Sunday, July 7, 2013

Msalaba mbele

Imani yangu ni kwa KRISTO mfufuka.

Niko kazini

Nikiwa kazini sina masihara. Uzalendo unaonekana kwenye kofia niliyoivaa. Hapa nakagua majaribio ya utafiti wa mpunga kwenye kituo cha Utafiti KATRIN-Ifakara mkoani Morogoro.

Raha jipe mwenyewe

Nikiwa nyumbani huwa napumzika nakupata 'lager' yangu- Kilimankaro

Tunavyotapeliwa na wachungaji feki

Vijana wa Dekania ya Kigamboni walionyesha igizo linaloonyesha jinsi watu wanavyotapeliwa na wachungaji katika uponyaji. Ona jinsi watu walivyoanguka chini wakimaanisha kuwa wametolewa pepo!

Vipaji vya Vijana

Vijana wa Dekania ya Kigamboni wakionyesha umahiri wao wa kucheza muziki wakati wa tamasha la vijana lililofanyika parokiani Vikindu tarehe 30/6/2013

Ngongoti Je?

Vijana wa Parokia ya Vikindu waliandaa ngongoti wakati wa tamasha la vijana dekania ya Kigambani lililofanyika tarehe 30/6/2013 parokiani Vikindu.

Hili si gari lao

Watoto wanapenda gari ingawa si mali yao.

Padri Moses a.k.a Musa

Padri Musa (katikati)Mlezi wa Vijana Dekania ya Kigamboni ndani ya Kanisa la Parokia ya Vikindu tarehe 30/6/2013 siku ya tamasha la Vijana Dekania ya Kigamboni.

Watoto na Birthday!

Birthday ya Joseph Julius Mwanadota (Katikati) wengine ni wapambe tu. (Picha na Catherine Banzi)

Ilipo St. Joseph University

Bango hili linaonyesha mahali ilipo St. Joseph University jiji Dar nchini Tanzania(Picha na John Banzi)

Friday, July 5, 2013

Kutoka Jumuiya Ndogondogo

Mwanangu Sisty akitoka kusali kwenye Jumuiya ndogondogo akiwa katika baskeli yake.

Mkwe ndani ya daladala

Daladala za Kisemvule hazina shida, hakuna kubanana inaingia basi na kutoka basi kama vile uwanja 'Skipor'airport ya Amsterdam.

Bodaboda na vijana

Pamoja na kuleta ajali nyingi lakini kwa vijana bodaboda inawaingizia mapato. Watengenezewe utaratibu maalumu wa mafunzo kwa bei nafuu kupunguza ajali.

Vijana na biashara

Vijana wa Kisemvule wakiuza machungwa kwenye kituo cha mabasi kijijini Kisemvule.