Thursday, August 23, 2012

Vichwa vya ASARECA

Dr. Fidelis A.Myaka (kulia) - Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika akifuatilia kwa makini mada inayozungumzia masuala ya utafiti kwenye moja ya mikutano ya ASARECA.

Macho yote kwenye aina ya mahindi inayovumilia ukame

ASARECA inawawezesha watafiti kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati ili kuweza kufanikiwa kupata aina ya mbegu ya mahindi inayovumilia ukame. Mtafiti Micah Songaleli (pichani)kutoka Tanzania ni mmoja wa watafiti hao
(Picha kwa hisani ya Jarida la The AgriForum-ASARECA - May -October 2012)

Mbegu mpya za mtama kupambana na Kiduha

Kwa muda mrefu watafiti wamekuwa wakipambana na gugu chawi au kiduha linalodhuru zao la mtama. Kupitia ASARECA watafiti wako tayari kupata aina mpya za mbegu za mtama zitakazokuwa na nguvu kinzani dhidi ya gugu hilo.
(Picha kwa hisani ya Jarida la AgriFORUM - ASARECA May-October 2012)

Madhara ya ' climate change'

Angalia jinsi mbuzi wanavyopata taabu ya maalisho. Kisa ni mabadiliko ya hali ya hewa. Ukame, ukame. Hata mtoto anashangaa jinsi mbuzi walivyopanda juu ya mti ili kujipatia chakula.
(Picha kwa hisani ya JARIDA LA agriForum-ASARECA)

Wednesday, August 22, 2012

Ngoma ya asili

Siku ya kilele cha maonyesho ya wakulima mwaka 2012. Waziri Mkuu Mhe. Kayanza Peter Pinda a.k.a M
toto wa Mkulima alitumbuizwa na ngoma ya asili kutoka mkoa wa Tanga

Alama ya ushindi

Kwa mara ya kwanza nikiwa Arusha nilibahatika kulishika kombe la ubingwa wa maonyesho ya Nanenane 2012

Ubingwa

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ilishika nafasi ya kwanza kwa upande wa utafiti na mshindi wa pili kwa ujumla kwenye maonyesho ya Nanenane 2012 kanda ya Kaskazni. Pichani Mkurugenzi wa Utafiti Kanda ya Kaskazini Dr. Mboyi Mugendi akitembeza kombe kwa furaha kwenye viwanja vya Temi-Arusha

Saturday, August 11, 2012

Katibu Mkuu WKCU - Nanenane Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika (WKCU) Bw. Mohamed Muya (mwenye T-SHIRT nyeusi na cap nyeusi)akipata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa vitengo mbalimbali kwenye banda la Wizara kwenye viwanja vya Temi -Arusha wakati wa maonyesho ya Nanenane 2012.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kaskazini Dkt. Lucas Mboyi Mugendi akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu kuhusu teknolojia za kilimo zilizobuniwa na watafiti mbalimbali mbali hasa wa kanda hiyo.
Hapa Katibu Mkuu anapata maelezo kuhusu ruzuku ya pembejeo kushoto kwake (Mwenye cap nyeupe)Mratibu wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kaskazini Bw. Charles Lyamuchai akisikiliza kwa makini.
Katibu mkuu anapata maelezo ya kupambana na visumbufu vya mimea hasa nzige,viwavi jeshi na ndege aina ya 'queleaquelea'
Na hapa Katibu mkuu anapata maelezo matumizi ya aina mbalimbali za mbolea kwenye zao la mahindi na hasa matumizi ya mbolea za kupandia za Minjingu mazao na DAP.
Katibu Mkuu Mawasiliano wakati wote akiwa amezungukwa na maafisa waandamizi wa kilimo wa Kanda ya Kaskazini akiwemo Afisa Kiungo wa Kanda (Mwenye koti jeusi) Bw. Jeremiah Sembosi

Hapa niliuziwa mishkaki na chips

Pembezoni mwa banda la JKT-Oljoro kulikuwa na huduma ya nyama choma, chips, mishkaki na kuku choma. Hapa niliuziwa mishkaki lakini ilibidi niisimamie kwani ukizubaa imeuzwa!

Kuna waliokesha kwenye banda la JKT-Oljoro

Kila mmoja alisherehekea kivyake wakati wa maonyesho ya wakulima 2012.Kwenye banda la JKT Oljoro - viwanja vya Temi, Arusha, pamoja na maonyesho ya vipando,k
ulikuwepo na huduma za vinywaji na vyakula. Naambiwa kuwa kuna waliokesha kwenye banda hilo.

Watoto walitembelea viwanja vya Temi-Arusha

Wazazi wenye mapenzi ya kilimo hawakuwaacha watoto wao nyumbani. Waliwachukua hadi viwanja vya Temi jijini Arusha kuangalia maonyesho ya wakulima 2012 maarufu Nanenane

Unaweza kuhifadhi kilo 400 za nafaka

Wadudu waharibifu hashanbulia mazao hata yakiwa shambani. Teknolojia nyingi zimebuniwa kudhibiti wadudu hao kama vile vifukusi na 'scania' wasishambulie mazao kwa kutumia madawa na njia nyinginezo. Lakini teknolojia hii ya ghala linalohamishika linaonekana kuleta ahueni kwa wakulima. Watafiti wa Kituo cha Utafiti Selian kanda ya Kaskazini wakishirikiana na CIMMYT wameanza kusambaza teknolojia hii kwa wakulima. Ghala la aina hiyo huuzwa kiasi cha shilingi 140,000/-. Ghala hili limeonekana kuwavutia wadau wengi kwenye maonyesho ya Nanenane 2012 katika viwanja vya Temi jijini Arusha.

Nzige ni balaa

Nzige ni wadudu aina ya panzi ambao hushambulia mazao yakiwa shambani.Huzaliana kwa wingi na wakitua eneo la majani mabichi hushambulia kila kitu. Kupambana na nzige ni kazi rahisi zinahitaji umaja wa kimataifa kwani wadudu hawa huruka bila ya mipaka wanaweza kuzaliana Kenya na kutua Tanzania au Kongo na kuja kuharibu mazao nchini Tanzania. Kwenye maonyesho ya Nanenane 2012 kanda ya Kaskazini jijini Arusha,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ilikuwa na sehemu ambayo wataalamu wake walikuwa wanaelezea masuala ya nzige na jinsi Serikali inavyopambana na wadudu hao waharibifu.

Friday, August 10, 2012

Queleaquelea kiwanjani Themi-Arusha

Ndege waharibifu wa mazao aina ya nafaka wajulikanao kwa jina la queleaquelea waliletwa kwa maonyesho kwenye banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika-Kanda ya Kaskazini viwanja vya Themi.Ili Wakulima na wadau wengine wa kilimo wawatambue na kuelimishwa madhara yake na jinsi ya kuwadhibiti wasiharibu mazao ya nafaka yakiwa shambani.

Nilifurahishwa na huduma za TTCL

TTCL ni kampuni kongwe ya mawasiliano nchini Tanzania. Kwenye maonyesho ya wakulima ya mwaka 2012 kanda ya Kaskazini kwenye viwanja vya Temi Jijini Arusha nilifurahishwa na huduma zao. Hapa niliweza kununua simu ndogo safi kwa bei ya sh 20,000/- na kusajiliwa hapohapo. Niliweza kununua betry charger kwa shilingi 5,000/- kwa simu yangu ya zamani ambao charger yake ilipotea. Pia niligawiwa vipeperushi pamoja na mfuko wa TTCL!

Hai ni zaidi ya bidhaa za shambani

Wilaya ya Hai walijipanga kisawasawa kwenye maonyesho ya Nanenane 2012 kanda ya Kaskazini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Temi Arusha. Wakulima kwenye makundi yao ya uzalishaji walionyesha bidhaa nyingine zaidi ya mazao ya kilimo.

Ngogwe na parachichi

Kwenye banda la Halmashauri ya wilaya ya Hai niliweza kujionea nyanya chungu (ngogwe)na parachichi na mazao mengine haya ni maonyesho ya wakulima mwaka 2012 Kanda ya Kaskazini

Bilinganya la Nanenane 2012 Kanda ya Kaskazini

Kwenye banda la maonyesho Manispaa ya Jiji Arusha moja ya kivutio ni bilinganya kubwa!

Friday, August 3, 2012

Ukiuliza nyodo utajibiwa nyodo

Eti yamepimwa angaza!

Na baadaye kukagua mipaka ya shule

Baada ya kukagua vyoo na kukuta viko katika hali mbaya sana. Ilibidi pia kukagua mipaka ya shule kwani tayari uvamizi wa eneo la shule umeshaanza.