Tuesday, December 2, 2014

Mawe ya saruji

    Mawe ya kutengeneza saruji yanapatikana kwa wingi mkoani Lindi. Pichani mawe     yamekusanywa  kando ya barabara kuu ya Dar-Mtwara tayari kusafirishwa kwenda kwenye viwanda vya saruji Dar Es Salaam.

Chama chao 'CUF'

Bendera nyingi za chama cha CUF zimesambaa mkoani Lindi. Hii maana yake chama hiki kimejijenga na kueleweka sana mkoani Lindi.Kwa vyama vingine inabidi kufanya kazi ya ziada 'kuipiku' CUF.

Engine nyuma limekufa!

Wengi wanazungumza kuwa kwa mazingira yetu magari yenye engine nyuma hayadumu kwa muda mrefu. Bus hili lenye engine nyuma limekufa kando ya barabara Dar-Lindi

Dar-Mtwara madaraja mengi



Ujenzi wa barabara ya Dar-Lindi umegharimu fedha nyingi sana. Changamoto kubwa ilikuwa ni katika ujenzi wa madaraja hasa katika mkoa wa Pwani na Lindi.

Satelite dish ipo

Hapa ni moja ya kijiji katika mkoa wa Lindi kando ya barabara ya Dar-Lindi-Mtwara wakazi wa hapa wanapata habari, wanaburudika na kuona matangazo ya michezo hasa mashindano ya mpira wa miguu duniani.

Alijaribu kujenga ghorofa!

Ni kweli  alitaka kuishi ghorofani. Lakini  sote tujiulize ghorofa hiyo ni imara?

Kitu hicho kijijini Lindi

Kandokando ya barabara ya Dar-Mtwara huwezi kuamini vitu vinavyochomoza (nyumba). Hiki kitu kiko kwenye kijiji kimoja mkoani Lindi. Watakaosoma kurasa huu na waliobahatika kusafiri kwa barabara hii wanaiambie nyumba hii iko kwenye kijiji gani?

Yamehamia kusini





Mabus ya kisasa yamehamia kusini na ni mashindano kwelikweli  barabarani. Haya ni matokeo ya barabara nzuri ya kutoka Dar -Mtwara

Dar-Mtwara-Makazi yameanza kuboreshwa



Ukisafiri kwa gari kutoka Dar kwenda Mtwara kando ya barabara ujenzi wa nyumba bora na za kisasa unaendelea

Matengenezo ya barabara sehemu za Ndundu

   Hiki ni kipande cha barabara ambacho hakijakamilika sehemu ya Ndundu

Hapa bado

   Harakati zimeanza kuboresha makazi ya kijiji hiki

Miwa ya Ikwiriri ni mitamu


Sehemu ya kujidai Ikwiriri


Ofisi ya mabus ya Afif - Ikwiriri



Kituo cha mabus Ikwiriri


Mafundi baiskeli bado wapo

 Baiskeli ni chombo cha usafiri kinachotumika katika  vijiji vingi hapa nchini. Nilipokuwa Ikwiriri nilishuhudia fundi huyu akirekebisha baiskeli ya mteja.

Bus la Afif likijiandaa kwa safari ya Dar kituoni Ikwiriri


Kifungua kinywa Ikwiriri

Moses Baynga akinawa mikono kabla ya kupata kifungua kinywa

Dereva wetu Omary Kizito akifanya mawasiliano

Ukitaka milango na madirisha fika Ikwiriri


Barabara ya Dar-Mtwara lami zimebaki km 6




Ukisafiri kutoka Dar kwenda Mtwara unakanyaga lami  kwa asilimia 98. Sasa zimebaki takribani kilometa 6 kukamilika. Banzi wa Moro ameshuhudia akiwa katika safari ya kikazi mkoani Mtwara hivi karibuni. Tukiwa njiani tulishuhudia  mabus ya kisasa ya kisafiri kwenda Mtwara, Lindi,Masasi,Nachingwea, Tandahimba, Kilwa na Ruangwa. Kweli Mtwara Lindi kuchele!