Wednesday, July 17, 2013
Ufunguzi wa Kituo cha Utafiti KATRIN -Ifakara
Kituo cha Utafiti wa Kilimo KATRIN kilichopo Ifakara kimefunguliwa rasmi tarehe 22/3/1970 na Baba wa Taifa Mwl. J.K.Nyerere saini yake inapatikana katika kitabu cha wageni cha kituo hicho. Hakika ni kumbukumbu nzuri.
Vifaa vya umwagiliaji katika shamba la utafiti Ilonga
Mhasibu Mwandamizi Christopher Gibbson wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika akishangaa mabomba ya umwagiliaji katika shamba la utafiti Ilonga.
Shambani Lumemo - Ifakara
Toyota-Landcruiser, gari hili linafaa sana kwa shughuli za shambani kama vile za utafiti kilimo. Bw . Omari Kizito na Shuhu Jr wamekuwa wakiendesha gari la aina hii wakiambatana na watafiti vijijini. Hapa wapo kwenye shamba la Utafiti KATRIN katika mto Lumemo-Ifakara.
Utafiti wa zao la mtama na alizeti kituo cha Utafiti Ilonga
Utafiti wa alizeti na mtama umeandelea kufanywa kwa miaka mingi katika kituo cha utafiti Ilonga. Matokeo mazuri yamepatikana kama vile mbegu bora zinazozaa kwa wingi zinazovumilia ukame na magonjwa.
Ushindi ARI-Ilonga
Vikombe vilivyonyakuliwa na kituo cha Utafiti Ilonga ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki.
Friday, July 12, 2013
Utafiti wa mtama kituoni Ilonga
Maelezo kutoka kwa watafiti wa mpunga Cholima-Dakawa
Teknolojia za kilimo cha Kichina kituo cha Dakawa
Mtaalamu wa Kichina wa kituo cha teknolojia za kilimo za Kichina akiwaonyesha wajumbe wa timu A ya kupelemba na kutathmini kanda ya Mashariki mwaka 2013 plot ya maonyesho ya vitunguu.
Pepeta za Ifakara!
Pepeta nazo ni tamu - kwa kiingereza zingeweza kuitwa 'Rice flakes' ni sawa kabisa na corn 'flakes'Nilipofika kwenye kivuko cha mto Kilombero nilinunua pepeta kiasi cha kilo tatu kwa gharama ya Tshs 4,500/=.
Monday, July 8, 2013
Daraja la mto Ruaha
Hapa ni Kidatu lilipo daraja la mto Ruaha si mbali sana na mahali panapozalishwa umeme kwa nguvu ya maji. Tegemeo la nishati hapa nchini.
Sunday, July 7, 2013
Mtafiti kijana wa Ilonga
Mtafiti kijana mwanamke
Watumishi wa misa
Masista wakipata msosi
Manjonjo ya ngongoti
Subscribe to:
Posts (Atom)