kisemvule-Pwani
Dr. Gregory Paul Constance Mluge alizaliwa tarehe 12 Machi 1937,wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambako baba yake Mwalimu Paul Lugonzo alikuwa anafundisha. Dr. Gregory Mluge alizaliwa katika familia ya Bw.Paul Lugonzo na Bibi Annastazia Hugo Mlachuma. Alikuwa mtoto wa pili kwenye familia ya watoto saba wakiwemo wanawake watano na wanaume wawili. Kati ya hao Sr. Philomena, Janeth, Rosemary na Frederick wametangulia mbele ya haki. Waliobaki ni Beatrice na Dolores. Marehemu Dr.Mluge alianza masomo yake ya msingi huko Bagamoyo na baadaye familia ilirudi Matombo, Kiswira ambako marehemu Paul Lugonzo aliendelea kufundisha katika Shule ya MsingiMatombo. Dr. Mluge alisoma shule za msingi Matombo na Bigwa. Aliendelea na masomo ya sekondari shule ya wavulana Tabora na baadaye shule ya sekondari maarufu hapa nchini ya Pugu. Dr. Mluge alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere , Kampala Uganda kutoka mwaka 1960 hadi 1965 ambako alipata shahada yake ya kwanza ya udaktari. Alianza kazi ya udaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam. Baada ya mwaka mmoja alihamishiwa hospitali ya mkoa Tabora. Baada ya muda aliteuliwa kuwa daktari mkuu wa wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora mwaka 1967. Hapo Nzega alikutana na afisa wa wauguzi ambaye alimpenda kwa jina Restituta Emmanuel Assenga wa Rombo Mashati mkoani Kilimanjaro ambaye alimrushia ndoana ya huba naye Restituta akanasa. Ukawa mwanzo wa uchumba na hatimaye kufunga ndoa. Dr. Mluge alipewa ‘scholarship’ ya kwenda Uingereza kuendelea na masomo ya udaktari bingwa mwaka 1969. Huko Uingereza alisomea diploma ya ‘Tropical Public Health’, katika chuo cha London School of Tropical Medicine na kupata stashahada. Mwaka 1971 huko Uingereza alipokea tena stashahada ya ‘Tropical medicine and Hygiene’. Mwaka 1972 hadi 1973 alisoma na kuhitimu shahada ya uzamili ya ‘Occupational medicine’ kutoka chuo kikuu cha London. Mwaka huo huo pia alisomea na kupokea shahada ya ‘Industrial health’ na mwaka 1973 hadi 1975 alipata shahada ya tatu ya medicine na cheo cha MRCP kutoka chuo kikuu cha London. Alifanya kazi katika hospitali bingwa mbalimbali nchini Uingereza kuanzia mwaka 1975 hadi 1980. Alipendwa sana na madaktari wenzake na wagonjwa wake wote. Mtoto wake pekee Janeth Mluge Schoemaeiker alizaliwa mwaka 1978. Mwaka 1980 Dr. Mluge aliajiriwa kama Proffessor wa udaktari na afya ya Jamii na mwalimu wa madaktari wadogo katika Chuo Kikuu cha Jeddah nchini Saudi Arabia. Mwaka 1989 alirudi Tanzania kufanya kazi zake mwenyewe, lakini mwaka huo huo aliombwa na serikali ya Saudi Arabia kurudi tena na kuendelea na kazi ya Proffessor huko. Alifanya kazi huko pamoja na mke wake Restituta ambaye alikuwa Mkurugenzi huko Saudi Arabia. Familia ya Dr. Gregory Mluge iliamua kurudi Tanzania mwaka 2006. Dr. Gregory Mluge alikuwa ni mtu aliyependa sana watu wote, mkarimu sana, aliyewasaidia watu wengi katika nyanja zote za maisha ikiwemo kitabibu, kielimu, kiushauri na mengine mengi ambayo nina imani itahitaji muda mwingi kuyataja yote. Dr. Mluge alikuwa ni mtu mwenye msimamo wa kweli. Alikuwa mkweli, mvumilivu sana, daktari mzuri na mpole sana. Na kwa hayo yote tunasema AHSANTE SANA. Dr. Mluge alikuwa mpenzi wa kilimo,ujenzi,na magari lakini ‘hobby’ yake kubwa ilikuwa muziki, na katika hilo alikuwa bingwa wa kupiga kinanda. Marehemu Dr. Mluge ameacha mjane, mtoto mmoja ,wajukuu wawili na dada wawili. RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA! NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI….AMINA.

Saturday, June 16, 2012

Maombolezo ya Dr. G.P.Mluge

Suzana Banzi (Mwanandota) na Aunt Ceci katika maombolezo makaburini - Matombo

Paul Wilbart

Uncle Paul Wilbart (wa kwanza kushoto) nguzo ya Waluguru anauwezo wa kumudu pilika za misiba. Tulikuwa naye kuanzia Dar hadi Matombo

Mama Mloka

Mama P.Mloka (katikati) alihakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa kuanzia Dar hadi Matombo kwenye mazishi ya Dr.G.P.Mluge. Wa kwanza kushoto ni Da Eliza Semsela na kulia ni Mama Beatrice P.Mhango

Vijana wa kazi

Kutoka kushoto Macarios Banzi, 'Supa' (Dereva wa Dr. G.P.Mluge) na Diku Wilbart

Kwetu Matombo

Wajukuu wa marehemu Marco na Lulu

Waratibu wa mazishi Dr. P.Mluge

Mzee Mangengesa Mdimi Bw.Innocent J.Banzi

Mapadri walioendesha ibada ya mazishi ya Dr. P.Mluge

Pdr.Francis Kolongo Padri Venance Jakka wa Ruaha (katikati ya watumishi) Padri Mogella (Paroko wa Matombo) Padri Msafiri kutoka Moshi (mwenye joho anayekomunisha)

Thursday, June 14, 2012

Mipango ya mazishi nyumbani Matombo

Watoto na wajukuu kanisani

Mtoto wa pekee wa Marehemu Bi. Janet G.Mluge na mumewe Tom wakiwa na watoto wao katika Ibada ya misa Takatifu Kanisani Mbezi Beach, Dar Es Salaam siku ya tarehe 10/6/2012 (wa kwanza kushoto)