Friday, August 3, 2012

Wajumbe walikagua vyoo

Kazi ilianza mara moja. Baada ya kikao wajumbe wa Bodi wakiongozwa na Mwenyekiti Bw. Bakari Chande walikagua vyoo.

Bodi ya VSS-Kikao cha I

Tarehe 30/6/2012 Bodi ya Vikindu Secondary School ilikaa kikao chake cha I na kumchagua Bw. Bakari Chande kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi. Mambo makuu yaliyozungumzwa katika kikao hicho ni kuhusu miundo mbinu ya shule hasa ubovu wa vyoo, upungufu wa viti na madawati kwa wanafunzi,mimba kwa wasichana na utoro sugu. Kuhusu tatizo la ubovu wa vyoo, wajumbe kwa pamoja waliamua kuchangia sh. 20,000/- kila mmoja na kuazimia kuitisha kikao na watendaji wa vijiji wa Kata ya Vikindu kuzungumzia matatizo yanayoikabili shule ya Sekondari Vikindu.

Wajumbe wa Bodi ya Vikindu Secondary School (VSS)

Hawa ni baadhi ya Wajumbe wapya wa Bodi ya VSS wakiwa katikam picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha I cha Bodi

Vikindu Secondary School

Hii ndiyo shule ya Sekondari Vikindu iliyoko wilyani Mkuranga katika kijiji cha Kisemvule

Kiatu cha harusi

Kiatu cha harusi bado kipo, koti la suti ipo, shati bado lipo isipokuwa suruali inabana sana. Samahani, watoto wameniibia gidamu za kufungia viatu ndiyo maana nimefunga kwa gidamu nyeusi!

Chakula cha miaka 15 ya ndoa

Wali, nyama, mchicha,njegere pamoja na bia kidogo

Banzi-Miaka 15 ya Ndoa

Jana tarehe 2/8/2012 ni kumbukumbu ya kubariki ndoa yetu mimi na mkewe wangu Nancy Ireneus Mbawala
.Ni miaka 15 imepita sasa.Kumbukumbu zinaonyesha bajeti ya sherehe za harusi yetu mwaka 1997 ilikuwa ni Tsh 830,000/-. Nawashukuru wote walioshughulika kwa ajili yetu. Tunamshukuru Mungu.

Matukio-Kipaimara cha Linda Lwezaura

Bi Linda Deogatias Lwezaura (kushoto) akiwa na mpambe wake
Watoto walikaribishwa.
Masista walialikwa.
Msosi wanguvu.
Miondoko ya mshehereshaji (mc)
Msosi kwa Linda na mpambe wake.
Dr. Julius Mwanandota akiserebuka.

Thursday, August 2, 2012

Raha ya vijijini

Mkutano unafanyika chini ya kivuli cha mti. Hapa ni wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa

Chips zinaanzia hapa

Huwezi kupata chips bila kulima viazi mviringo. Chips zinaanzia kwenye kilimo.

Kilimo cha umwagiliaji - Mtazamo

Mbuzi wadogo

Mbuzi wakiwa wadogo wanapendeza sana. Hukimbia huko na huko. Kwa kifupi ni watundu. Mbuzi wakifugwa kitaalamu hutoa nyama choma nzuri na hata maziwa, hivyo kuboresha lishe na kipato.Pale inapowezekana fuga mbuzi.

Wanasubiri mafunzo ya ziada

Elimu popote. Banzi wa Moro aliwanyaka wanafunzi hawa wa Kisemvule Shule ya Msingi wakisubiri mafunzo ya ziada a.k.a tuition

Na hii ndiyo Mbagala Rangi 3

Mbagala Rangi 3- Picha imechukuliwa kutoka kwenye kighorfa cha Huduma Bar (Kwa wale wanaoifahamu Mbagala Rangi 3)

Uwanja wa Taifa

Manispaa ya Temeke imebahatika kuwa na viwanja vikuu viwili vya michezo. Uwanja wa Taifa na Uwanja wa UHURU. Vyote vimejengwa katika sehemu moja.Picha inaonyesha lango kuu la Uwanja wa Taifa (NATIONA STADIUM).

Wednesday, August 1, 2012

Mazingira ya mkoa wa Morogoro

Mkoa wa Morogoro una mazingira tofauti tofauti.Kuna sehemu za vilima vilima na sehemu za mabonde. Kuna sehemu za baridi kali na sehemu za joto kali.Pichani ni sehemu ya bonde na mlima unaoonekana kwa mbali.

Sekondari ya Magereza Ubena

Sekondari ya Magereza Ubena imejengwa katika maeneo haya, miti mingi imeoteshwa hivyo kutoa mazingira mazuri ya kujisomea.

Chai kwa magimbi

Siku hizi migahawa mingi na mahoteli mjini Morogoro huuza vitafunwa vya magimbi kwa kifungua kinywaji. Pichani wateja wakipata chai kwa magimbi na mihogo bila kusahau supu!

Ghala la mchele - Moro

Hili ni moja ya maghala mengi binfasi ya mchele yaliyotapakaa mjini Morogoro. Mwezi Julai mwaka huu kilo moja ya mchele iliuzwa kwa sh1500/= wafanyabiashara wanabashiri kuwa hali ya upatikanaji wa mchele haitokuwa nzuri kwa mwaka ujao huenda bei ikapanda sana.

Ametoka Bungeni

Mmoja wa wataalamu wa Wizara ya Kilimo Bw. Sarema wa Idara ya Uendelezaji Mazao akitokea Bungeni Dodoma mwezi Julai 2012 akifanya mazoezi pale Dumila akiwa njiani kuelekea Dar.