Tuesday, November 5, 2013

Nashangaa barabara ya Dumila -Mikumi

Nikiwa kijijini Mvumi, Kilosa nilipata fursa ya kuvinjari kando kando ya barabara mpya inayojengwa kutoka Dumila hadi Mikumi kwa kiwango cha lami!

Banzi wa Moro msibani Mvumi-Kilosa

Niko msibani  kijijini Mvumi, Kilosa, Morogoro tarehe 3/11/2013. Kutoka kushoto Prosper Mloka, Mwl. Aniani Kobelo na Kaka George Mdoti wa Ifakara.

Kaka George Mdoti msibani

  Kwenye msiba ndipo mahali ndugu kutoka sehemu mbalimbali wanapokutana. Kaka George Mdoti (Kushoto) na uncle Prosper Mloka tulikutana kijijini  Mvumi, Kilosa Dakawa kwenye msiba wa marehemu Lawrence Mbunda.

Jeneza nje kwa Ibada

Jeneza lilolobeba mwili wa marehemu Lawrence Mbunda likiwa nje tayari kwa ibada ya mazishi kijini Mvumi, Kilosa, Morogoro, tarehe 3/11/2013.

Msibani Kijijini Mvumi

Watu wengi walihudhuria mazishi ya marehemu Lawrence Mbunda yaliyofanyika kijijini Mvumi, Kilosa Morogoro tarehe 3/11/2013.

Akina mama wakipata riziki msibani

Akina mama wakipata chakula kabla ya mazishi ya marehemu Lawrence Mbunda huko kijijini Mvumi, Kilosa Morogoro siku ya tarehe 3/11/2013

Bi.Halima Kihemba akikabidhi rambirambi

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Halima Kihemba akikabidhi rambirambi  yake pamoja na familia kwa mke wa marehemu Mbunda Bi. Angelina Mshana (Catherine) wakati alipohudhuria mazishi ya marehemu Lawrence Mbunda yaliyofanyika kijijini Mvumi, Kilosa, Morogoro tarehe 3/11/2013.

Bi Helmina Mwenda akiaga mwili wa mkwe

Bibi Helmina Mwenda a.k.a Bi Kilemba (Dada yetu mkubwa) akiaga mwili wa mkwewe marehemu Lawrence Mbunda wakati wa mazishi kijijini Mvumi, Kilosa, Morogoro tarehe 3/11/2013

Mtoto anamuaga baba yake

Haamini! Lucy Larence Mbunda akilia kwa uchungu mbele ya jeneza la baba yake Lawrence Mbunda  siku ya tarehe 3/11/2013 kijijini Mvumi. Kilosa, Morogoro  yalipofanyika mazishi.

Ndugu wakiaga mwili wa marehemu Lawrence Mbunda

Si rahisi kuamni kuwa ndugu yako amefariki unapoona mwili wake umelazwa ndani ya jeneza. Ndivyo ilivyokuwa wakati ndugu marehemu Lawrence walipopita mbele ya jeneza lake kumuaga.

Bi Angelina Mshana akilia kwa uchungu

Bi  Angelina Mshana (Catherine) akilia kwa uchungu wakati wa kuombolza kifo cha mmewe Lawrence Mbunda kilichotokea jijini Dar Es Salaam tarehe 1/11/2013

Bi Angelina akiaga mwili wa mumewe

Bi Angelina Mshana akiuaga mwili wa mumewe marehemu Lawrence Mbunda aliyefariki tarehe 1/11/2013 na kuzikwa kijijini kwao Mvumi, Kilosa Morogoro, tarehe 3/11/2013. AMINA

Jeneza lililobeba mwili wa Lawrence Mbunda

Jeneza la Lawrence Mbunda likipelekwa makaburini kijijini Mvumi, Kilosa, Morogoro tarehe 3/11/2013

Waombolezaji makaburini -Mvumi

Waombolezaji waliusindikiza mwili wa marehemu Lawrence Mbunda hadi makaburini Mvumi kwa mazishi tarehe 3/11/2013

Shada juu ya kaburi

Mke wa marehemu Lawrence Mbunda, Bi.Angelina Mshana (Catherine) akiweka shada juu la kaburi la mumewe kijijini Mvumi tarehe 3/11/2013

Friday, November 1, 2013

Mama Janeth Kahama anakabidhi Rozari

Moja ya zawadi alizotoa Mama Janeth Kahama (pichani) kwa Bw na Bibi Joe Mutahangarwa ni Rozari. Akiwataka wanandoa kusali. Nyumba iwe ya sala katika maisha yao yote wakimtegemea MUNGU.

Bi Daphrosa alikabidhiwa kibuyu

Bi Daphrosa Mutahangarwa alikabidhiwa kibuyu chombo cha kutunzia kinywaji ili mumewe anapochoka apate kutuliza kiu!

Joe alikabidhiwa mkuki

Mila na utamaduni wa Kihaya hazikusahauliwa kwenye tafrija ya harusi ya Bw. na Bibi Joe Mutahangarwa. Pichani Joe anakabidhiwa  mkuki alama ya ulinzi wa kumlinda mkewe!

Thursday, October 31, 2013

Gari la maharusi

Gari lililowachukua Bw & Bibi Joe Mutahangrwa mara baada ya kufunga ndoa Kanisani Vikindu- Tarehe 26/10/2013.

Kampa amapofurahia utamaduni wa kwao

Ukimuona mtu mzima anaingia ndani ya uwanja basi tambua kwamba imemkuna. Pichani Mkurugenzi wa TANDAN FARMS ya Vikindu-Kisemvule Bw. Kampa ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe ya kuwapongeza Bw & Bi Joe Mutahangarwa baada ya kufunga ndoa yao akicheza ngoma ya asili ya  Kihaya.