Friday, June 3, 2011

Na hapa ni Ruangwa


Royal Pub ni mahali pa zuri pa kupata chakula na kinywaji ukiwa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi. Ilibidi nipige picha. Ruangwa bomba sana!

Wachaga kwa nyama!


Watafiti kutoka ARI-Naliendele,kushoto ni John Tenga na kulia Dkt. Peter Masawe wakitafuna nyama ya mbuzi. Huku wakidai leta huku kisusio! Wapi huko? (Toa jibu)

Hii siyo gari yetu.



Mbona haina namba! Anashangaa Omary Shomari dereva wa gari STH 5470 (Haisomeki)Toyota Double Cabin. Hii ni baada ya kumaliza kilometa 60 za Somanga Ndundu tukitokea Mtwara tarehe 1/6/2011. Kipande hicho cha barabara ni kichafu kweli kweli

Maelezo ya ziada kutoka kwa mtafiti


Ilibidi tupate maelezo ya ziada kuhusu Cashew Development Centers (CDC) kutoka kwa mratibu wa Utafiti wa Korosho Dkt. Peter Masawe tulipotembelea CDC-Nanyanga-Tandahimba.

Ufuta kwa wingi Lindi


Mkoa wa Lindi ni moja kati a mikoa inayozalisha kwa wingi

Mwache mkulima ajieleze


Utafiti shambani kwa wakulima. Huko Mtama, Lindi kikundi cha wakulima kinafanya utafiti wa zao la embe. Pichani mkulima mwanamama akijieleza.Tulimsikiliza na kumuuliza maswali na alitujibu barabara. Kijiji hiki kimo ndani ya jimbo la Mh. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Huyo ni nani?

Ni mtafiti wa raslimali ya udongo Bw.John Tenga wa ARI-Naliendele, Mtwara. Mara tu aliposhuka kutoka garini alielekea moja kwa moja ofisi za kituo cha Utafiti Mkumbwa, Nachingwea

Watafiti wanasubiri kwenda Kilwa vijijini


Kushoto n mtafiti wa mbegu za mafuta Bi. Joan Kasuga na kulia ni Mratibu wa Utafiti wa Korosho nchini Tanzania, Dkt Peter Massawe wakisubiri kwenda vijijini Kilwa kukagua shughuli za utafiti.

Sahani yenye chapati ni ya nani?


Mambo ya Kilwa hayo. Breakfast chapti na supu ya kuku

Taxi za Kilwa babu kubwa



Ukiambiwa kwenda kufanya kazi Kilwa Masoko utafikiri kama umepewa adhabu. Huo ni mtazamo wa zamani. Mwisho wa mwezi huu nilikuwa Kilwa Masoko kikazi. Kilwa mambo ni kama hivi:-

-hakuna kukatika umeme (umeme wa songas)
-magari aina ya Noah niyo Taxi zao (Kilwa- Nangurukuru)
-Samaki ndo usiseme (wa kukaanga,supu au wa kuungwa)
-wali kwa nazi
-kuku wa kienyeji!
-Guest bei poa na ni self contained
-beach safi
-Ulabu kama Dar tu

Baiskeli Kilwa

Nilipotembelea Kilwa Masoko hivi karibuni nilivutiwa na baiskeli hii. Kilichonishangaza zaidi ni kwamba baiskeli hii ilinunuliwa kwa bei ya Tshs 60,000/= ! Kilwa kumekucha.

Pengo na Mapadre


Hii ni picha ya ukumbusho.

Watoto wa utatu walitoa burudani



Walijiandaa, walitoa burudani, walifurahisha. Yote ni kwa kumtukuza MUNGU.

Tufunge zawadi


Zawadi hazikukosekana. Hilo furushi ni zawadi za Padri Fortunatus Oscar Banzi. Asante kwa wote waliotoa kwa mapenzi mema.

Hongera Banzi


Ndivyo walivyosema Baba Mdogo George Mdoti (kushoto) na mdogo wake Jakka (kulia). Waliokuwepo kanisani kushuhudia tendo la kihistoria.

Vituo vya Radio vilikuwa hewani



Katika tukio la upadrisho jana.Radio Tumaini na Radio Maria vilitoa matangazo ya moja kwa moja.Picha ya Chini mtangazaji wa Radio Tumaini akiwa hewani na juu Radio Maria.

Mapadri walitoa Baraka



Tarehe 2/5/2011 waumini walifurika katika Kanisa la Maxmillian Kolbe kushudia upadrisho wa Mapdre wa tano uliotolewa na Mhashamu Kardinali Polycarp Pengo. Mapdri walitoa baraka kwa waumini

Mwili wa Kristu


Padre F.Banzi anakomunisha

Anavalishwa Joho la Kipadri


Nikuvalishe joho la Kipadri (Linaitwaje?)

Mapadri kifudifudi


Inaposomwa Latania ya Watakatifu. Mapadri hulala kifudifudi wakisali na kuomba.