Monday, November 10, 2014
Huwezi kuwakataza watoto wa familia
Watanzania tumekuwa na tabia mbaya ya kuandika kwenye kadi kuwa watoto hawaruhusiwi kwenye hafla za harusi na sendoffs. Lakini huwezi kuwakataza watoto wa familia. Watajifunzaje kushughulikia matukio haya muhimu wakati tunawakataza? Pichani watoto wa Familia ya Mbetwa wakiwa ukumbini siku ya harusi ya baba yao mdogo Mpoki. Angalia jinsi wanavyoburudika na soda!
Violet msanii mwenye sauti nyororo
Kama ungeisikia sauti ya Violet(aliyeshika microphone) akiimba moja ya wimbo wa marehem Whitney Houston ungeamini kuwa Whitney amefufuka! La hasha huyo ni Violet mtoto wa Kinyakyusa aliyekuwa akiwatumbuiza wageni waalikwa na maharusi wakati wa reception ya Bw & Bi Mpoki Mbetwa ndani ya Marantha Hall- Msimbazi jiji Dar. Msichana huyu ana kipaji kikubwa cha uimbaji nangojeea single yake ya kwanza!
Barabara ya Kawawa inaandaliwa kwa mabus ya kwenda kasi
Hapa ni Magomeni QTR jijini Dar. Ujenzi wa barabara ya Kawawa kwa matumizi ya mabus ya kwenda kasi unaendelea. Kituo cha mabus hayo kimeshajengwa. Mbele yake linaonekana jengo la Kanisa Katoliki Parokia ya Magomeni lililokarabatiwa.Ndani ya jengo hili Bw na Bibi Innocent J.Banzi walifunga ndoa yao mwaka 1997.
Magomeni Mapipa jana
Magomeni Mapipa nilivyoikuta jana jioni baada ya ujenzi wa barabara ya mabus ya kwenda kasi. Wakati ule sisi tunaishi pale Magomeni Qtrs hapa Mapipa hakukuwa na ghorofa hata moja. Wakati tunakwenda Jangwani kuangalia mazoezi ya Simba na Yanga tulikuwa tunakatiza hapo juu. Dar Es Salaam na vitongoji vyake inabadilika kwa kasi ya ajabu!
Subscribe to:
Posts (Atom)