Tuesday, July 31, 2012
Uncle God Kyando Luhungu
Tarehe 28/7/2012 kwetu Kisemvule tulitembelewa na mgeni maarufu si mwingine ni uncle God Kyando Luhungu anayeishi Kurasini jijini Dar. God, ni mtoto wa dada yangu marehemu Averina Constantine Gega (Mrs A.Luhungu) a.k.a Dada Ave aliyefariki siku chache baada ya kuzaliwa God.God sasa yuko darasa la sita. Ingawa amevalia T-shirt ya kijani (pichani) yeye ni mpenzi mkubwa wa klabu ya Simba (mnyama) kwa hapa nyumbani na ni shabiki wa Chelsea huku majuu!.Angalia jinsi anavyofuatilia matangazo ya mechi ya Yanga na Azam iliyochezwa tarehe 28/7/2012 kupitia kiredio kidogo ambapo Yanga iliibuka mshindi na kunyakua Kombe la Kagame kwa kuibamiza Azam 2-0. Uncle God pamoja na mimi mjomba wake (Mwanachama wa Simba) hatukufurahia hata kidogo ushindi huo wa Yanga!
Dafu la Kwanza
Tupo Kisemvule takribani miaka minane sasa. Tumeanza kuonja matunda ya bustani yetu. Na hili ndilo dafu la kwanza.Mnazi ni wa Kipemba'
Na huyu alimalizia kwa kulikomba ina maana lilikuwa tamu kwelikweli!
Monday, July 30, 2012
Happy Birthday dada Doreen
Jana tarehe 29/7/2012 ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa dada Doreen (Mrs Dr.Doreen Moshi)Mumewe Prof.M.Moshi alimwandalia ndafu.
Hii ndiyo keki yake ya Birthday
Happy Birthday Doreen! Ndivyo anavyosema Prof. Moshi wakati alipokuwa akimlisha ndafu mkewe.
TFRA Mkoani Ruvuma
Wakaguzi wa Wakala wa Mbolea (TFRA) ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Saidi Mwambungu wakijitambulisha na kueleza madhumuni ya safari yao ya kikazi mkoani Ruvuma.
Wakulima wanapodanganywa kuhusu mbolea
Hivi ndivyo wakulima wanavyodanganywa. Mbolea imewekwa kwenye mifuko yenye maandishi ya lugha isiyo ya kawaida. Kwa vyovyote vile hiki si kiswahili wala kiingereza pengine unaweza kusema ni Kichina. Ni aina gani ya mbolea, hufahamu. Matumizi yake je? Hatufahamu. Hivi ndivyo wakulima wetu wanavyodanganywa. Na haya ni mojawapo wakala wa mbolea (TFRA) imegundua katika ukaguzi wake wa maduka yanayouza mbolea mkoani Ruvuma mapema mwezi Juni.
Utafiti wa mbolea aina mbalimbali kwa zao la mahindi
Watafiti hapa nchini wanaendelea na utafiti wa matumizi wa aina mbalimbali za mbolea kwa zao la mahindiJaribio la Mbolea ya TSP pamoja na UREA
Jaribio la mbolea ya DAP na UREA
Utafiti wa mbolea ya Minjingu Hyper pamoja na UREA
Jaribio la mbolea ya Minjingu mazao na Urea
Urea pekee kwenye mahindi
Kulima mahindi bila kuweka mbolea Je?
Katika majaribio haya mtafiti atashauri ni aina gani ya mbolea itumike katika udongo wa aina fulani kwa ajili ya zao la mahindi kutokana na matokeo aliyoyapata. Kwa kawaida utafiti huu ufanywa kwa zaidi ya msimu mmoja.
Mbolea kwenye rambo ! Haiwezekani
Ndivyo alivyokuta CEO wa Tanzania Fertilizer Regulatory Agency Dkt. Suzana Ikerra wakati wa ukaguzi wa maduka yanayouza mbolea mkoani Ruvuma. Kuna sehemu alikuta mbolea imefungwa kwenye vifuko vidogo vyepesi na vyeusi vya rambo. Wauzaji wakidai wanauza mbolea ya 'Sulphate of Ammonia' (SA)! Hii haiwezekani hata kidogo mbolea kuuzwa kwenye mifuko ya rambo. Kuna athari nyingi kwa kufanya hivyo baya zaidi hata wakulima hawana uhakika na bidhaa wanayouziwa matokeo yake mbolea hiyo ikitumiwa mashambani inaweza kutoa matokeo yasiyotarajiwa kama vile kuunguza mimea.
Monday, July 16, 2012
Mitindo hiyo!
Kama unataka kufahamu mitindo iliyopo kwenye chart basi hudhuria shughuli mbalimbali utapata uipendayo.
Baadaye walijimwaga uwanjani
Mama Banzi akizirudi
Mama Ngahulira naye alikuwa mstari wa mbele kutaka kuzirudi ngoma akikumbuka enzi zake.
Wake zetu
Kutoka kushoto Mrs Ngahulira (mke wa marehemu Thomas Ngahulira) na Mrs Banzi (Mke wa Banzi wa Moro). Marehemu Ngahulira alikuwa rafiki yangu,mfanyakazi mwenzangu na tulikuwa tukifanya kazi kwenye chumba kimoja na wote tulichagua 'black beauties' mnazoziona pichani. Karibu miaka 20 sasa lakini bado wamo.
Mama na Mwana
Deogratias Lwezaura akizngumza na mama yake mzazi (wa kwanza kulia) wakati wa hafla ya kumpongeza binti yao Linda Lwezaura nyumbani kwao Mtoni Kijichi tarehe 8/7/2012
Banzi wa Moro alikuwepo
Banzi wa Moro katika miondoko ya 'gospel songs' kwenye mnuso wa Linda Lwezaura nyumbani kwao Mtoni Kijichi-DAR
Friday, July 13, 2012
Karibuni wageni
Bw na Bibi Deogratias Lwezaura wakiwakarisha wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya kumpongeza binti yao Linda aliyepata Sakramenti ya Kipaimara tarehe 8/7/2012 katika Parokia ya Mtoni Kijichi-Temeke, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.
Tuesday, July 3, 2012
Hakuna sababu ya kununua samani kutoka nje
Samani inayopakwa 'vanish'imetengenezwa na mdogo wangu Macarios Banzi (hayupo pichani). Ametumia mbao za bei rahisi lakini kwa ubunifu zinaonekana kuwa nzuri. Hizi ndizo samani zilizopo kwenye sebule yangu. Ni mwaka wa tatu sasa natumia samani hizi na bado ni imara. Kwa nini tununue samani kutoka China?
Mhandisi Saidi Jambuya
Saidi Mohamed JAMBUYA (aliyevaa fulana ya njano) ni mmoja wa Wahandisi wa Kilimo katika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.Mhandisi Saidi Mohamed Jambuya. Huyu ni mzaliwa wa Kiroka, Morogoro Vijijini. Kwa sasa ndiye anayesimamia shughuli za uhandisi kilimo mkoa wa Morogoro anajua ni mashine gani zinafaa kwa aina ya udongo wa sehemu mbalimbali na mazao mbalimbali na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 ameshariki katika shughuli mbalimbali zinazohusu mashine za kilimo. Pichani akiwa katika maonyesho ya wakulima kwenye viwanja vya Nane Nane mkoani Morogoro.
Amewahi kikaoni
Watanzania tuna tabia isiyoridhisha ambayo inatakiwa tujirekebishe haraka sana. Tabia ya kuchelewa kwenye mkutano,sherehe, kazini siyo tabia nzuri. Utakuta wachache wamewahi lakini wengi huchelewa tena inawezekana hata zaidi ya masaa mawili! Pichani Dada Ghana Kunambi kushoto amewahi,akiwa na mwenyeji wa kikao cha Africana Dada Editruda nyumbani kwake Buguruni.Wengine wako wapi? Kwa Dar Es Salaam kama umeambiwa kikao ni saa 6.00 mchana anza kusafiri kuanzia saa 4.00. Ni heri kuwahi kuliko kuchelewa. Dar vurugu ni nyingi, traffic jams pia kuna weza kutokea tukio ambalo hukulitegemea likakuchelewesha. Kumbuka sababu na samahani nyingi sana mara nyingi haziwasaidie wengine sana sana unaendelea kupoteza muda tu. Kumbuka kuchelewa ni gharama!
Huyu ni uncle 'Junior'
Monday, July 2, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)
